Jinsi ya kufanya biashara ya FOREX

Post iliyopita ilikuwa na utangulizi muhimu kuhusu FOREX, kama hujaisoma, waweza bofya kiungo kifuatacho kuisoma:
Forex ni nini?

Kama tayari una uelewa wa awali wa biashara hii, bofya kiungo kifuatacho ili ujisajiri na broker anayekubalika zaidi East Africa!

BOFYA HAPA KUJIUNGA

Sasa twende Sokoni. Twende kwa Hatua pia:

1. Forex inafanyika kwa kulinganisha thamani za Sarafu Mbili kwa pamoja (Currency Pairs).
Kule sokoni unapoingia, ili uweze kununu na kuuza, utakuta bidhaa (currency) zimewekwa kwenye mafungu mafungu ya mbili mbili (pairs). Mfano:
i)Euro na US Dollar pamoja,
ii) Paund (GBP) na USD pamoja,
iii) USD na Yen (JPY) pamoja,..nk. nk. nk
Zinavyopangwa, utazikuta hivi:
EUR/USD
USD/JPY
GBP/USD
USD/CAD

Chukua EUR/USD kwamfano;
Hiyo ya mwanzo (EUR) Inaitwa BASE currency, na hiyo ya pili, USD, unaitwa COUNTER Currency. Sasa, bei unazoziona kwenye grafu zikipanda na kushuka ni bei za Base Currency kwa kulinganishwa na Counter Currency. Chukulia hii;

EUR/USD = 1.25358

Maana yake, Euro 1 = 1.25358 USD. Kama unataka kununua EURO 1, utalipa 1.25358 USD.

Bei za Euro sokoni, kwa kulinganishwa na USD, zinaweza kubadilika ndani ya sekunde! Sasa, faida zinapatikana kwa wewe KUNUNUA Currency moja, wakati bei iko chini na KUIUZA wakati bei inapopanda. As Simple as that. Sasa, ili kujua kwamba baada ya muda itapanda ili UNUNUE sasa hivi na uuze itakapopanda, au, kujua kwamba itashuka zaidi ya hapo ilipo ili, UUZE sasa hivi na UNUNUE itakapofika bei ya chini zaidi,...mchakato huo unaitwa MARKET ANALYSIS.

2. Forex Trading, hufanyika kwa "Kubonyeza tu" kitufye cha kuBUY au cha kuSELL. Basi. Hilo tu. Unakuwa umefanya TRADE. Lakini sasa, ili uweze kujua, unabonyeza kipi, muda gani, uTRADE kiasi gani ili upate faida gani, inabidi uwe unajua kufanya MARKET ANALYSIS mwenyewe au uwe na MTAALAMU unayemuamini akufanyie na akupe taarifa hiyo. Sasa, hiyo taarifa ndiyo inaitwa "Fx Signals" au "Trade Signals"..nk.

3. Faida au hasara kwenye Forex Trade zinapimwa kwa PIPS.

PIP ni kitu Gani? Kitefu chake ni "Percentage In Point". Pip ni tofauti ya POINT MOJA katika bei ya Pair ya Currency tokea ulipoweka ORDER yako. Its a 1point Price Movement ama kwenda juu au kuja chini.

Hii tofauti ya bei (Pip) inapimwa katika viwango vya Desimali. Currency Pairs nyingi (sio zote tafadhali) zinatumia SEHEMU NNE ZA DESIMALI. Utakuta kwenye Platform wanaandika SEHEMU TANO lakini ni ili kukusaidia wewe mfanyabiasha, ila zinazohesabika ni NNE.

 Utaelewa vizuri kwenye mfano. Chukulia hiyo ya pale juu:

EUR/USD = 1.25358

Tunaangalia "Price Movement" katika sehemu ya 4 ya desimali. Ile ya tano inakupa tu sehemu ya Pip.

Chukulia hapo bei ibadilike ama kwenda juu au chini kama ifuatavyo:


EUR/USD = 1.25458
                     ⬆️
EUR/USD = 1.25358
                     ⬇️
EUR/USD = 1.25258

▶️ Kutokea 1.25358 kwenda 1.25458 maana yake bei imepanda kwa 10pips.

▶️ Kutokea 1.25358 mpaka 1.25258 bei imeshuka kwa 10pips.

Swali, je kutoka 1.25258 mpaka 1.25200?

Jibu, imeshuka kwa 5.8pips. Sawa mpaka hapo?

Kwa hiyo, FAIDA na HASARA katika Forex zinapimwa kwa PIPS. Ukiwakuta watu wanaambiana, mimi leo nimepata, 30 USD, 50 Yen, 70 Paunds...unajua tu hawa sio professionals. Kule watu wanajisifia Pips sio Dola au Paundi au Yen. Utakuta mtaalam anasema, Mimi ninapata Average/Wastani wa 500Pips, au 700Pips au 1100Pips kwa wiki au kwa mwezi, nk. Sio Dola! Na mtaalamu anayependwa na wateja,..Anayeaminiwa kwamba anao uwezo wa Market Analysis mzuri ni yule anayejikusanyia PIPS nyingi mwisho wa siku.

Swali: Je, naweza kupata PIPS kidogo na nikawa na faida KUBWA kuliko aliyepata PIPS nyingi kunizidi?

Jibu: Ndio. Inawezekana! Lakini, wooote, tutakujua kwamba huna PROFFESSIONALISM bali umeRISK sana na ungeweza ukapoteza hela nyingi sana pia! Sema tu bahati yako leo. Hakuna mtu mwenye hela zake atakayekuamini tukikujua hivyo. Nitaeleza zaidi hili sehemu inayofuata.

5. Nini Thamani ya PIP moja? Ili nijibu hili swali, kuna maelezo lazima nikupe. Ila kwa kifupi, thamani ya PIP moja inaweza kuwa ni 10 USD, au 1 USD, au 0.1 USD. Angalia:

Kumbuka, hii ni biashara kubwa sana. Kule kwenye soko la dunia, CURRENCY zinauzwa kwa jumla. Huwezi kwenda kununua eti Dola 1, au Paundi 5 au Euro 8. No. Unanunua kwenye mafungu! Kule kuna mafungu matatu tu maalum yanayouzwa:

a) 100,000 USD, au
b) 10,000 USD, au
c) 1,000 USD

Kwani hata Buteau de Change si wanauza kwa mafungu? Utakuta;

1 - 50 USD bei yake
51- 100USD bei yake
101- 1000USD bei yake
N.k. nk, nk..ndo ivo ivo kule.

Sasa,..

Wale waliosoma Science Sekondary mnikumbushe hii: S.I Unit maana yake nini tena? International Standard Unit? Nimesahau. Ila maana yake ni hii. Kipimo maalum kilichokubalika dunia nzima kupimia kitu mfano;
Urefu, S.I.Unit ni Meter
Ujazo, S.I.Unit ni Litre
Uzito, S.I.Unit ni Gram
N.k, n.k,...

Sasa kwenye Forex, kipimo kilichokubalika kupimia kiwango cha MAFUNGU ya kuuza na kununua Currency kinaitwa "Lot" Tumezoea kuita, "Standard Lot".
➡️ Lot moja ukiigawa kwa KUMI utapata 1 Mini~Lot.
➡️ Mini~Lot moja ukiigawa kwa KUMI (au Standard Lot moja ukiigawa kwa MIA) unapata 1 Micro~Lot.

Angalia sasa;

1 Std Lot = 100,000 USD,
1 Mini~Lot = 10,000 USD
1 Micro~Lot = 1,000 USD

Nenda kinyumenyume, utaona kwamba:

1lot = 10 mini~lots = 100 micro~lots

Au kwa namna nyingine;

1Micro~lot = 0.1 Mini~lot = 0.01lot.

Sasa, unapokwenda KUPLACE ORDER ya kuBUY au kuSELL kuna sehemu utaulizwa ujaze SIZE ya ORDER yako. Utajaza 1Lot kwa maana ya unanunua au kuuza 100,000USD au utajaza 0.1lot kwa maana ya unauza au kununua 10,000USD au utajaza 0.01lots kwa maana ya unauza au kununua 1,000 USD.

Sasa twende kwenye thamani ya PIP.

Endapo ULIUZA au KUNUNUA "1 Standard Lot", kila PIP moja unayoipata sokoni kama faida, ni sawasawa na 10 USD. Maana yake, kwa 100,000 USD ulizoTRADE, umepata faida ya 1PIP au 10 USD.
Kama uliTRADE 1minilot, 1PIP ni sawa na 1 USD na kama uliTRADE 1 microlot, PIP moja ni sawa na 0.1 USD.

Umenielewa mpaka hapo? Ngoja nikusisitize yafuatayo kama NB.

Note1: Si kila Currency Pair PIP yake inapimwa kwa 4decimal places. Kuna baadhi sio, mfano Currency Pairs ambazo zina Japaneese Yen ndani yake kama EUR/JPY au USD/JPY na zingine, PIP yake moja inahesabiwa katika sehemu MBILI za Desimali. Ukishakuwa sokoni utazizoea tu usiogope. Utazijua zote.

Note 2: Sio kila 1PIP ni sawa na 10USD kwa 1lot. Kuna tofauti zake pia. Baadhi ya currency pairs, 1lot zao, 1PIP utakuta ni 8USD, 11USD au hata 7USD. Inategemea. Ile ya 1Pip = 10 USD ni Standard. Utazielewa pia ukishaingia sokoni. Ila mpaka hapa, unaweza kuelewa kwamba, aliyepata 25pips za 1lot za:
i) EUR/USD,
ii) EUR/JPY, na
iii) GBP/USD
wanatofautiana kwenye hela kwa sababu thamani ua 1PIP kwao zinatofautiana. Ila tofauti zao si kubwa saaana. Zoote, zinakaribi pale pale kwenye Kwa 1std lot, 1Pip = 10 USD.

6. Hivi Kweli, kuna Retail Trader ataweza kununua 1lot, au 1minilot, au hata 1microlot (kiasi cha chini kabisa cha order moja ambacho ni 1000usd = 2.4mil Tzs) na akasavaivu kwenye hii biashara kweli. Huko si ni kubaguana? Wataifanya wenye nacho tu, si ndiyo?

Hapo sasa, ashukuriwe Mungu kuna Mtukati anaitwa Broker. Ndiye anayetuwezesha mimi na wewe tushiriki Forex. Vingenevyo, ingebaki kuwa ni biashara ya Mabenki, Serikali, Taasisi kubwa kubwa za Kifedha ma Matycoon wakubwa.

Kazi kubwa ya Broker ni kukukopesha hela zake ili uzifanyie biashara ya Forex. Atakuambia kwamfano; ukifungua account ya mtandaoni kwangu, uka~deposite hela, kwa kila Dola 1 utakayo~deposite, nitakukopesha Dola 100 au, 200, au 500 au wengine mpaka 1000! Hicho kitendo kinaitwa "Leverage".

Wanaandika hivi:

Leverage:
1:50 (kwa kila dola 1 uyakayoweka kwangu, nakukopeaha 50), au
1:100 (weka 1, kopa 100), au
1:500 (weka 1 kopa 500) n.k, n.k


What is PIP in Forex



Kwamfano sasa, ukiweka USD 100 kwenye account yenye Leverage ya 1:500 maana yake ni nini?

Kwa kila dola 1 uliyo~deposite anakukopesha dola 500. Kwa hiyo, jumla utakuwa na dola 100 x 500 = 50,000. Hiyo inaitwa "Purchasing Power". Hapo maana yake ni kwamba unauwezo sasa wa kununua au kuuza USD 50,000 ambayo ni sawa na 0.5 lot size, tofauti na awali ambapo ungetegemea 100$, usingeweza kuuza au kununua chochote (hata order ndooogo kabisa ambayo ni Micro~Lot = 1000usd).

Brokers wanakuchaji wewe comission wakati wowote unapoTRADE, ndipo kipato chao kilipo. Siku nyingine nitawazungumzia kwa undani kidogo hawa maBroker.

Kama tayari una uelewa wa awali wa biashara hii, bofya kiungo kifuatacho ili ujisajiri na broker anayekubalika na kuaminika zaidi East Africa

BOFYA HAPA KUJIUNGA

Sharing is Caring:


WE LOVE COMMENTS


0 comments:

Post a Comment

Zinazosomwa Zaidi

Followers