Showing posts with label Forex. Show all posts
Showing posts with label Forex. Show all posts

Jifunze Forex: Jinsi ya kutambua supply and demand zones

Supply na demand hizi ni kanda au zone ambazo zinapatikana katika chart ya forex, hizi zone huwa ndio zinazozingatiwa sana na matrader wote wa aina tatu, ambao ni seller buyer na institutions, ambao seller na buyer kwa neno moja tunawaita retailer yani wafanya biashara wadogo wadogo na hao walio kwenye taasisi mbali mbali ambazo zinajihusisha katika biashara hii ndio hao tunawaida wafanya biashara wakubwa na ndio hasa wenye nguvu katika soko hili la forex.

N.B:
Kama ndio unaanza kujifunza biashara ya Forex, unashauriwa kujiunga kwa kutengeneza account kwa broker anayekubalika zaidi Afrika Mashariki:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Ukishatengeneza account yako ya Forex, usisahau ku verify email uliyotumia kutengeneza account pamoja na namba yako ya simu

Tuendelee na somo letu la leo:


Jifunze Forex Kiswahili

Kwa hiyo kwakua wafanya biashara wote huwa wanaheshimu zones(ukanda) basi hii inapelekea uhakika zaidi pindi unapotrade kwakutumia zone, maana ndipo jicho la kila mfanya biashara lilipo duniani kote.

Kama nilivyosema hapo juu kwamba support na resistance huwa hazina utofauti sana na supply na demand kwa kuziangalia kwa macho ila kiufundi huwa utofauti upo tena ni wamuhimu sana na ili utrade hii strategy ni lazima uzingatie utofauti huo, maana usipozingatia huo utofauti utakua umetoka kwenye maana halisi ya supply na demand na unaingia kwenye support na resistance

Utofauti uliopo kati ya demand na supply ukilinganisha na support na resistance ni kwamba support na resistance huwa yenyewe inasisitiza sana kwenye idadi ya candlestick ambazo zinagusa kwenye hizo mistari ya support na resistance huwa kadri inavyogusa Mara nyingi na kushindwa kuvuka upande wa pili wa huo mstari basi ndio uimara wa huo mstari wa support au resistance unavyoongezeka.

Ila kwenye supply na demand hii kitu imekataliwa kabisa na kuna sababu nyingi ambazo zimetolewa zinazofanya hiyo point ikataliwe, huku wanasema kwamba ili zone ya demand au supply iwe imara basi ni lazima iguswe na candle moja mbaka tatu zikizidi hapo basi hiyo si ukanda imara kwahiyo achana nao, sasa wakatoa sababu za kwanini haiwi zone imara ikiguswa na candle ya zaidi ya mbili au tatu...tutaziona hapo chini

Kumbuka haya masomo yote nnayoyatoa hapa ni elimu so ni muhimu na wewe ukapita pita kwenye vitabu ili upate zaidi...nnavyosema elimu namaanisha ni kitu nlichobaki nacho kichwani baada ya kupita pita kwenye vitabu vingi so nenda kaongeze maarifa kwenye vitabu baada ya hapa ili upate mengi ambayo hayapo kwenye elimu yangu ndogo, nikiwa na maana kwamba nimeyasahau.

Sababu ya kwanza ya kwanini supply na demand strategy imekataa kwamba idadi ya miguso mingi kwenye ukanda si uimara wa ukanda huo.

Kwanza tupate picha then tutaenda kwenye sababu moja kwa moja, kama tulivyowahi kusema huko juu kwamba soko huwa linamove up and down na wakati mwingine linakua limekaa kwenye usawa na likiwa linapanda juu huwa tunasema demand wananguvu kuliko supply na likiwa linashuka chini huwa tunasema supply wananguvu kuliko demand na likiwa katika usawa hapa tunasema supply na demand wote wako na nguvu sawa.

Kwahiyo ili soko litembee kwenda juu au kurudi chini ni lazima kuwe na kuzidiana kwa nguvu kati ya demand na supply na endapo wakitoshana nguvu basi soko huwa linakua linafanya haki, yani watakao nunua watanunua sawa na watakao uza.

Kwahiyo kutokana na sababu hii ya kinachopelekea soko litembee juu chini au chini juu, ndio sababu ya kwanza inayopelekea supply na demand kukataa ile dhana ya kwamba eti uimara wa zone unapimwa na idadi ya miguso mingi ya candlestick.

Kwa sababu endapo ukanda utaguswa na candle Mara nyingi hii inamaanisha supply na demand nguvu zao hazina utofauti sana au ndio zinaelekea kwenye uwiano sawa, ila endapo itaguswa na candle moja au mbili then reaction ya kwenda juu au chini ikawa imetokea basi hapo tunasema demand na supply hawako katika usawa na hapo lazima kutakua na pips nyingi sana.

Pia kama hujaelewa hapo njoo kwenye mfano huu mwingine wa kawaida sana tu.

Kwamfano chukua kitenesi kidundishe kwenye sakafu then kiangalie vile kitakwenda juu na kurudi kugonga sakafu then kitakwenda baadae kitapungua kasi na baadae zaidi kitaishiwa nguvu na kitaanza kuroll na hatimae kitatulia sehemu moja...basi hata kwenye zone candlestick zitakwenda zitagusa na kugusa tena na tena na baadae zitatulia hapo kwa muda mwingi bila kushuka sana wala kwenda upande wa pili, so kadri zone inavyoguswa Mara nyingi ndio udhaifu wake unaongezeka.....kwenye mpira ukiruhusu timu pinzani iwe inakuja kwenye himaya yako Mara kwa Mara lazima utafanya makosa tu na utaachia na utafungwa goal so miguso ikitokea mingi itafikia mahali usawa utaonekana na usawa ukitokea basi ukatili utafuata(initiative), hii ndio tofauti ya hao jamaa na ndio maana kuna watu wanasemaga support na resistance haina jipya nlimskiaga mtu aliwahi sema hivi pia na marumbano yalikua mengi mno ingawa sijajua kama na yeye alitumia point hii au alikua na maana nyingine.

Kwa kawaida head and shoulder pattern huwa inakua na mabega mawili la upande wa kushoto na upande wa kulia na katikati ya mabega hayo huwa kuna head.

Kimsingi ili head and shoulder iwe valid kwa kiasi kikubwa ni lazima bega la upande wa kushoto liwe kubwa kuliko la upande wa kulia, ndio ikiwa hivi hapa tunakua na uhakika zaidi kuliko kinyume chake....najua utauliza kwanini sasa iwe hivi?, inakua hivi kwasababu zifuatazo.

Kwa kawaida head and shoulder ili itokee ni lazima kuwa na strong momentum ama kwenye support au resistance na hiyo strong momentum inapelekea support au resistance ivunjwe na price itaenda juu bila kufanya pullback baada ya kuvunja support au resistance itaenda juu kwa umbali flani then itakutana na demand au supply wengi so hao waliofanya hiyo initiative wataingiwa na wasiwasi wataanza kuchukua partial profit na kitendo cha kufanya hivi basi itapelekea retracement kutokea na hii retracement itakua kipimo cha kwanza kwa hao waliofanya initiative wataitumia hii kupima nguvu zao, sasa wataitumiaje kupima nguvu zao, twende tuone huu mfano hapa chini.

Majeshi ya nchi Fulani yanapotaka kuvamia nchi nyingine kwa kawaida huwa mashambulizi yanaanzia kwenye mpaka, so wataweka ngome mpakani then wataanzia hapo kuingia ndani ya hiyo nchi kwa mashambulio ya taratibu, ila pia kuna ile unaingia kwa nguvu zote ili kuwaogopesha zaidi then ukiona nao wamejipanga zaidi unarudi nyuma kuweka ngome kwenye mipaka yao ili watakapokuja wewe uanze kuwashambulia hapo, basi ndivyo ilivyo baada ya kuvunja let say support hawakusubiri pullback wakaingia wakakuta nguvu zao nyingi ila hazina effect kubwa so wanaamua kurudi nyuma kwenye zone wanaweka pending order nyingi hapo na hao wa upande wa pili wakifika hapo wanakua hawana uwezo wa kupita upande wa pili na hapo demand wataichukua hiyo nafasi na kuipeleka price juu kwa kasi coz wataona hao jamaa kumbe ni dhaifu maana wameweza kuwaingilia kwenye ukanda wao kwa kasi ila wao wameshindwa kutumia nguvu nyingi kurudisha hayo mashambulizi na kiwarudisha hao demand kwenye zone yao ila wanaishia kwenye mpaka ambao ndio support na hii ndio itawafanya jamaa waongeze nguvu nyingi na kuipeleka price juu zaidi na hapa ndio tunatengeneza head wakati huo bega la kushoto ndio limetengenezwa kwa ile initiative na retracement iliyofanyika so ikishaenda juu itafika kwenye zone ambayo hao jamaa nao wako wengi na pia majeshi ya upande wa pili yataingiwa na hofu so wataanza kupunguza kasi na hapo demand wataanza kuchukua profit zao na kitendo hiko kitapelekea supply waongeze nguvu na kurudisha price chini tena na price ikifika kwenye mpaka yani support itakutana na jamaa bado wapo wengi sana hapo wanasubiri mguso wa pili uje waende nao juu lakini kumbuka wakati initiative inatokea kutengeneza bega la kushoto supply walikua hawakujipanga so baada ya kuona hiyo initiative basi nao wataweka pending order zao mwisho wa hilo bega kwahiyo baada ya mguso wa pili wa kukamilisha head kwenye support, demand watachukua price kwenda juu lakini wakati huo supply wamesogeza ngome karibu yani pale ambapo bega la kushoto limeishia ili wakirudi tena hao demand wasiende mbali zaidi so demand wakifika eneo hilo wanakutana na supply wengi sana na hapo watashindwa kwenda mbali zaidi na price itarudishwa chini tena hapo bega la kulia linakua limekamilika so head and shoulder inakua imekamilika.

Je head and shoulder ni lazima ishuke chini endapo itakua kwenye support? Jibu ni hapana, coz forex si science ila kinachopeleka price up and down ni hali ya utofauti wa uwiano kati ya demand na supply na alama inayotuonesha kwamba supply ana nguvu kuliko demand au kinyume chake basi ni uwezo wa kuipeleka price kwenye zone ya mwenzie bila vikwazo au kuonesha vikwazo wakati unapotaka kushamuliwa kwenye ngome yako.

So kwenye head and shoulder shambulio la bega la kwanza ni lakushtukiza na baadae ikapelekea head na baada ya hapo hao watu wa upande wa pili wataona ela zao nyingi zinapotea au currency yao inakua weak so ili kuipandisha ni lazima waongeze nguvu wauze sana na hapo watakamilisha kichwa na wakifika kwenye zone tena

hawaendi kwa papara watajipanga upya ili kujua nguvu iliyopo upande wa pili kama bado ni ile ile au inapungua na ili wagundue hilo watasogeza zone usawa wa bega la kwanza na hao demand wakishindwa kupita hapo basi watajua kweli wamelegea so wataongeza nguvu zaidi na hatimae kuishuka price chini kwa kuingia kwenye zone yao na hii huwa inatokea sana kulingana na session husika na currency zilizounda pair husika zinauhusiano gani na hiyo session..

Na nlisema patten ni lazima zianze kwenye zone au ziishie kwenye zone, sasa hii pattern ya head and shoulder huwa inatokea kwenye zone na inaishia kwenye zone ila mabega yake huwa yanatengeneza minor zone, but kichwa huwa kinakua kwenye major zone na huku chini tunakoweka neckline huwa ni kwenye major zone pia


Jifunze Forex Kiswahili Huu ndio mfano wa head and shoulder
Ukiangalia hiyo picha utagundua imetokea kwenye support na maelezo yote nliyoyatoa hapo juu yako hapo kwenye picha, ila hapa nataka nielezee kwanza kwa kuunganisha na concept ya supply na demand.

Angalia hapo sasa kwenye neckline utaona hiyo zone imeguswa zaidi ya Mara moja na kama tunavyosema zone kadri inavyoguswa Mara nyingi ndivyo inavyopoteza ubora so baada ya kupoteza ubora nadhani umeona kilichofuta....hii ni confluence ya kwanza.

Pia confluence ya pili ni kwamba ukiangalia upande wa kulia wa hiyo head na bega hilo la kulia utagundua price imeform flat pattern ambayo hii inaonesha kwamba trend imeshabadilika si up tena ila ni down.

Why down ni kutokana na formation higher high ambayo ndio hiyo head then baada ya hapo ikashuka kuform lower high na lower low.


So hapo ndio tunapata confluence ya pili kwamba kuna uwezekano mkubwa wa hiyo price kushuka chini but hii sio sheria ila ni lazima tujue balance ya supply na demand ndio hasa inayosababisha market I move
Technical analysis inatusaidia kutambua mipaka iliyopo kati ya supply na demand ila si kwamba ndio hasa inapeleka soko juu na chini, so si kila mchoro unaouchora na ukausoma ukataka ufanye kazi kama vile ulivyosoma hapo utakua unaifanya forex iwe science wakati haiko hivyo
Nlisema hizi pattern kuna wakati huwa zinaathiriwa sana na session flani flani hasa hizi za triangle ila hizi za divergence Mara nyingi huwa zinatokea wakati soko linapokua haliko kwenye trend yani soko linapofanya fair treatment(haki), so huwa inapoonekana tu lazima ifuate uelekeo wake kwa asilimia kubwa ingawa sio sana, unaweza ukachunguza hii


Soko linapokua kwenye pattern hasa za triangle watu huwa wanafananishaga na mnada,  ndio mnada...kwamba kwenye mnada huwa kunakuaga na mtajo wa bei kutoka chini kwenda juu yani bei inapanda kuzidiana so mwenye ela nyingi anampiku mwenzie so kuna wale ambao huwa wanasubiri hadi bei inapogota sehemu Fulani na ikawa hakuna yeyote ambae anauwezo wa kuongeza juu so hapo ndio anagundua kwamba wameshindwa hawana uwezo tena wa kifedha so yeye ni muda wake wa kuongeza ela kuchukua hiyo bidhaa....Basi ndivyo ilivyo kwa forex tunapokua katika pattern let say ya triangle labda katika pair ya EURUSD katika session ya Asia na hiyo pattern ikadumu hadi asubuhi muda wa London basi hapo kuna uwezekano mkubwa mabadiliko yakatokea na mabadiliko hayo yatambeba zaidi EUR kwa maana hiyo session ya London ndio moja ya currency ambazo zinakipaombele sana pamoja na GBP....ila ikatokea kuanzia asubuhi London imefunguliwa hadi mida ya kukaribia New York session hakuna mabadiliko yoyote kwenye ile pattern basi hapo lazima dollar atakua na uwezo mkubwa wa kufanya initiative coz wataona jamaa wameishiwa nguvu so wao wakiingiza nguvu mpya basi lazima waendeshe price iwe upande wao, but kama nao watashindwa basi choppy itaendelea kuendelea so ndio maana nkasema kama mnada coz kuna mtegeano wa nyakati kabla ya kufanya maamuzi.

Kuna kitu ambacho pia napenda niseme kidogo, kwamba kuna watu wanakawaida ya kubashiri reversal mahali itakapoenda kufanyika kwakuangalia mikunjo so wengine wanadiriki hata kuweka pending order wakiamini price ikifika hapo ni lazima itageuka tu...utakufa kama unafanya hivi coz forex huwa tunatrade tunachokiona so ukianza kubashiri kwamba price ikifika sehemu Fulani lazima igeuke eti kisa kuna resistance au support kongwe acha, na utakua unakosa fulsa kila siku maana utakaa sana kusubiri na price inaweza isifike hapo so unabaki kushangaa tu.

Wataalamu wanasema ni ngumu kutambua reversal hadi itokee na hata big boys wenyewe hawana uwezo wa kutambua reversal sema wao wananguvu kwenye order so big boy mmoja anaweza akaweka order ya matrader wengi sana na akayumbisha soko mahali anapotaka liende yeye and si kweli kwamba wanaweka pending order kwenye zile zone za zamani let say kwenye zone ambayo ni ya miezi kadhaa ilitokea nyuma, hii ni biashara and watu wa nataka wapate ela kila siku so inaingiaje akilini mtu akaweke pending order kwenye zone itakayofikiwa na price ndani ya mwezi au miezi obvious haiwezekani.

So point muhimu ni kwamba usijiaminishe kubashiri reversal ya price kwenye ukanda wa zamani maana si sahihi ila huwa tunaingia au kubashiri kwenye zone ambayo imefikiwa na hapo ndipo ambapo jicho la matrader wengi duniani linapokua na watu sasa wanaanza kuweka order zao hapo na watakao shinda kuwa na order nyingi basi wanakua wameshinda kuipeleka price kwenye upande wanaoutaka wao.

Hii ni muhimu sana kaa nayo kichwani....

Jinsi ya kutambua hizo zone
  1. Demand na supply huwa sheria yake namba moja tunaangalia uwezo wa price kugonga na kutoka kwenye hiyo zone, kama tulivyosema awali ili zone ya demand au supply iwe valid basi ni lazima iguswe na candle zisizozidi tatu, maana hii ni zone so tunategemea kupata order nyingi kwahiyo wingi wa order utapelekea price isikae sana kwenye hilo eneo na endapo itakaa sana basi hiyo zone ni dhaifu coz inaonekana nguvu ya order zilizowekwa na seller na buyer haina utofauti mkubwa that's why price haimove katika ubora.
  2. Hakikisha haubashiri zone kwenye eneo ambalo unaamini itaenda kutokea kisa tu hilo eneo ilishawahi tokea zone siku za nyuma, ndio labda unaweza ukajiambia kwamba hapo mahali huwa kuna pending order but kumbuka pending order sio order mbaka iwe order so haina madhara kwenye movement ya price, kwahiyo kuna mawili price ifike hapo ipiyilize au price ifike hapo irudi ilikotoka na au price ifike hapo ikae kwenye hali ya uwiano.
  3. Ukanda mzuri ni ule ambao unatokea mahali ambapo kuna nafasi kubwa nyeupe, yani price haijafika hilo eneo kwa muda mwingi sana, kwasababu lazima itakua ni juu sana au itakua ni chini sana na hakuna trader ambae hapendi kubuy low na kusell high so zone ikitokea maeneo hayo huwa tunasema imetokea mahali ambapo mauzo yalifanyika mengi mno au manunuzi yamefanyika mengi mno kwahiyo reversal itatokea, ila usisahau forex sio science so hii si sheria hadi ikamilike yani hadi itokee.
  4. Hakikisha ukanda wako umeendana sawa na trend ya kwenye D1 hasa kama wewe ni intra day trader, hii itakufanya uwe na uhakika na kuhold kwa siku nzima maana uelekeo wa soko upo sawa na ulipoweka order yako siku hiyo.
  5. Hakikisha hauchukui zone ambayo imetokea katikati mwa price, coz hizi huwa zinakuaga ni trap za market marker, na nnaposema katikati namaanisha kabla trend haijaonesha kubadilika we ukaingia kwenye retracement hapo lazima ufe, kwasababu big boys huwa wanalichukua soko toka mwanzo mwa trend then wanapanda nalo au wanashuka nalo katika sheria zile zile za 3 impulse and 2 correction so watakwenda nalo then watafika mahali watachukua faida zao hapo utaona kama trend ni up basi soko linashuka kidogo na hapa kuna watu wanavutiwa wataingia hasa wale wa like yes yes soko linashuka hili unatia order yako wataacha tuingie kwawingi then wanarudi tena kwenda kukamilisha trend hapo ndio unaanza kulia, kwahiyo usifanye hivo.

Jinsi ya kuchora hizo kanda, na nilazima kabla ya kujua kuchora tujue hizo zones au kanda huwa zinakua zipo katika mafungu mafungu, kwahiyo ukiiona zone ni lazima uelewe hii ni zone ya aina gani.

Ngoja tuongee kuhusu hizi zone zinazosababishwa na big boys pindi wanapochukua faida na zile zinazosababiswa na big boys pindi wanapoweka order.

Kuna wakati unaweza ukafungua Mt4 yako ukakuta trend ni up ila ikawa inaenda juu then inashuka kwa pips kadhaa halafu inarudi tena kuendelea na trend na wakati inashuka huwa inatengeneza zone basi hii ndio huwa tunaita zones ambazo zimesababishwa na hawa jamaa big boys kuchukua faida zao.

Pia kuna zile zone ambazo ukifungua Mt4 yako utazikuta zinaanzia juu kwenye supply au chini kwenye demand na zinakwenda moja kwa moja katika uelekeo wa trend huku ikitengeneza HH,HL na LH,LL ambazo hazifiki kwenye mahali ambapo zone ipo, hii ndio inaitwa zone ambayo imesababishwa na big boys kuweka order na kinachofanya price isifike kwenye mahali ambapo hizi order zipo ni kwamba hawa jamaa big boys huwa hawaruhusu kitendo hiki kitokee coz wanahofia endapo wataruhusu price ifike kwenye usawa wa order zao basi wananweza wakawavutia wawekezaji wengine wakadhani kwamba hii zone sasa imekwisha muda wake so ni muda wa kuweka order nyingi ambazo zikifanikiwa kuwa nyingi kuliko zilizokuwa kwenye hiyo zone basi price itakwenda kinyume na wao na kupelekea wao kupata hasara.

So hii ni muhimu ambayo ni lazima tuifahamu kwamba zone inayosababishwa na big boys wakati wanachukua faida huwa inakwenda na kurudi mahali kwa awali then inavunja hiyo zone na kwenda juu zaidi kama trend ilikua up au kushuka chini zaidi kama trend ilikua down.

Ila zone inayosababishwa na uwepo wa order nyingi za big boys huwa price ikienda chini kwa downtrend itatengeneza hizo swing za LH, LL ambazo haziwezi kufikia mahali ambapo order iliwekwa, kwanini iko hivi? Hii ni kuonesha kwamba zone bado imara.


Jifunze Forex Kiswahili

Ukiangalia hiyo picha hapo juu trend ni down na Mimi nimejaribu kuonesha kwenye upande wa zone za supply tu ila ukiangalia kwa umakini kwa chini ya hizo zone utaona vijizone vidogo vya demand pia, so navo ni muhimu ukiwa unafanya analysis uvichoree, ila hiyo picha hapo inaonesha upande wa supply na kwa jina moja unaweza ukaiita drop base drop, kwamaana inakua inashuka then inatengeneza consolidation kidogo then inashuka tena, so ndio maana ikaitwa drop base drop...coz inaanza kushuka inatengeneza base ambayo ndio consolidation halafu inakuja kushuka tena...tutaiongelea baadae hii drop base drop, rally base rally na drop base rally pamoja na rally base drop.


Jifunze Forex Kiswahili

Hii ni ile aina ya zone ambayo inatokea baada ya big boys kuchukua faida, iangalie vizuri hapo

Ukirejea hapo nyuma nliwahi kusema uimara wa zone haupimwi na ukongwe wake ispokua zone inatokea pale tu ambako kuna uwingi wa order, ila kuna wakati ukijaribu kuangalia unaweza ukaona zone ambayo ilitokea mwezi uliopita katika D1 ukaona na leo imefikiwa tena na price na inafanya reversal hapo, hapa wengi watapingana na hiyo kauli kwamba zone haipimwi kwa ukongwe wake....ila hiyo kauli iko sahihi ispokua price ikitoka kwenye zone wanasema inaweza ikarudi baada ya muda flani na hii ni kulingana na timeframe ambayo wewe unatumia, kwamfano kwenye 1H timeframe price ikitoka kwenye zone na ikarudi baada ya 24hours basi hii zone tunasema bado iko valid ila ikichelewa kurudi basi hii zone tunasema haiko valid.

Pia kwenye D1 timeframe price ikitoka kwenye zone ili hiyo zone iendelee kuwa valid basi lazima ije irudi baada ya siku 30 kinyume chake basi hiyo zone haitokua valid tena, so ndio maana kuna wakati unaweza ukaona zone ambayo unaamini ni kongwe lakini bado ikawa iko valid ni kutokana na kwamba price ilirudi kwenye eneo hilo kwa muda sahihi na sio kwamba eti ni kongwe hapana.

Sasa unaweza ukajiuliza kwanini price ikitoka kwenye zone itaenda then itarudi baada ya muda flani?

Hii inatokana na kwamba, banks nyingi huwa zinapenda kuweka order zao kwenye zone so price ikifika kwenye zone tu basi bank wataweka order zao hapo, kama ni kwenye supply basi wataweka order za kusell na kama ni kwenye demand basi wataweka order za kubuy, sasa kipindi wanapobuy au kusell katika zone watakwenda na price katika umbali ambao wao watahitaji then wakishafika hapo basi wataanza kuchukua faida zao na kipindi wanafanya hivi basi reversal itatokea na price itaanza kugeuka kurudi tena kwenye zone, na hapa sasa watawavutia ma retailer wengi watadhani sasa trend imechange wataanza kuingia na price ikifika tena kwenye zone bank watatumia ile faida yao waliyoipata kurudisha tena price kule ilikotoka na hapa wengi wataliwa ela zao....hii ni sababu ya kwanza.

Sababu ya pili ni kwamba bank nyingi huwa hazipendi kuuza au kununua katika umbali ambao price zimeachana sana, so ili iwe rahisi kwa wao kucalculate faida wanayohitaji basi wataweka order kwenye zone wataishusha price ila katika izo order kuna zingine zitasalia kwenye zone so watakwenda na order chache then wakishapata faida wanayoitaka watamanipulate soko yani watalipeleka vile wao wanataka na hapa watachukua faida then price itarudi kule kwenye order zao then wataziingiza na hizo order sokoni tena na hapo mambo yatarudi yalikotoka so hii pia itawasababishia watu wengi yani akina sisi kula za us

Ila kuna wakati unaweza ukaona price imetoka kwenye zone ikaenda kwenye upande tarajiwa kwenye upande wa supply au upande wa demand, ila baadae ikafika sehemu price ikawa inarudi sasa ilikotoka na ikafika kwenye zone ikapitiliza hadi upande wa pili, hapa tunasema hao mabank hapa walishatoka so hakuna order ambazo zilibaki kwenye hiyo zone na ndio maana price iliporudi kwa Mara ya pili ikapitiliza, na hapa sasa investor wengine wataingia coz wataamini zone ambayo ilikuepo mwanzo now imekua si valid tena kwahiyo nao wataweka order zao then price itakwenda kwenye upande ambao order ni nyingi.

NB:
Wingi wa order hausababishwi na uwingi wa watu katika demand au katika supply, isipokua anaweza akawa mtu mmoja tu ambae anaela nzuri akaweka order za kutosha na akayumbisha soko na hata kama upande mwingine unawatu elfu kumi ila wakawa na order ambazo ndogo kuliko alizotoa huyo mtu mmoja basi hawatokua na ujanja wa kuyumbisha soko richa ya uwingi wao...na hii aliifanya George Soro

Namna ya kufanya biashara ya Forex

Karibu katika site yetu hii ambapo kama kawaida tunaendelea na mfululizo wa masomo mbali mbali kuhusu namna bora ya kufanya biashara ya Forex kwa faida.

Jinsi ya kufanya biashara ya Forex

Tukumbuke kwamba biashara ya Forex ndio biashara kubwa kuliko zote duniani ambayo ina mzunguko wa zaidi ya trillion 5 za kimarekani kwa siku.

Iwapo utafanya maamuzi sahihi, na kuamua kujifunza vyema biashara hii, basi nawe utakua miongoni mwa watu wanaonufaika vyema na biashara hii duniani kote.

Jambo la msingi kufahamu ni kwamba, Forex ni biashara ya kubadilisha Fedha za kigeni, biashara hii hufanyika kwa njia mbali mbali, lakini pale unapotaka kuifanya kwa faida, basi utaifanya mtandaoni kwa kufungua account kwa taasisi zinazokuwezesha ku nunua na kuuza pair mbali mbali za Forex katika masoko makuu ya Forex duniani.

Masoko haya yanayokuwezesha kuuza na kununua, yameunganishwa kwa mtandao maalum unaojulikana kama ECN yaani Electronic Communication Network.

Iwapo ungependa kuanza biashara hii ya Forex, basi itakulazimu kuanza kwa kufungua account kwa broker atakayekuwezesha kununua na kuuza pamoja na kukuwezesha ku withdraw faida utakayokua umeipata baada ya kujiunga na Forex.

Yupo broker ambaye tunamtumia kwa Africa Mashariki, ambaye bahati nzuri naye anakupatia dola 30 za bure za kuanza kufanya biashara hii, na pindi utakapofanikiwa kufikisha vigezo vyao, utaweza ku withdraw hadi dola 100 bure kabisa.

Kujiunga na biashara hii ya Forex kupitia broker wa TemplerFX, bonyeza kitufe kifuatacho kutengeneza account, kisha kwenye fomu itakayofunguliwa, fuata maelekezo yote ikiwa ni pamoja na kujaza taarifa zako, na baadae utapaswa ku upload copy za kitambulisho wako ili kuthibitisha au ku verify identity yako.

Bofya kitufe kifuatacha kujiunga na Forex:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Ukishamaliza kutengeneza account yako, endelea kuperuzi site hii ambapo tumekupatia maelekezo mbali mbali kabisa na mepesi ambayo yatakuwezesha kukupa elimu ya awali ya biashara hii ya Forex.

Mbinu kuzuia hasara kwenye biashara ya Forex

Iwapo ndio kwanza umeanza biashara ya Forex, au tayari ni trader mzoefu wa Forex, jambo la msingi kabisa ambalo unapaswa kuzingatia muda wote unapofanya biashara hii ni namna ya kuhakikisha kwamba pesa yako inabaki salama kwa kuzingatia mbinu mbali mbali zenye lengo la kuhakikisha unaepukana na uwezekano wa kuunguza account yako au kufunga positions zako kwa hasara kubwa.

Forex Risk Management

Zipo mbinu mbali mbali ambazo trader unapaswa kuzizingatia ili kuweza kuwa na uhakika wa pesa yako kubaki salama.

Iwapo ndio unaanza kujifunza Forex, na bado hujatengeneza account, bofya kitude kifuatacho kujiunga na Forex:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Kama tulivyokwisha kusoma kwenye post zilizopita pamoja na angalizo juu ya biashara ya Forex, unapaswa kufahamu kwamba haijalishi kwamba una uzoefu na elimu kiwango gani juu ya Forex, muda wowote unaweza kupata hasara itakayopelekea sehemu au pesa yako yote kupotea.

Sasa ili angalau kuweza kuzuia hasara au upotevu wa pesa yako kwenye biashara hii ya Forex, yakupasa kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Soma na Fuatilia

Kujifunza kuhusu Forex, jinsi inavyofanya kazi, misingi yake na technique zake zote ndio msingi mkubwa wa mafanikio katika biashara ya Forex. Iwapo utaamua kuwa Forex trader, basi yakupasa uwe makini na kuwa active kwenye kufuatilia mambo mbali mbali au news zinazoweza kupelekea movement kubwa kwenye masoko ya Forex, jambo hili litakusaidia kufanya maamuzi sahihi pale unapoamua kuingia sokoni.

Kusoma na kufuatilia, kutakufanya kuwa na hali ya kujiamini pale unapoamua kuingia sokoni kwa kuwa yapo matukio makubwa ya kisiasa na kiuchumi yanayoweza kugeuza uelekeo wa soko ghafla na kujikuta ukiingia kwenye hasara kubwa.

2. Epuka Brokers wanaolalamikiwa sana

Uzuri tunaishi kwenye nyakati ambazo ni rahisi kufahamu heshima/reputation ya broker unayetaka kujiunga naye, waweza kufahamu zaini kuhusu broker huyo kwa ku search kwenye mtandao au kutembelea tovuti iitwayo ForexPeaceArmy ili kufahamu ni kiwango gani cha malalamiko broker huyo anayo, ni vizuri pia kufahamu mambo mbali mbali kuhusu broker huyo ikiwa ni pamoja na kufahamu njia za kuweka na kutoa pesa, ufahamu fee zao, na pia hakikisha ni broker ambaye yupo regurated na vyombo vinavyoheshimika kufanya regulations za taasisi za fedha.

3. Anza na account ya majaribio (demo account)

Tumeshajifunza jinsi ya kutengeneza account ya demo kwa ajili ya kuanza ku practise ku trade Forex, waweza soma post hii:

Jinsi ya kufungua na kutumia Demo account kwenye Forex

Ni vyema kabla hujaanza kuweka pesa zako kwenye Forex, ukajaribu kutumia demo account ili kujifunza zaidi na kupima uelewa wako juu ya ku trade Forex, vinginevyo kama huna ufahamu wa kutosha, ukikimbilia kuanza ku trade moja kwa moja kwa real account, utapoteza fedha zako.

4. Epuka kutumia Leverage kubwa sana

Moja kati ya sababu zinazofanya Forex ipendwe zaidi ni matumizi ya leverage, leverage ni utaratibu unaowekwa na broker wa kuhakikisha kwamba una uweza wa kupata faida kubwa hata kama kiwango chako ulicho deposit ni kidogo, leverage ni uwiano wa kiwango cha pesa ulicho nacho, na kiwango cha pesa unacho trade. Matumizi ya leverage kubwa yanakupa uwezekano wa either faida kubwa sana, au hasara kubwa sana kwa muda mfupi.

Jinsi ya kufungua account Forex

Jinsi ya kufungua account Forex

Baada ya kujifunza jinsi ya kujiunga na Forex, na kufahamu kwamba unapaswa kuanza biashara ya Forex kwa kufanya majaribio kwa kutumia account ya DEMO, sasa ni wakati muafaka wa kujua jinsi ya kujiunga na biashara hii kubwa duniani.

Jinsi ya kufungua account Forex
Jinsi ya kufungua account Forex
Kama hukusoma kuhusu jinsi ya kufungua na kutumia demo account ya forex, soma post hii:

Jinsi ya kufungua na kutumia DEMO account kwenye Forex

Kifuatacho sasa ni kufahamu jinsi ya kufungua account ya FOREX, kama nilivyokwisha kuwafahamisha hapo awali kwamba jambo la msingi ni kuchagua broker ambaye utakua unamtumia katika biashara ya forex, na kwa kuwa tunafahamu kwamba broker ambaye atakuwezesha kutuma na kupokea pesa kwa East Africa kwa urahisi zaidi kwa sasa ni TemplerFx ambaye anakuwezesha kutuma na kupokea pesa kwa huduma ya M Pesa ya Vodacom.

Kufungua account ya TemplerFX bofya kiungo kifuatacho ambacho kitakupeleka kwenye fomu maalum ambayo utapaswa kuijaza.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Mara baada ya kutengeneza account, utapaswa kuithibitisha account yako ambapo utaombwa u upload copy ya kitambulisho chako kinachoweza kuthibitisha taarifa kuhusu wewe.

Jinsi ya kujiunga na Forex

Jinsi ya kujiunga na Forex

Baada ya kujifunza kuhusu utangulizi wa biashara ya Forex, sasa ni wakati muafaka wa kujifunza jinsi ya kujiunga na biashara hii ya Forex.

Iwapo tayari umekwisha pitia maelezo ya awali, ni wakati sasa wa kutengeneza account yako ya Forex. Waweza tengeneza account kupitia Broker maarufu zaidi East Africa na Duniani mwenye wateja zaidi ya milion 2.5 katika nchi 190 duniani.

Bofya kitufe kifuatacho kufungua account yako ya Forex bure kabisa:

FUNGUA ACCOUNT

Jambo ambalo ni muhimu zaidi kuhusu biashara ya Forex, ni kufahamu misingi yote ya biashara hii, na kuhakikisha kwamba unafahamu hatua zote muhimu za kuchukua ili kuzuia hasara (Risk Management Strategies)

Jinsi ya kujiunga na forex

Mbinu za kuzuia hasara katika biashara ya Forex unaweza kuzisoma kwenye post ifuatayo

Mbinu kuzuia hasara kwenye biashara ya forex (Risk Management Strategies)

Baada ya kuwa na uelewa mpana wa jinsi biashara ya Forex inavyofanya kazi, na kufahamu mbinu za kuzuia hatari ya account yako ya forex kuungua, sasa unaweza kujiunga na Forex.

Kama ndio unajiunga kwa mara ya kwanza, unashauriwa kuanza kwa kutengeneza account ya majaribio au DEMO ACCOUNT, account hii itakuwezesha kujaribu uwezo wako wa kufanya biashara hii ya forex, kutengeneza account ya majaribio ni rahisi zaidi, kwani unachopaswa kufanya ni ku install app ya Meta Trader 4 kwenye simu yako, account hiyo itakuwezesha kuunganishwa na Forex DEMO bure kabisa bila kupaswa kulipia kitu chochote.

Post ifuatayo nimeandika kwa kirefu kuhusu DEMO account kwenye forex

Jinsi ya kufungua na kutumia DEMO account kwenye Forex

Kujiunga na Forex demo, fungua simu yako, kama ni ya android nenda kwenye Play Store, na kama ni iPhone nenda kwenye App Store, halafu andika neno Meta Trader 4 Hapo itafunguka app hii ya Meta Trader 4 ambapo ukisha i install, moja kwa moja itakufungulia demo account ambayo waweza kuitumia kwa majaribio.

Ukishaweza kutumia demo account vizuri, sasa waweza hamia kwenye REAL ACCOUNT kujiunga na real account waweza mtumia broker wetu ambaye tunamtumia zaidi East Africa anayeitwa XM kwa ku bofya kiungo kifuatacho.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Endelea kuwa pamoja nami katika safari hii ya mafanikio kupitia biashara ya Forex

Jinsi ya kutumia M-Pesa kuweka na kutoa fedha katika Forex

NOTE:
Huduma ya ku deposit na ku withdraw kwa kutumia M-Pesa Tanzania kupitia Broker TemplerFx kwa sasa imesitishwa hadi hapo iPay na Vodacom watakapokamilisha taratibu zilizowekwa na BOT.
Huduma hii inaendelea kupatikana kupitia Safaricom M-Pesa Kenya ambapo waweza ku deposit au ku withdraw kwa kuchagua M-Pesa Kenya.
Kama bado huna account ya Forex kupitia TemplerFx, bofya kitufe kifuatacho kujiunga:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Moja kati ya changamoto nyingi zinazoikumba biashara ya Forex hususani kwa nchi zinazoendelea ni namna bora ya kuweka na kutoa pesa kwenye account yako ya Forex.

Templer fx M Pesa
Templer Fx M Pesa

Jambo hili kwa kawaida huwa linasimamiwa na broker uliyeamua kumtumia. Brokers walio wengi wanakuwezesha kuweka pesa kwenye account yako kwa kupitia njia ya Bank kupitia credit cards kwa mfano Visa au Mastercard.

Jambo zuri kwa forex Traders wa East Africa ni kwamba yupo broker ambaye anakuwezesha kuweka na kutoa pesa kwa kutumia Vodacom M-Pesa papo kwa papo. Broker huyu si mwingine bali ni TemplerFx ambaye anatumia huduma ya iPay Africa kukuwezesha kuweka na kutoa pesa kwenye account yako ya M Pesa muda wowote. Sasa tukaangalie ni kwa jinsi gani unaweza kutumia huduma hii.

Bofya kitufe kifuatacha kujiunga na Templer Forex kutumia huduma ya M-Pesa kuweka na kutoa pesa kwenye Forex:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Jinsi ya kuweka na kutoa pesa Templer Fx kwa M Pesa:

Ikiwa umeshajiunga na tayari una account ya templerfx ambayo ni verified. Fuata mtiririko ufuatao:
  1. Kwa kutumia computer yako, Login kwenye account yako ya TemplerFx
  2. Kwenye menu ya upande wa kushoto, bofya palipoandikwa Finance
  3. Chini yake utaona Deposits, bofya link hiyo.
  4. Kwenye ukurasa utakaofunguka, chagua account unayotaka ku-deposit, na iwapo bado hujatengeneza account, utaambiwa utengeneze account.
  5. Ukishachagua account, bofya sehemu iliyoandikwa Select a payment System
  6. Chagua palipoandikwa IPay Africa
  7. Baada ya hapo utachagua Method of payment
  8. Hapo sasa utachagua M-Pesa Tanzania, iwapo upo Tanzania au M-Pesa Kenya iwapo upo Kenya
Baada ya hapo, fuata maelekezo yafuata jinsi ya kulipa pesa, na muda huo huo ukishalipa utaona balance yako kwenye account yako ya TemplerFx

Mtaji wa kuanzia Forex

Je unahitaji mtaji kiasi gani wa kuanzia biashara ya FOREX?

Mtaji wa kuanzia Forex

Kama tulivyoona katika mada ya utangulizi kuhusu biashara ya Forex, kwamba Forex ndio biashara kubwa zaidi duniani ambayo ina mzunguko wa dola za kimarekani trilioni 5 kwa siku. Iwapo na wewe ungependa kuwa sehemu ya mzunguko huu wa pesa, huna budi kujifunza vizuri misingi yote ya biashara hii yenye ushindani mkubwa, ili kuepuka kupata hasara.

Kiwango cha awali cha kuanzia biashara ya FOREX kinategemea na dalali wako wa forex (Forex broker), wapo baadhi ya Forex brokers ambao unaweza ukaanza na kiwango kidogo kidogo cha dola 10 na wengine hata dola 1.

Tena baadhi ya brokers hawa, watakupatia pesa ya ziada ya kulinda account yako kama mkopo (Credit) kwa mfano broker maarufu ajulikanae kwa jina la XM.COM yeye anakuwezesha kuanza na mtaji mdogo wa dola 5 na kukupatia mkopo wa dola 30 iwapo utafungua MT4 account aina ya STANDARD.

Broker mwingine ambaye amekua akitumiwa na watanzania wengi ni TEMPLERFX ambaye anakuwezesha kuanza na kiwango kidogo zaidi cha dola 1 (naam, dola moja tu) ambacho unaweza kuki deposit kwa kutumia account yako ya M-Pesa.

Historia inaonesha kwamba, ni wafanyabiashara wachache sana wa FOREX ambao wana uwezo wa kuanza na kiwango kidogo cha pesa na kuweza kukipandisha hadi kufikia kiwango kikubwa kwani unapokua na balance ndogo, ndivyo ambavyo ni rahisi kwa account yako kuisha pale soko linapo panda na kushuka.

Iwapo ungependa kujiunga na broker anayekuwezesha kuanza na kiwango kidogo cha dola 5 ambacho waweza kukiweka kwa kutumia M-Pesa Mastercard au Skrill, bofya kiungo kifuatacho.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Na iwapo hujafahamu jinsi ya kuweka na kutoa pesa za forex kwa kutumia Vodacom M-Pesa, bofya link ifuatayo ambayo nimekuandalia maelezo mengi juu ya namna ya kutumia M-Pesa kuweka na kutoa pesa ya Forex.

Jinsi ya kutumia M-Pesa kuweka na kutoa fedha katika Forex

Jinsi ya kufanya biashara ya FOREX

Post iliyopita ilikuwa na utangulizi muhimu kuhusu FOREX, kama hujaisoma, waweza bofya kiungo kifuatacho kuisoma:
Forex ni nini?

Kama tayari una uelewa wa awali wa biashara hii, bofya kiungo kifuatacho ili ujisajiri na broker anayekubalika zaidi East Africa!

BOFYA HAPA KUJIUNGA

Sasa twende Sokoni. Twende kwa Hatua pia:

1. Forex inafanyika kwa kulinganisha thamani za Sarafu Mbili kwa pamoja (Currency Pairs).
Kule sokoni unapoingia, ili uweze kununu na kuuza, utakuta bidhaa (currency) zimewekwa kwenye mafungu mafungu ya mbili mbili (pairs). Mfano:
i)Euro na US Dollar pamoja,
ii) Paund (GBP) na USD pamoja,
iii) USD na Yen (JPY) pamoja,..nk. nk. nk
Zinavyopangwa, utazikuta hivi:
EUR/USD
USD/JPY
GBP/USD
USD/CAD

Chukua EUR/USD kwamfano;
Hiyo ya mwanzo (EUR) Inaitwa BASE currency, na hiyo ya pili, USD, unaitwa COUNTER Currency. Sasa, bei unazoziona kwenye grafu zikipanda na kushuka ni bei za Base Currency kwa kulinganishwa na Counter Currency. Chukulia hii;

EUR/USD = 1.25358

Maana yake, Euro 1 = 1.25358 USD. Kama unataka kununua EURO 1, utalipa 1.25358 USD.

Bei za Euro sokoni, kwa kulinganishwa na USD, zinaweza kubadilika ndani ya sekunde! Sasa, faida zinapatikana kwa wewe KUNUNUA Currency moja, wakati bei iko chini na KUIUZA wakati bei inapopanda. As Simple as that. Sasa, ili kujua kwamba baada ya muda itapanda ili UNUNUE sasa hivi na uuze itakapopanda, au, kujua kwamba itashuka zaidi ya hapo ilipo ili, UUZE sasa hivi na UNUNUE itakapofika bei ya chini zaidi,...mchakato huo unaitwa MARKET ANALYSIS.

2. Forex Trading, hufanyika kwa "Kubonyeza tu" kitufye cha kuBUY au cha kuSELL. Basi. Hilo tu. Unakuwa umefanya TRADE. Lakini sasa, ili uweze kujua, unabonyeza kipi, muda gani, uTRADE kiasi gani ili upate faida gani, inabidi uwe unajua kufanya MARKET ANALYSIS mwenyewe au uwe na MTAALAMU unayemuamini akufanyie na akupe taarifa hiyo. Sasa, hiyo taarifa ndiyo inaitwa "Fx Signals" au "Trade Signals"..nk.

3. Faida au hasara kwenye Forex Trade zinapimwa kwa PIPS.

PIP ni kitu Gani? Kitefu chake ni "Percentage In Point". Pip ni tofauti ya POINT MOJA katika bei ya Pair ya Currency tokea ulipoweka ORDER yako. Its a 1point Price Movement ama kwenda juu au kuja chini.

Hii tofauti ya bei (Pip) inapimwa katika viwango vya Desimali. Currency Pairs nyingi (sio zote tafadhali) zinatumia SEHEMU NNE ZA DESIMALI. Utakuta kwenye Platform wanaandika SEHEMU TANO lakini ni ili kukusaidia wewe mfanyabiasha, ila zinazohesabika ni NNE.

 Utaelewa vizuri kwenye mfano. Chukulia hiyo ya pale juu:

EUR/USD = 1.25358

Tunaangalia "Price Movement" katika sehemu ya 4 ya desimali. Ile ya tano inakupa tu sehemu ya Pip.

Chukulia hapo bei ibadilike ama kwenda juu au chini kama ifuatavyo:


EUR/USD = 1.25458
                     ⬆️
EUR/USD = 1.25358
                     ⬇️
EUR/USD = 1.25258

▶️ Kutokea 1.25358 kwenda 1.25458 maana yake bei imepanda kwa 10pips.

▶️ Kutokea 1.25358 mpaka 1.25258 bei imeshuka kwa 10pips.

Swali, je kutoka 1.25258 mpaka 1.25200?

Jibu, imeshuka kwa 5.8pips. Sawa mpaka hapo?

Kwa hiyo, FAIDA na HASARA katika Forex zinapimwa kwa PIPS. Ukiwakuta watu wanaambiana, mimi leo nimepata, 30 USD, 50 Yen, 70 Paunds...unajua tu hawa sio professionals. Kule watu wanajisifia Pips sio Dola au Paundi au Yen. Utakuta mtaalam anasema, Mimi ninapata Average/Wastani wa 500Pips, au 700Pips au 1100Pips kwa wiki au kwa mwezi, nk. Sio Dola! Na mtaalamu anayependwa na wateja,..Anayeaminiwa kwamba anao uwezo wa Market Analysis mzuri ni yule anayejikusanyia PIPS nyingi mwisho wa siku.

Swali: Je, naweza kupata PIPS kidogo na nikawa na faida KUBWA kuliko aliyepata PIPS nyingi kunizidi?

Jibu: Ndio. Inawezekana! Lakini, wooote, tutakujua kwamba huna PROFFESSIONALISM bali umeRISK sana na ungeweza ukapoteza hela nyingi sana pia! Sema tu bahati yako leo. Hakuna mtu mwenye hela zake atakayekuamini tukikujua hivyo. Nitaeleza zaidi hili sehemu inayofuata.

5. Nini Thamani ya PIP moja? Ili nijibu hili swali, kuna maelezo lazima nikupe. Ila kwa kifupi, thamani ya PIP moja inaweza kuwa ni 10 USD, au 1 USD, au 0.1 USD. Angalia:

Kumbuka, hii ni biashara kubwa sana. Kule kwenye soko la dunia, CURRENCY zinauzwa kwa jumla. Huwezi kwenda kununua eti Dola 1, au Paundi 5 au Euro 8. No. Unanunua kwenye mafungu! Kule kuna mafungu matatu tu maalum yanayouzwa:

a) 100,000 USD, au
b) 10,000 USD, au
c) 1,000 USD

Kwani hata Buteau de Change si wanauza kwa mafungu? Utakuta;

1 - 50 USD bei yake
51- 100USD bei yake
101- 1000USD bei yake
N.k. nk, nk..ndo ivo ivo kule.

Sasa,..

Wale waliosoma Science Sekondary mnikumbushe hii: S.I Unit maana yake nini tena? International Standard Unit? Nimesahau. Ila maana yake ni hii. Kipimo maalum kilichokubalika dunia nzima kupimia kitu mfano;
Urefu, S.I.Unit ni Meter
Ujazo, S.I.Unit ni Litre
Uzito, S.I.Unit ni Gram
N.k, n.k,...

Sasa kwenye Forex, kipimo kilichokubalika kupimia kiwango cha MAFUNGU ya kuuza na kununua Currency kinaitwa "Lot" Tumezoea kuita, "Standard Lot".
➡️ Lot moja ukiigawa kwa KUMI utapata 1 Mini~Lot.
➡️ Mini~Lot moja ukiigawa kwa KUMI (au Standard Lot moja ukiigawa kwa MIA) unapata 1 Micro~Lot.

Angalia sasa;

1 Std Lot = 100,000 USD,
1 Mini~Lot = 10,000 USD
1 Micro~Lot = 1,000 USD

Nenda kinyumenyume, utaona kwamba:

1lot = 10 mini~lots = 100 micro~lots

Au kwa namna nyingine;

1Micro~lot = 0.1 Mini~lot = 0.01lot.

Sasa, unapokwenda KUPLACE ORDER ya kuBUY au kuSELL kuna sehemu utaulizwa ujaze SIZE ya ORDER yako. Utajaza 1Lot kwa maana ya unanunua au kuuza 100,000USD au utajaza 0.1lot kwa maana ya unauza au kununua 10,000USD au utajaza 0.01lots kwa maana ya unauza au kununua 1,000 USD.

Sasa twende kwenye thamani ya PIP.

Endapo ULIUZA au KUNUNUA "1 Standard Lot", kila PIP moja unayoipata sokoni kama faida, ni sawasawa na 10 USD. Maana yake, kwa 100,000 USD ulizoTRADE, umepata faida ya 1PIP au 10 USD.
Kama uliTRADE 1minilot, 1PIP ni sawa na 1 USD na kama uliTRADE 1 microlot, PIP moja ni sawa na 0.1 USD.

Umenielewa mpaka hapo? Ngoja nikusisitize yafuatayo kama NB.

Note1: Si kila Currency Pair PIP yake inapimwa kwa 4decimal places. Kuna baadhi sio, mfano Currency Pairs ambazo zina Japaneese Yen ndani yake kama EUR/JPY au USD/JPY na zingine, PIP yake moja inahesabiwa katika sehemu MBILI za Desimali. Ukishakuwa sokoni utazizoea tu usiogope. Utazijua zote.

Note 2: Sio kila 1PIP ni sawa na 10USD kwa 1lot. Kuna tofauti zake pia. Baadhi ya currency pairs, 1lot zao, 1PIP utakuta ni 8USD, 11USD au hata 7USD. Inategemea. Ile ya 1Pip = 10 USD ni Standard. Utazielewa pia ukishaingia sokoni. Ila mpaka hapa, unaweza kuelewa kwamba, aliyepata 25pips za 1lot za:
i) EUR/USD,
ii) EUR/JPY, na
iii) GBP/USD
wanatofautiana kwenye hela kwa sababu thamani ua 1PIP kwao zinatofautiana. Ila tofauti zao si kubwa saaana. Zoote, zinakaribi pale pale kwenye Kwa 1std lot, 1Pip = 10 USD.

6. Hivi Kweli, kuna Retail Trader ataweza kununua 1lot, au 1minilot, au hata 1microlot (kiasi cha chini kabisa cha order moja ambacho ni 1000usd = 2.4mil Tzs) na akasavaivu kwenye hii biashara kweli. Huko si ni kubaguana? Wataifanya wenye nacho tu, si ndiyo?

Hapo sasa, ashukuriwe Mungu kuna Mtukati anaitwa Broker. Ndiye anayetuwezesha mimi na wewe tushiriki Forex. Vingenevyo, ingebaki kuwa ni biashara ya Mabenki, Serikali, Taasisi kubwa kubwa za Kifedha ma Matycoon wakubwa.

Kazi kubwa ya Broker ni kukukopesha hela zake ili uzifanyie biashara ya Forex. Atakuambia kwamfano; ukifungua account ya mtandaoni kwangu, uka~deposite hela, kwa kila Dola 1 utakayo~deposite, nitakukopesha Dola 100 au, 200, au 500 au wengine mpaka 1000! Hicho kitendo kinaitwa "Leverage".

Wanaandika hivi:

Leverage:
1:50 (kwa kila dola 1 uyakayoweka kwangu, nakukopeaha 50), au
1:100 (weka 1, kopa 100), au
1:500 (weka 1 kopa 500) n.k, n.k


What is PIP in Forex



Kwamfano sasa, ukiweka USD 100 kwenye account yenye Leverage ya 1:500 maana yake ni nini?

Kwa kila dola 1 uliyo~deposite anakukopesha dola 500. Kwa hiyo, jumla utakuwa na dola 100 x 500 = 50,000. Hiyo inaitwa "Purchasing Power". Hapo maana yake ni kwamba unauwezo sasa wa kununua au kuuza USD 50,000 ambayo ni sawa na 0.5 lot size, tofauti na awali ambapo ungetegemea 100$, usingeweza kuuza au kununua chochote (hata order ndooogo kabisa ambayo ni Micro~Lot = 1000usd).

Brokers wanakuchaji wewe comission wakati wowote unapoTRADE, ndipo kipato chao kilipo. Siku nyingine nitawazungumzia kwa undani kidogo hawa maBroker.

Kama tayari una uelewa wa awali wa biashara hii, bofya kiungo kifuatacho ili ujisajiri na broker anayekubalika na kuaminika zaidi East Africa

BOFYA HAPA KUJIUNGA

Forex ni nini?

FOREX ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni ambayo imeonekana kuwa na mzunguko mkubwa zaidi kuliko biashara yoyote dunianini kwani inazungusha zaidi ya dolla za kimarekani trillion 5 kwa siku.

Mtu yoyote anaweza kujifunza biashara ya forex, na kuwa Forex trader mwenye mafanikio. Ili kuwa Forex trader, ni lazima uwe na account ya Forex

Biashara ya Forex imechangiwa sana na mapinduzi ya teknolojia ambapo sasa mtu yeyote unaweza ukafanya biashara hii mahali popoke akiwa na huduma ya mtandao wa intaneti kwa kompyuta au simu janja(smartphone)

  1. Forex ni kifupisho cha FOReign EXchange kwa maana ya biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni. Kama unavyoijua kazi ya Bureau de Change, ndiyo iyo hiyo tunaifanya kwenye Forex sema hii ni ya mtandaoni.
  2. Forex ni biashara halali na inafanyika ulimwenguni mwote na taasisi kubwa kubwa za kifedha na mabenki na central banks.
  3. Biashara hii ni ya mtandaoni na wauzaji na wanunuzi hukutana huko ~soko lake ni la mtandaoni na ni la dunia nzima. Inakadiriwa kuwa, biashara hii imevutia wawekezaji ambao kwa pamoja (wakubwa na wadogo) wanaTRADE zaidi ya US Dollars Trilioni 5.3 kila siku!
  4. Hii biashara kwa kuwa ni ya mtandaoni, ukitaka kuifanya ni lazima uwe na fedha mtandaoni. Unafungua account mtandaoni kama unavyofungua bank, unaweka fedha zako. Unazifanyia biashara na siku ukitaka kuzitoa, unazitoa mtandaoni zinakuwa cash za kutumia.
  5. Biashara hii, kwa kuwa ni ya mtandaoni, unaweza kuifanyia popote! Nyumbani, chumbani, njiani, sokoni..popote! Unahitaji tu vitu vitatu:
    • Computer/Laptop ambayo itakusaidia kuliangalia soko na kujua muelekeo (Market Analysis) 
    • Internet connection. Kwa sababu ni biashara ya mtandaoni, unahitaji kujiung na mtandao.
    • Programu maalum yenye uwezo wa kusoma soko. Hii inaitwa Trading Platform. Hii ni software ambayo, unai~download na kui~install kwenye Computer yako. Hizi ziko nyingi sasa lakn moja maarufu ambayo inatumika sana duniani inaitwa Meter Trader 4 (MT4).

Note 1:
Ni lazima uwe na Computer/Laptop au smartphone na u-install MT4 kama unafanya Market Analysis mwenyewe lkn, kama kuna mtu mwingine anaweza kufanya kwa niaba yako na akakupa kile tunaita Trading Signal, sio lazima uwe na computer, unaweza tu ukawa na simu yako au gadget yoyote ile inayoweza kuunganishwa na mtandao. Note 2:
Baada ya kutimiza hayo, kabla hujaanza KUNUNUA NA KUUZA fedha za kigeni mtandaoni, Ku Trade Forex, unamuhitaji mtukati anayeitwa Broker. Kwanini? Nitafafanua zaidi pale chini lakini, kwa hapa niseme tu, ndiye anayesimama kama bank ya mtandaoni kwako. Utafungua account kwake kama unavyofungua account NMB, NBC, Equity, Exim, n.k. Utampatia taarifa zako zote rasmi, Vitambulisho vyote muhimu, Uraia, Anuani ya unapoishi,...kila kitu. Ndipo atakuruhusu kufungua account ya mtandaoni. Niwaonye wanaopenda kudanganya, hapa usijaribu, utafeli. Hapa wanahitaji taarifa zako halisi na sahihi. Hii ni kwa sababu, hii ni biashara halali kabisa, na ni ya dunia nzima na, inakupatia kipato halali. Sasa, siku umepata faida unataka kuzitoa pesa zako, watakuambia hatukupi maana si wewe, endapo utawasilisha utambulisho mwingine tofauti na ule uliojazaga. Baada ya kuifungua account kwa Broker, unaweka hela zako humo, labda USD, GBP, JPY..utakavyo mwenyewe.

Baada ya hapo, sasa upo tayari kuanza biashara.

Forex ni nini?


Katika kuanza biashara ya Forex, jambo kubwa na la muhimu ni kuhakikisha una trade kupitia broker ambaye yupo regulated, na anaaminika zaidi ili kuepuka matatizo mbali mbali yanayotokana na ku trade kupitia broker asiye na sifa.

Bofya link ifuatayo kutengeneza account kupitia broker anayeheshimika zaidi duniani na mwenye clients zaidi ya 2 milion kutoka nchi mbali mbali duniani ikiwemo Tanzania na Kenya na nchi zote za Afrika Mashariki.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT


Zinazosomwa Zaidi

Followers