Showing posts with label TemplerFx. Show all posts
Showing posts with label TemplerFx. Show all posts

Jinsi ya kuweka na kufunga order ya Forex kwa kutumia MT4

Karibu tena tuendelee kupeana elimu kuhusu mambo mbali mbali yahusuyo biashara ya Forex. Leo tutaenda kuangalia jinsi ya kuweka na kufunga order kwa kutumia programu ya Meta Trader 4 au kwa kifupi MT4 kama ilivyozoeleka.

Jinsi ya kuweka na kufunga order ya Forex kwa kutumia MT4

Kama ambavyo tulisoma kwenye makala ihusuyo jinsi ya kutumia MT4 inayopatikana  >> HAPA << leo tutajifunza juu ya namna ya kuweka na kufunga order za forex kwenye programu hii ya MT4. MT4, ni programu maalumu iliyotengenezwa kukuwezesha kuweka order (position) za forex, pamoja na kuwa na chart mbali mbali ambazo zinaonesha historia ya pair fulani ya Forex kwa nyakati zilizopita, ambapo historia hiyo, inaweza kukusaidia kufanya uchambuzi juu ya uelekeo wa pair husika.

Programu hii ya MT4, inaweza kutumiaka kwenye simu yako ya mkononi, au kwenye computer yako, kuipata programu hii kwenye simu yako ya mkononi, iwapo unatumia simu zenye mfumo wa Android, nenda kwenye PLAY STORE na tafuta neno meta trader 4 au mt4, na utaiona, kisha install, na iwapo unatumia simu za iPhone, vivyo hivyo nenda kwenye App Store ya simu yako, kisha tafuta neno MT4 au Meta Trader 4, kisha install.

Iwapo unatumia computer, login kwenye account yako ya Forex kwa broker uliyejiunga naye, halafu nenda kwenye menu ya DOWNLOADS, kisha chagua version ya Meta Trader 4 inayoendana na computer unayotumia, yaani kama ni Windows, au kama ni Mac, baada ya hapo uta install kama unavyo install programu nyingine kwenye computer yako.

Kama bado huna account ya Forex, bofya link ifuatayo ili utengeneze account kwa broker tunayemtumia zaidi Africa Mashariki wa TEMPLER FX

BOFYA HAPA KUTENGENEZA ACCOUNT

Ukishafanikiwa ku install program ya MT4, sasa yafuatayo ni maelekezo ya jinsi ya kufungua na kufunga order (au position)

Kufunga na kufunga order kwa kutumia computer

Kwenye kufungua order, kuna vitendo vikuu viwili kwenye pair husika, ni aidha unanunua yaani BUY au unauza yaani SELL pair husika.

Kwenye ku BUY au ku SELL kuna order za aina kuu mbili ambazo ni INSTANT na ya pili ni PENDING:
  1. BUY or SELL kwa kutumia instant execution 
  2. BUY or SELL kwa kutumia pending order
Hatua ya kwanza unapaswa kufanya, ni kufungua programu yako ya META TRADER 4, na ukiangalia kwenye menu iliyoko juu, utaona kitufe kimeandikwa NEW ORDER, bofya kitufe hicho kama inavyoonekana pichani, halafu utaona order za aina mbili either instant execution, ambayo ni order inayojazwa muda huo huo, au pending order ambayo ni order inayojazwa baada ya bei husika uliyoweka kufikiwa

Meta Trader 4 open order

Kabla hujabofya kutufe cha SELL au BUY, kuna sehemu za kuangalia, nazo ni kama zifuatazo:
Symbol, hii ni PAIR ambayo unatarajia ku deal nayo either kwa ku SELL au kwa ku BUY

ya pili ni Volume volume au ujazo kwa jina lingine inaitwa LOT SIZE, hiki ni kiwango ambacho unakitumia kulingana na mtaji ulio nao, kwa mfano kama unaanza kwa mtaji mdogo, unashauriwa kuweka volume ya chini kabisa, ambayo ni 0.01. na utakuwa unaiongeza kulingana na jinsi mtaji wako unavyokua.

Kingine cha muhimu ni  Stop Loss pamoja na Take Profit, stop loss au SL, ni kiwango unachotarajia kukiweka, kwamba iwapo pair imeenda kinyume na matarajio yako, basi utakua tayari kupoteza kiwango flani kwa kuamua kuweka stop loss.

Ya tatu ndio sehemu ya kuchagua kama ni Instant Execution au ni Pending order.

Ukishajiridhisha na taarifa ulizo jaza, uta bofya button ya BUY au SELL kulingana na jinsi unavyo predict uelekeo wa soko kwa pair uliyoamua ku deal nayo.

Mara baada ya kubofya SELL au BUY, ikishakua executed, utaona order yako ikiwa inaendelea either  kukua, iwapo ulienda uelekeo sahihi, au ikiendelea kuwa ndogo iwapo ulienda uelekeo ambao sio, na uki right click kwenye order hiyo, una uwezo wa kuifunga kwa kubofya CLOSE

Makala ifuatayo, tutajifunza zaidi jinsi ya kutumia MT4 version ya simu.

Jinsi ya ku-verify account yako ya Templerfx (Full Verification)

Ni matumaini yangu kwamba unaendelea vyema na safari yako ya mafanikio kupitia biashara ya Forex.

Jinsi ya kuverify account ya forex

Leo tutaenda kuangalia ni namna gani ya kuweza kupata full verification templerfx account, ambayo itakuwezesha kufanya mambo mbali mbali kwa uwepesi ikiwepo kuwa na njia nyingi zaidi za ku deposit na ku withdraw pamoja na kuwa na uwezo wa kuomba salio la bure la dola 30 za kuanzia ku trade Forex (No Deposit Bonus)

Ikiwa umeshatengeneza account yako ya Forex, utaona kwamba unatakiwa ufanye verification (uthibitisho) katika maeneo makuu matano, na iwapo bado huna account ya Forex, basi bonyeza kutufe kifuatacho kutengeneza account hiyo bure kabisa:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Kama tayari una account ambayo haijawa verified, utatakiwa kufanya verification ya:
  1. Email Address
  2. Namba yako ya simu
  3. Kitambulisho chako (Identity Verification)
  4. Address Vefirication (Uthibitisho wa makazi) 
  5. Credit Card Verification (Uthibitisho wa kadi yako ya bank)
Ukishatengeneza account yako ya templerfx, utapaswa ku login kwenye account yako na kwenda kwenye menu, kisha bofya sehemu iliyoandikwa My TemplerFx na kwa chini yake utaona sehemu imeandikwa Verification, bofya sehemu hiyo, na fuata maelekezo kwa vipengele vyote vitano, ingawa vipengele muhimu ni vitatu, yaani Email, Namba ya simu na Identity verification.


Jinsi ya kuverify

1. Kuthibitisha Barua pepe (email)

Hii itakupasa kwenda kwenye inbox yako ya Email, na utabofya link utakayotumiwa ku-confirm email address yako.

2. Kuthibitisha Namba yako ya simu

Hi itakupasa kubofya kitufe cha ku verify namba yako ya simu, halafu automatically utatumiwa SMS yenye namba ya uthibitisho, nakili namba hiyo halafu iandike kwenye kibox utakachoulizwa, baadae bofya confirm, na namba yako itakuwa imeshathibitishwa na utaona tick la kijani.

3. Kuthibitisha Kitambulisho chako.

Kuthibitisha kitambulisho chako (Identity Verification) utapaswa kupiga picha kitambulisho chako kinachokubalika kwa mfano Leseni ya Udereva, kitambulisho cha mpiga kura, passport au kitambulisho cha uraia. Halafu utaki-upload kitambulisho hicho kwa ku bofya sehemu iliyoandikwa "Upload Identity" itakuchukua masaa kadhaa kuthibitishwa, na ukishathibitishwa utaona tick ya kijani kwamba umeshathibitishwa.

4. Kuthibitisha Anuani ya Makazi.

Kuthibitisha anuani ya makazi ni jambo muhimu kwenye biashara ya forex, na ni sehemu ya kitu kinachoitwa KYC au Know Your Customer. Njia rahisi ya kuthibitisha anuani ya makazi, ni kwenda kuomba statement ya account yako ya bank hata ya muda mfupi, hakikisha statement hiyo ina jina lako kamili na anuani yako, halafu utai upload statement hiyo na baadae account yako itapata address verification ambapo utaona umewekewa tick ya kijani.

5. Kuthibitisha kadi ya bank

Mwisho kabisa utatakiwa kuthibitisha kadi yako ya bank, hii ni muhimu pale unapotaka kuomba dola 30, za kuanza ku trade Forex (No Deposit Bonus) na pia ni muhimu pale unapotaka ku deposit kwa kutumia njia ya SKRILL

Ukifanikiwa kufuata vipengele vyote vya uthibitisho wa account yako kama nilivyoeleza hapo juu, utakuwa umefanikiwa kuwa na FULL VERIFIED templerfx account ambayo itakuwezesha ku trade forex na kutumia huduma zote zinazotolewa na broker wako.

Iwapo huna account ya Forex hadi sasa, usisite kuanza kwa kusoma post hii inayoelezea jinsi ya kujiunga na forex:

Jinsi ya kujiunga na biashara ya Forex

Na iwapo ungependa kufungua account ya Forex, bofya kitufe kifuatacho:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Endelea kuwa pamoja nami katika kujifunza mbinu mbali mbali za mafanikio kupitia Forex

Jinsi ya kutoa pesa Skrill kwenda M-Pesa Tanzania

Katika post hii tutaona njia unayoweza kuitumia kuhamisha pesa kutoka Skrill kwenda M-Pesa Tanzania. Skrill ni moja kati ya huduma nzuri kabisa za kutuma, kupokea pesa na kufanya malipo mtandaoni.

Skrill to M-Pesa Tanzania


Kama bado hujajiunga na huduma hii, bofya kitufe kifuatacho kufungua account Skrill.

 

Au waweza soma post hii kuhusu jinsi ya kufungua account Skrill:

Jinsi ya kufungua account Skrill

Kama tayari una account Skrill, na unajiuliza ni mbinu gani utumie kuhamisha pesa zako kwenda M-Pesa Tanzania, ungana nami katika mtiririko huu:

Cha kwanza kabisa hakikisha una account ya Forex ambayo iko Verified kwa broker wa TemplerFX, kama bado huna, account TemplerFX, hakikisha unatengeneza account kwa kubofya kitufe kifuatacho:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

  • Ukishafungua account, hakikisha umei verify, kwa ku upload vitambulisho vyako, pamoja na ku verify card yako ya bank (utaelekezwa kufuta baadhi ya namba zilizopo kwenye card yako ya bank)
  • Ukishakua na full verified TemplerFx account, nenda kwenye sehemu ya ku deposit pesa, ambapo utaona njia mbali mbali za ku deposit
  • Chagua Skrill kama njia ya ku deposit
  • Deposit kiasi cha pesa unachotaka, nacho kitahamishwa muda huo huo kutoka Skrill kwenda TemplerFx.
  • Kiasi chako cha pesa kikishaingia TemplerFx, waweza sasa ukachagua ku withdraw, ambapo utachagua njia ya wallet, ambayo itakuelekeza hatua zifuatazo, na wewe utachagua M-Pesa, kisha utachagua namba yako ya M-Pesa na baada ya hapo muda huo huo kiasi hicho cha pesa kitakua kimehamishwa kutoka TemplerFX kwenda kwenye namba yako ya M-Pesa.
Kama umefurahishwa na post hii, usisahau ku share kuwafahamisha wengine.

Jinsi ya kuweka hela Forex

Baada ya kufahamu jinsi ya kutumia M Pesa kuweka hela kwenye account yako ya Forex chini ya broker maarufu East Africa anayefahamika kwa jina la TemplerFX sasa ni wakati wa kujifunza hatua kwa hatua ni namna gani unaweza ukaweka hela kwenye account yako ya Forex.

Jinsi ya kuweka hela Forex
Jinsi ya kuweka hela Forex


Zipo namna nyingi za kuweka hela kwenye account ya Forex kutegemea na broker unayemtumia, wengine wanatumia M-Pesa, PayPal, Visa card au Mastercard, Skrill na baadhi ya njia nyingine za kutuma na kupokea pesa kwa kupitia mtandao.

Kwa kuwa Watanzania walio wengi ni watumiaji wa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu, basi tutaenda kujifunza kuweka pesa kwa kutumia M-Pesa.

Kama umeamua kuwa serious na biashara ya Forex, basi ni vyema ukawa na bank account maalum ambayo utaitumia kuweka na kutoa fedha kwa kupitia Visa au Mastercard, njia hizi utaziona pindi unapo bofya kwenye link ya DEPOSIT katika members area ya account yako ya forex.

Na iwapo unalazimika kutumia M-Pesa, basi huna budi kujiunga na broker aitwaye TEMPLERFX kwa kubofya hapa chini:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT
Maelekezo yote ya namna ya kutumia mtandao wa M-Pesa kupitia huduma ya Ipay Africa nimeyaweka kwenye article ifuatayo, bofya link then utaona ni jinsi gani unaweza kuweka hela kwenye account yako ya Forex kwa kutumia M Pesa.

Jinsi ya kuweka hela Forex kwa kupitia M Pesa

Nimatumaini kwamba makala hii imeweza kukuelekeza vizuri namna ambayo waweza itumia kuweka hela kwenye Forex

Na iwapo ungependa kuweka pesa kwa kutumia huduma ya Skrill, bofya link ifuatayo kufungua account Skrill

FUNGUA SKRILL ACCOUNT

Jinsi ya kutumia M-Pesa kuweka na kutoa fedha katika Forex

NOTE:
Huduma ya ku deposit na ku withdraw kwa kutumia M-Pesa Tanzania kupitia Broker TemplerFx kwa sasa imesitishwa hadi hapo iPay na Vodacom watakapokamilisha taratibu zilizowekwa na BOT.
Huduma hii inaendelea kupatikana kupitia Safaricom M-Pesa Kenya ambapo waweza ku deposit au ku withdraw kwa kuchagua M-Pesa Kenya.
Kama bado huna account ya Forex kupitia TemplerFx, bofya kitufe kifuatacho kujiunga:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Moja kati ya changamoto nyingi zinazoikumba biashara ya Forex hususani kwa nchi zinazoendelea ni namna bora ya kuweka na kutoa pesa kwenye account yako ya Forex.

Templer fx M Pesa
Templer Fx M Pesa

Jambo hili kwa kawaida huwa linasimamiwa na broker uliyeamua kumtumia. Brokers walio wengi wanakuwezesha kuweka pesa kwenye account yako kwa kupitia njia ya Bank kupitia credit cards kwa mfano Visa au Mastercard.

Jambo zuri kwa forex Traders wa East Africa ni kwamba yupo broker ambaye anakuwezesha kuweka na kutoa pesa kwa kutumia Vodacom M-Pesa papo kwa papo. Broker huyu si mwingine bali ni TemplerFx ambaye anatumia huduma ya iPay Africa kukuwezesha kuweka na kutoa pesa kwenye account yako ya M Pesa muda wowote. Sasa tukaangalie ni kwa jinsi gani unaweza kutumia huduma hii.

Bofya kitufe kifuatacha kujiunga na Templer Forex kutumia huduma ya M-Pesa kuweka na kutoa pesa kwenye Forex:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Jinsi ya kuweka na kutoa pesa Templer Fx kwa M Pesa:

Ikiwa umeshajiunga na tayari una account ya templerfx ambayo ni verified. Fuata mtiririko ufuatao:
  1. Kwa kutumia computer yako, Login kwenye account yako ya TemplerFx
  2. Kwenye menu ya upande wa kushoto, bofya palipoandikwa Finance
  3. Chini yake utaona Deposits, bofya link hiyo.
  4. Kwenye ukurasa utakaofunguka, chagua account unayotaka ku-deposit, na iwapo bado hujatengeneza account, utaambiwa utengeneze account.
  5. Ukishachagua account, bofya sehemu iliyoandikwa Select a payment System
  6. Chagua palipoandikwa IPay Africa
  7. Baada ya hapo utachagua Method of payment
  8. Hapo sasa utachagua M-Pesa Tanzania, iwapo upo Tanzania au M-Pesa Kenya iwapo upo Kenya
Baada ya hapo, fuata maelekezo yafuata jinsi ya kulipa pesa, na muda huo huo ukishalipa utaona balance yako kwenye account yako ya TemplerFx

Zinazosomwa Zaidi

Followers