Showing posts with label Meta Trader 4. Show all posts
Showing posts with label Meta Trader 4. Show all posts

Jinsi ya kuweka na kufunga order ya Forex kwa kutumia MT4

Karibu tena tuendelee kupeana elimu kuhusu mambo mbali mbali yahusuyo biashara ya Forex. Leo tutaenda kuangalia jinsi ya kuweka na kufunga order kwa kutumia programu ya Meta Trader 4 au kwa kifupi MT4 kama ilivyozoeleka.

Jinsi ya kuweka na kufunga order ya Forex kwa kutumia MT4

Kama ambavyo tulisoma kwenye makala ihusuyo jinsi ya kutumia MT4 inayopatikana  >> HAPA << leo tutajifunza juu ya namna ya kuweka na kufunga order za forex kwenye programu hii ya MT4. MT4, ni programu maalumu iliyotengenezwa kukuwezesha kuweka order (position) za forex, pamoja na kuwa na chart mbali mbali ambazo zinaonesha historia ya pair fulani ya Forex kwa nyakati zilizopita, ambapo historia hiyo, inaweza kukusaidia kufanya uchambuzi juu ya uelekeo wa pair husika.

Programu hii ya MT4, inaweza kutumiaka kwenye simu yako ya mkononi, au kwenye computer yako, kuipata programu hii kwenye simu yako ya mkononi, iwapo unatumia simu zenye mfumo wa Android, nenda kwenye PLAY STORE na tafuta neno meta trader 4 au mt4, na utaiona, kisha install, na iwapo unatumia simu za iPhone, vivyo hivyo nenda kwenye App Store ya simu yako, kisha tafuta neno MT4 au Meta Trader 4, kisha install.

Iwapo unatumia computer, login kwenye account yako ya Forex kwa broker uliyejiunga naye, halafu nenda kwenye menu ya DOWNLOADS, kisha chagua version ya Meta Trader 4 inayoendana na computer unayotumia, yaani kama ni Windows, au kama ni Mac, baada ya hapo uta install kama unavyo install programu nyingine kwenye computer yako.

Kama bado huna account ya Forex, bofya link ifuatayo ili utengeneze account kwa broker tunayemtumia zaidi Africa Mashariki wa TEMPLER FX

BOFYA HAPA KUTENGENEZA ACCOUNT

Ukishafanikiwa ku install program ya MT4, sasa yafuatayo ni maelekezo ya jinsi ya kufungua na kufunga order (au position)

Kufunga na kufunga order kwa kutumia computer

Kwenye kufungua order, kuna vitendo vikuu viwili kwenye pair husika, ni aidha unanunua yaani BUY au unauza yaani SELL pair husika.

Kwenye ku BUY au ku SELL kuna order za aina kuu mbili ambazo ni INSTANT na ya pili ni PENDING:
  1. BUY or SELL kwa kutumia instant execution 
  2. BUY or SELL kwa kutumia pending order
Hatua ya kwanza unapaswa kufanya, ni kufungua programu yako ya META TRADER 4, na ukiangalia kwenye menu iliyoko juu, utaona kitufe kimeandikwa NEW ORDER, bofya kitufe hicho kama inavyoonekana pichani, halafu utaona order za aina mbili either instant execution, ambayo ni order inayojazwa muda huo huo, au pending order ambayo ni order inayojazwa baada ya bei husika uliyoweka kufikiwa

Meta Trader 4 open order

Kabla hujabofya kutufe cha SELL au BUY, kuna sehemu za kuangalia, nazo ni kama zifuatazo:
Symbol, hii ni PAIR ambayo unatarajia ku deal nayo either kwa ku SELL au kwa ku BUY

ya pili ni Volume volume au ujazo kwa jina lingine inaitwa LOT SIZE, hiki ni kiwango ambacho unakitumia kulingana na mtaji ulio nao, kwa mfano kama unaanza kwa mtaji mdogo, unashauriwa kuweka volume ya chini kabisa, ambayo ni 0.01. na utakuwa unaiongeza kulingana na jinsi mtaji wako unavyokua.

Kingine cha muhimu ni  Stop Loss pamoja na Take Profit, stop loss au SL, ni kiwango unachotarajia kukiweka, kwamba iwapo pair imeenda kinyume na matarajio yako, basi utakua tayari kupoteza kiwango flani kwa kuamua kuweka stop loss.

Ya tatu ndio sehemu ya kuchagua kama ni Instant Execution au ni Pending order.

Ukishajiridhisha na taarifa ulizo jaza, uta bofya button ya BUY au SELL kulingana na jinsi unavyo predict uelekeo wa soko kwa pair uliyoamua ku deal nayo.

Mara baada ya kubofya SELL au BUY, ikishakua executed, utaona order yako ikiwa inaendelea either  kukua, iwapo ulienda uelekeo sahihi, au ikiendelea kuwa ndogo iwapo ulienda uelekeo ambao sio, na uki right click kwenye order hiyo, una uwezo wa kuifunga kwa kubofya CLOSE

Makala ifuatayo, tutajifunza zaidi jinsi ya kutumia MT4 version ya simu.

Jinsi ya kutumia Metatrader 4 mt4 ku trade Forex

Makala hii itaenda kukuelimisha jinsi ya kutumia program ya Metatrader 4 au kwa kifupi mt4 kukuwezesha kufanya biashara ya Forex.

Jinsi ya kutumia Metatrader 4 mt4 ku trade Forex


Metatrader ni program maalum inayotumika kuwezesha ufanyaji wa biashara ya Forex yaani kufungua position, pamoja na kukupatia chart ambazo zitakuwezesha kuona uelekeo au historia ya pair za Forex na pia kukuwezesha kufanya uchambuzi wa pair hizo kwa kitaalam technical analysis.

Kuanza kutumia program hii, yakupasa uwe na account katika moja ya broker utakayemtumia ku trade Forex.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Metatrader ina version kuu mbili, Metatrader 4 na Metatrader 5, hizi ni programu mbili tofauti na haimaanishi kwamba Metatrader 5 ni toleo la juu la metatrader 4, la hasha. Hizi ni program tofauti kabisa, ingawa zinatengenezwa na kampuni moja, na programu ambayo inatumika zaidi kwa biashara ya Forex, ni Metatrader 4 au kwa kifupi MT4.

Jinsi ya ku-install Metatrader4

Program ya Metatrader 4 inapatikana katika vifaa vyote tunavyotumia ku trade Forex yaani simu, PC pamoja na Mac. Zipo version za mt4 za Android, iOS na hata Windows kwa ajili ya computer yako.

Kuweza kutumia vyema program hii ya Metatrader 4, yakupasa uwe umeshafungua account kwa broker unayemtumia.

Ukishatengeneza account, aidha kwa kutumia simu yako ya mkononi au kwa kutumia computer yako, fungua menu, au angalia menu iliyopo upande wa kushoto, utaona menu imeandikwa Downloads, bofya sehemu hiyo kisha bofya sehemu iliyoandikwa Platforms na utaona maelekezo pamoja na orodha za platform ambazo unatumia ili u download program hii ya Metatrader 4. Kama unatumia windows computer, bofya sehemu iliyoandikwa  TemplerFX trader on windows, na kama unatumia simu ya mkononi, nenda moja kwa moja kwenye PlayStore kama unatumia Android, au AppStore kama unatumia iPhone au iPad, kisha search neno MT4 au neno Metatrader4 ambapo utaona program hii, na utai install.

Ukisha install, utaona option ya kufungua Demo account, ambapo una uhuru wa kufungua default demo account kutoka kwa watengenezaji wa program ya mt4, au waweza ingiza taarifa za demo account za broker wako.

Kama hutapenda kuweka demo account, una uhuru wa kuweka login na password zako za account yako uliyotengeneza kwa broker wako.

Kumbuka kwamba, taarifa zako za ku login, zipo kwenye site ya broker wako, kama unatumia broker wa templerfx, basi kupata taarifa zote, login kwenye site ya templerfx, halafu kwenye menu kuu, bofya sehemu iliyoandikwa Open an Account halafu chini yake, bofya new account.  Kwenye orodha ya account za kutengeneza, utaulizwa uchague aina ya account ya kutengeneza, chagua yoyote inayokufaa kati ya either DEMO ACCOUNT (kama hupo tayari kuanza na real account) au chagua LIVE UNIVERSAL FX kutengeneza live/real forex account.

Jinsi ta kufungua account ya mt4

Mara baada ya kutengeneza, utapewa Login Id, na Password. Ambazo sasa, ndio unazopaswa kuzitumia ku login kwenye program yako ya Metatrader 4.

Endelea kuwa nasi katika makala hii ambayo itaendelea kukufundisha jinsi ya kutumia menu mbali mbali zilizopo kwenye program uliyo install ya Metatrader 4.

Napenda kukufahamisha tena, kama huna account bado, bofya link ifuatayo kutengeneza account yako ya Forex.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Kama una maoni, ushauri, au swali, usiache kutushirikisha kwa kuandika kwenye sehemu ya comments, au kuwasiliana nasi kwa kubofya menu ya Telegram hapo juu.

Namna ya kufanya biashara ya Forex

Karibu katika site yetu hii ambapo kama kawaida tunaendelea na mfululizo wa masomo mbali mbali kuhusu namna bora ya kufanya biashara ya Forex kwa faida.

Jinsi ya kufanya biashara ya Forex

Tukumbuke kwamba biashara ya Forex ndio biashara kubwa kuliko zote duniani ambayo ina mzunguko wa zaidi ya trillion 5 za kimarekani kwa siku.

Iwapo utafanya maamuzi sahihi, na kuamua kujifunza vyema biashara hii, basi nawe utakua miongoni mwa watu wanaonufaika vyema na biashara hii duniani kote.

Jambo la msingi kufahamu ni kwamba, Forex ni biashara ya kubadilisha Fedha za kigeni, biashara hii hufanyika kwa njia mbali mbali, lakini pale unapotaka kuifanya kwa faida, basi utaifanya mtandaoni kwa kufungua account kwa taasisi zinazokuwezesha ku nunua na kuuza pair mbali mbali za Forex katika masoko makuu ya Forex duniani.

Masoko haya yanayokuwezesha kuuza na kununua, yameunganishwa kwa mtandao maalum unaojulikana kama ECN yaani Electronic Communication Network.

Iwapo ungependa kuanza biashara hii ya Forex, basi itakulazimu kuanza kwa kufungua account kwa broker atakayekuwezesha kununua na kuuza pamoja na kukuwezesha ku withdraw faida utakayokua umeipata baada ya kujiunga na Forex.

Yupo broker ambaye tunamtumia kwa Africa Mashariki, ambaye bahati nzuri naye anakupatia dola 30 za bure za kuanza kufanya biashara hii, na pindi utakapofanikiwa kufikisha vigezo vyao, utaweza ku withdraw hadi dola 100 bure kabisa.

Kujiunga na biashara hii ya Forex kupitia broker wa TemplerFX, bonyeza kitufe kifuatacho kutengeneza account, kisha kwenye fomu itakayofunguliwa, fuata maelekezo yote ikiwa ni pamoja na kujaza taarifa zako, na baadae utapaswa ku upload copy za kitambulisho wako ili kuthibitisha au ku verify identity yako.

Bofya kitufe kifuatacha kujiunga na Forex:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Ukishamaliza kutengeneza account yako, endelea kuperuzi site hii ambapo tumekupatia maelekezo mbali mbali kabisa na mepesi ambayo yatakuwezesha kukupa elimu ya awali ya biashara hii ya Forex.

Jinsi ya kufungua na kutumia DEMO account kwenye Forex

Jinsi ya kufungua na kutumia DEMO account kwenye Forex

Kama tulivyokwisha ona umuhimu wa kuwa na ujuzi wa kutosha kabla hujaanza rasmi ku trade Forex kwa kutumia real account, ni muhimu kuanza na practice account ambayo itakuwezesha kufahamu trend ya soko, na taratibu mbali mbali za ku trade Forex.

Jinsi ya kufungua demo account

Forex Demo Account ni nini?

Forex demo account ni aina ya account maalum ya Forex ambayo inatolewa na wawezeshaji (trading platform au broker wako) ambayo imewekewa kiasi cha pesa ambazo sio halisi kwa ajili ya wewe kujifunza namna ya kufanya biashara ya Forex.

Tofauti ya Demo account na Real account ni kwamba Demo account imewekewa kiasi cha pesa ambacho ni fake, wakati account halisi au real account ni account ambayo umeiwekea pesa halali.

Njia rahisi kabisa ya kufungua account ya demo, ni ku download program ya Meta Trader 4 kwenye simu yako au kwenye computer yako, na baada ya ku install programu hiyo, automatically itakutengenezea account ya demo ambayo waweza itumia kufanya trading za majaribio wakati ukiendelea kujifunza. Iwapo ungepende kufungua LIVE account, basi bofya kitufe kifuatacho:
BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT
Ambapo utaweza kufungua REAL account kwa broker TemplerFx

Zinazosomwa Zaidi

Followers