Showing posts with label Jifunze Forex. Show all posts
Showing posts with label Jifunze Forex. Show all posts

Jinsi ya kuweka na kufunga order ya Forex kwa kutumia MT4

Karibu tena tuendelee kupeana elimu kuhusu mambo mbali mbali yahusuyo biashara ya Forex. Leo tutaenda kuangalia jinsi ya kuweka na kufunga order kwa kutumia programu ya Meta Trader 4 au kwa kifupi MT4 kama ilivyozoeleka.

Jinsi ya kuweka na kufunga order ya Forex kwa kutumia MT4

Kama ambavyo tulisoma kwenye makala ihusuyo jinsi ya kutumia MT4 inayopatikana  >> HAPA << leo tutajifunza juu ya namna ya kuweka na kufunga order za forex kwenye programu hii ya MT4. MT4, ni programu maalumu iliyotengenezwa kukuwezesha kuweka order (position) za forex, pamoja na kuwa na chart mbali mbali ambazo zinaonesha historia ya pair fulani ya Forex kwa nyakati zilizopita, ambapo historia hiyo, inaweza kukusaidia kufanya uchambuzi juu ya uelekeo wa pair husika.

Programu hii ya MT4, inaweza kutumiaka kwenye simu yako ya mkononi, au kwenye computer yako, kuipata programu hii kwenye simu yako ya mkononi, iwapo unatumia simu zenye mfumo wa Android, nenda kwenye PLAY STORE na tafuta neno meta trader 4 au mt4, na utaiona, kisha install, na iwapo unatumia simu za iPhone, vivyo hivyo nenda kwenye App Store ya simu yako, kisha tafuta neno MT4 au Meta Trader 4, kisha install.

Iwapo unatumia computer, login kwenye account yako ya Forex kwa broker uliyejiunga naye, halafu nenda kwenye menu ya DOWNLOADS, kisha chagua version ya Meta Trader 4 inayoendana na computer unayotumia, yaani kama ni Windows, au kama ni Mac, baada ya hapo uta install kama unavyo install programu nyingine kwenye computer yako.

Kama bado huna account ya Forex, bofya link ifuatayo ili utengeneze account kwa broker tunayemtumia zaidi Africa Mashariki wa TEMPLER FX

BOFYA HAPA KUTENGENEZA ACCOUNT

Ukishafanikiwa ku install program ya MT4, sasa yafuatayo ni maelekezo ya jinsi ya kufungua na kufunga order (au position)

Kufunga na kufunga order kwa kutumia computer

Kwenye kufungua order, kuna vitendo vikuu viwili kwenye pair husika, ni aidha unanunua yaani BUY au unauza yaani SELL pair husika.

Kwenye ku BUY au ku SELL kuna order za aina kuu mbili ambazo ni INSTANT na ya pili ni PENDING:
  1. BUY or SELL kwa kutumia instant execution 
  2. BUY or SELL kwa kutumia pending order
Hatua ya kwanza unapaswa kufanya, ni kufungua programu yako ya META TRADER 4, na ukiangalia kwenye menu iliyoko juu, utaona kitufe kimeandikwa NEW ORDER, bofya kitufe hicho kama inavyoonekana pichani, halafu utaona order za aina mbili either instant execution, ambayo ni order inayojazwa muda huo huo, au pending order ambayo ni order inayojazwa baada ya bei husika uliyoweka kufikiwa

Meta Trader 4 open order

Kabla hujabofya kutufe cha SELL au BUY, kuna sehemu za kuangalia, nazo ni kama zifuatazo:
Symbol, hii ni PAIR ambayo unatarajia ku deal nayo either kwa ku SELL au kwa ku BUY

ya pili ni Volume volume au ujazo kwa jina lingine inaitwa LOT SIZE, hiki ni kiwango ambacho unakitumia kulingana na mtaji ulio nao, kwa mfano kama unaanza kwa mtaji mdogo, unashauriwa kuweka volume ya chini kabisa, ambayo ni 0.01. na utakuwa unaiongeza kulingana na jinsi mtaji wako unavyokua.

Kingine cha muhimu ni  Stop Loss pamoja na Take Profit, stop loss au SL, ni kiwango unachotarajia kukiweka, kwamba iwapo pair imeenda kinyume na matarajio yako, basi utakua tayari kupoteza kiwango flani kwa kuamua kuweka stop loss.

Ya tatu ndio sehemu ya kuchagua kama ni Instant Execution au ni Pending order.

Ukishajiridhisha na taarifa ulizo jaza, uta bofya button ya BUY au SELL kulingana na jinsi unavyo predict uelekeo wa soko kwa pair uliyoamua ku deal nayo.

Mara baada ya kubofya SELL au BUY, ikishakua executed, utaona order yako ikiwa inaendelea either  kukua, iwapo ulienda uelekeo sahihi, au ikiendelea kuwa ndogo iwapo ulienda uelekeo ambao sio, na uki right click kwenye order hiyo, una uwezo wa kuifunga kwa kubofya CLOSE

Makala ifuatayo, tutajifunza zaidi jinsi ya kutumia MT4 version ya simu.

Jinsi ya kuanza biashara ya Forex bila mtaji

Wapo watu wengi wanatamani kuanza biashara hii ya Forex lakini wengi wamekua na kikwazo kwenye mtaji wa kuanzia  biashara hii kubwa duniani.
Habari njema ni kwamba, wapo baadhi ya brokers ambao wanakupatia kianzio cha bure kabisa ambacho kitakuwezesha kupata pesa ya bure kabisa kuanza biashara hii ya Forex, na kwa bahati nzuri, hapa kwetu Tanzania yupo broker ambaye atakupatia bure kabisa dola 30, ambayo inaitwa NO DEPOSIT BONUS, utakachopaswa kufanya ni kuanza kukuza kiwango hicho hadi kufikia dola 100 na utakuwa na uwezo wa kui withdraw.

Free 30 USD Templer Forex

Ili kuweza kupata kianzio hichi cha bure cha dola 30, jiunge na Forex kwa broker wa templer kwa kufuata kitufe kifuatacho:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Ukishatengeneza account yako ya Forex, fuata hatua zifuazo ili ku-request dola 30 za bure:
  • Login kwenye dashboard yako ya Templer Fx
  • Ukisha login, kwenye menu kuu iliyopo upande wa kushoto chagua BONUS
  • Click request NBD 30$ ambapo utapatiwa login id, pamoja na password ya kulogin kwenye mt4
No deposit bonus templerfx

Tayari utakua umeshapata dola 30 za bure kabisa zinazokuwezesha ku trade Forex.

Zifuatazo ni sheria na taratibu za kukuwezesha ku withdraw faida utakayoipata baada ya ku trade kwa NDB.
  • Unatakiwa u trade hizo dola 30 ulizopatiwa, hadi zifike dola 100 ndani ya mwezi mmoja na iwapo utashindwa kufikisha dola 100 ndani ya huo mwezi mmoja, utakua umeshindwa kutimiza vigezo vya No Deposit Bonus.
  • Ndani ya huo mwezi mmoja ambao utapaswa kufikisha dola 100, total lot size/volume inatakiwa isipungue 5 yaani kwa mfano kama una trade kwa lot size ya 0.05, basi kwa ujumla uwe ume fungua na kufunga jumla ya trades 100 ndani ya huo mwezi mzima yaani 5 gawa kwa 0.05
  • Jumla ya positions zinazo run kwa wakati mmoja, zisizidi volume ya 0.3, kwa mfano kama una trade kwa 0.1, basi zitahesabiwa maximum positions 3 ambazo jumla ndio inakua 0.3
Iwapo umefanikiwa kutimiza vigezo vyote hivyo, utapaswa account yako iwe imekua full verified, yaani email, identification, number ya simu na card, then utatuma email au uta chat na mtu wa support aliye online muda wote, ili kuweza ku withdraw amount uliyotengeneza ya dola 100. Kumbuka kwamba, amount utakayopewa kutokana na ku trade No Deposit Bonus ni dola 100 pekee, na utakua na uhuru wa kuamua either kuzi withdraw kabisa, au kuendelea kuzi trade kama mtaji wako mpya. 

Jifunze Forex: Jinsi ya kutambua support and resistance levels

Support and Resistance
Hii ni moja kati ya strategy za awali kabisa katika forex na walimu wengi huwa wanaifundishaga but sisi wanafunzi wengi huwa tukishaanza kujua vitu vingine vya mbele kama trendline na vinginevyo basi huwa tunaipuuza hii strategy, ila kiuhalisia hii ndio strategy mama, nkisema strategy mama namaanisha strategy nyingi za forex zimeanzia hapa.

Jifunze Forex Kiswahili

N.B:
Kama ndio unaanza kujifunza biashara ya Forex, unashauriwa kujiunga kwa kutengeneza account kwa broker anayekubalika zaidi Afrika Mashariki:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Ukishatengeneza account, hakikisha una verify email yako pamoja na namba yako ya simu.
Kwahiyo support na resistance ni muhimu kuijua na kuizingatia coz hii ndio imebeba forex na kuthibitisha hili embu tuongee kuhusu forex kuhusisha na hili.

Kwenye forex huwa kunaforce mbili ambazo ndio hasa zinafanya soko litembee juu au chini na wakati mwingine litulie sehemu moja.

Hizi force ni Demand na Supply

Demand hii ni force ambayo inasababisha price kutoka chini kupanda juu na demand ndio huwa tunawaita buyer yani wanunuzi.

Supply hii nayo ni force ambayo inachukua price kutoka juu nakuishusha chini kuelekea kwa demand na supply kwa maana nyingine ni seller yani wauzaji.

Kwahiyo endapo demand watakua na nguvu kuliko supply basi hapa ndio tunaona soko linamove kutoka chini kwenda juu na endapo supply watakua na nguvu kuliko demand basi hapa ndio tunaona soko linamove kutoka juu kushuka chini nakama supply na demand wako na nguvu sawa basi soko linakua liko katika usawa yani haliendi juu sana wala halishuki sana linakua liko kwenye consolidation.

Kwahiyo wakati demand wananguvu ndio hapa huwa tunabuy na wakati hawa supply wananguvu basi hapa huwa tunasell na pindi supply na demand wakiwa na nguvu sawa hapa huwa tunasubiri maana hatujui wapi soko litaelekea.

Sasa basi ili utambue wapi demand wataanzia na kumalizia na pia ujue wapi supply wataanzia na kumalizia ni lazima utumie support na resistance zones na kwa maelezo haya hapa ndipo tunapata jibu kumbe support na resistance ni zone muhimu ambazo zinatufanya tutambue force ya soko iko vipi.
Kama nlivyosema awali tunabuy kwenye support na kusell kwenye resistance ila je wapi support ilipo na wapi resistance ilipo? Tukasema support iko chini ni mfano wa sakafu na resistance iko juu ni mfano wa paa la nyumba, je ntawezaje sasa kujua hapa ndio niweke support na hapa ndio niweke resistance katika chart yangu? Hili ndio swali ambalo tutaenda kulijadili hapo chini na kabla hayujafika huko kwanza nataka tuangalie movement ya soko huwa iko vipi then tutarudi kwenye sehemu gani yapaswa niweke support na wapi niweke resistance.
Kama tulivyosema awali soko linatembea up au down kutokana na force mbili za demand na supply na kuna wakati pia huwa linatulia sehemu moja.

Kwahiyo kutokana na maelezo hayo basi soko linatrend za aina mbili kuu na moja ni hiyo ya consolidation.

Tuko na uptrend na downtrend

Ambayo uptrend inatokea kipindi demand au buyer wanapokua na nguvu kuliko supply au seller... Na downtrend hutokea kipindi ambacho hao supply au seller wanapokua na nguvu kuliko demand au buyer na pia endapo wote watakua na nguvu sawa basi hapo tunasema soko liko kwenye consolidation.

Sasa hizi trend ndio nataka tuanze nazo kwanza huwa zinakua kua vipi kabla hatujaenda kwenye support na resistance tena
SUPPORT na RESISTANCE ni nini hasa?

Support na resistance ni zone muhimu sana ambazo zinatufanya tutambue demand na supply walipo.

SUPPORT

Support ni kama sakafu katika nyumba yako au chumba chako na hapa ndio hasa buyer huwa wanapatikana kusubiri price ifike wao waichukue na kuipeleka juu zaidi, kwahiyo hapa kwenye support ndio sehemu ambayo huwa tunabuy endapo price itakua imefika hapa na ikawa imekidhi vigezo vyote.

RESISTANCE

Hii ni kama sling board ya nyumba au chumba chako, ukisimama hapo kwenye sakafu yani kwenye support na ukiangalia juu ya paa la nyumba au chumba unaangalia kwenye resistance. Why support ni kama sakafu na resistance ni kama paa la nyuma?

Embu fikiria endapo ungekua umejenga nyumba isiyo na paa then ukasimama ndani ya nyumba na kuangalia juu, hivi macho yako yangekua na ukomo wakuangalia? Obvious hapana coz ungeangali pasipo kikomo but uwepo wa paa la nyumba linafanya ukiangalia juu macho yako yanagonga juu ya paa na kuishia hapo....na hata kwenye support endapo ungekua umejenga nyumba hewani then huku weka sakafu au ghorofa ya juu isiwekwe sakafu then uambiwe usimame unadhani nini kitatokea? Obvious utaanguka hadi ukutane na support itakayokufanya au kukuzuia usiendelee kudrop na hivi ndivyo ilivyo kwa price ikipita sehemu ambayo hamna support huwa inatembea coz sehemu isiyo na support huwa hamna force pingamizi ambayo ni demand force ambayo itazuia price isidondoke ila ikifika kwenye support itatulia maana itakua imekutana na force zuizi na ndivyo ilivyo pia kwenye resistance.

Sasa basi baada ya utangulizi huu wa awali nadhani sasa ni wakati wa kuingia kwenye kuzijua kiundani hizi zone za support na resistance vile zinavyofanya kazi na jinsi ya kuzitambua.

Soko linapokua lipo kwenye uptrend huwa haliendi moja kwa moja kama mstari mnyoofu ambao umepigwa na rula hapana huwa linakwenda na kutengeneza mikunjo flani flani kila baada ya muda na hiyo mikunjo huwa tunasema soko limefanya correction au retracement na utaijuaje retracement kwenye uptrend?

Utaijua pindi soko linapomove kwenda juu na ikafikia mahali likaanza kurudi chini kidogo then ghafla linaanza tena kuelekea juu...basi hapo huwa ndio tunasema trend ipo kwenye retracement au ipo kwenye correction.

Na pia kwenye downtrend huwa inatokea kwenye supply zone kuja chini so nayo huwa haiji kama mstari mnyoofu inakuja chini na kutengeneza correction au retracement ambapo humu kwenye downtrend tunategemea kuona wakati price inashuka basi kunakua na mikunjo inayoelekea juu kidogo then price inaendelea tena katika uelekeo wake na hapa ndio tunasema kwamba trend imeretrace au imefanya correction.

Na katika consolidation huwa inatokea wakati soko liko kwenye usawa yani haliendi juu sana wala haliendi chini sana...kama likienda juu hatua mbili basi litarudi chini hatua mbili pia so hapa ndio tunasema ipo kwenye usawa.

Ngoja tuone mifano sasa ya hizo trend kabla hatujaenda mbele zaidi


Jifunze Forex Kiswahili 

Jifunze Forex Kiswahili


Na hii nayo ndio downtrend mikunjo ndio kama unavyoiona hapo na hiyo mikunjo ndio ya correction au retracement tulisema

Sasa basi baada ya kuonesha hizo trend kwa mifano michache utaona kwenye uptrend huwa inatengeneza higher high na higher low yani wakati price inapanda juu ikianza kutengeneza correction itapinda na kutengeneza kama pembe tatu hivi kwajuu hiyo ndio tunaita higher high(HH) na pia ikishashuka hadi level flani lazima itarudi kuelekea na uptrend yake na wakati itakapo rudi itatengeneza tena mkunjo kwa chini na hiyo ndio tunaita higher low kwamaana kwamba ilikua iko higher coz inaelekea juu ila ikashuka kutengeneza correction chini yani low ndio tunasema higher low

Na kwenye downtrend nayo huwa hivyo hivyo wakati inashuka lazima ifanye correction coz haiwezi kwenda kama mstari mnyoofu na ikifanya correction kwakua yenyewe ni downtrend yani inaelekea chini basi kwenye correction tutaona inapanda kidogo na wakati inapanda itaenda kidogo then itaweka mkunjo kama wa pembe tatu kwamaana itarudi tena chini ili kuendelea na trend yake basi ule mkunjo wa juu tutauita lower high kwamaana ilikua inaelekea chini coz ni downtrend but ikapanda juu kidogo nakutengeneza mkunjo juu kidogo yani high na ndio maana tukasema lower high na pia ule mkunjo wa chini yake huwa tunauita lower low yani uelekeo ni chini na mkunjo imetokea chini pia

Na hivyo ndivyo ilivyo sasa kwenye hizo trend nlikua nataka tuzione hizo trend na hiyo mikunjo yake ambayo hiyo mikunjo ndio hasa huwa tunaitumiaga kutafutia zone za support na resistance, kivipi? Tutaona si muda kwa sasa naomba urudie kuangalia hizo trend na pia uielewe hiyo mikunjo ya higher high, higher low kwa uptrend na lower high, lower low kwa downtrend.

Kwa kawaida katika market huwa price inakwenda juu na inashuka chini na kuna wakati huwa inatulia sehemu moja na sasa basi swali limakuja je ni nini huwa kinasababisha market iwe katika mtindo huu?

Na hili ndio swali ambalo linatakiwa lijibiwe na traders wote wa forex coz kwakujibu hili swali basi litafanya ujue nini chakufanya kwenye market, yani utrade muda gani na pair gani na muda gani usitrade.

Najua jibu unalijua ila wacha na Mimi nijibu na kuongeza idea au kama haujui basi ntakua nimekusaidia katika safari yako ya forex, kumbuka forex ni yakila mmoja coz forex sio kipaji sema mtu anazaliwa nacho hapana, bali forex ni ujuzi ambao mtu anaupata kwa mafunzo endapo anapenda so kwakua uko hapa naamini unapenda na ndio maana kila nkijuacho nakiweka hapa ili wote twende sawa.

Sasa ngoja tuone jibu la swali letu hapa chini.
Katika forex huwa kuna kitu kinaitwa pair na kingine kinaitwa currency hili najua unalifahamu na kama haulifahamu basi usijali utafahamu hapa

Pair ni muunganiko wa currency mbili na mfano wa pair ni EURUSD, NZDJPY, GBPCAD na kadhalika, na pia mfano wa currency ni EUR, USD, JPY, CAD, GBP, NZD na kadhalika.

Kwahiyo pair haiwezi kukamilika bila currency mbili kuungana hili muhimu unatakiwa uelewe.

Pia katika forex huwa hatutrade currency bali tunatrade pair so hata kwenye kufanya uchambuzi yani analysis huwa tunafanya kwenye pair ili hili ni kosa kubwa and why kosa kubwa, ntakuonesha hapa.
Mara nyingi tunabuy kama trend ikiwa up na tunasell kama trend ikiwa down na ikiwa kwenye consolidation huwa tunatulia coz hatujui soko litaelekea wapi zaidi, ingawa kuna baadhi ya consolidation huwa zinatradika kwa maana zinakuaga na pips hata 10 mbaka 15 so unaweza ukawa unatrade zone tu zone yani kutoka kwenye support hadi kwenye resistance na kwenye resistance to support, tutaona hapo baadae kwa kadri tunavyoendelea na somo letu la support na resistance ambalo ndio tunaendelea nalo.

Sasa basi ili soko liende juu yani uptrend basi lazima kwenye pair kuwe na currency ambayo ni weak na nyingine strong na ile strong ndio inaipeleka price juu...mfano ukiwa na pair ya EURUSD ukaona inapanda juu inamana hapa EUR ni strong na USD ni weak so ndio maana EUR ameweza kucontrol price au movement ya pair.

Na ukiona soko linamove kwenye downtrend basi ujue hapo katika pair kuna currency moja ni dhaifu na nyingine inanguvu, mfano USDJPY ukaona inamove down hapa jua kabisa USD ni dhaifu na JPY inanguvu ndio maana hii pair inamove kuelekea juu, kuna mtu hapa namuona hajanielewangoja nirudi hapa kwanza ili tuende sawa.

Katika pair kuna currency mbili na hizo currency kuna ambayo inaanza na kuna ambayo inafuata ukihesabu kutoka kushoto kwenda kulia, kwamfano EURUSD hii ni pair ambapo EUR ndio imeanza mwanzo na USD ndio imefuata na pair zote huwa tunahesabu hivi, sasa basi ili price iende juu basi lazima huyu anaeanza awe na nguvu kumpita anaemfuata so kwa hiyo pair ili iende juu basi ni lazima EUR awe na nguvu kumpita USD na ili market ishuke chini basi lazima EUR awe dhaifu kumpita USD so inamaana kwamba USD anatakiwa awe na nguvu kumpita EUR ndio aweze kupeleka price chini, tumeelewana sasa hapa

Kwahiyo popote unapoona soko linamove kutoka juu kuja chini yani kutoka kwenye resistance kuja kwenye support basi hapo currency ya pili ndio inanguvu kuliko currency yakwanza na ukiona inamove kutoka kwenye support kwenda kwenye resistance basi hapo jua currency ya kwanza inanguvu kuliko currency ya pili, simple like tha
Kitu cha msingi ambacho watu wengi huwa hawakifanyi katika analysis zao kutenga pair katika currency zake mbili then ndio uanze kufanya analysis.

Kabla hujafanya analysis zako kwa pair Fulani hakikisha kwanza unaitenga katika mafungu mawili na hii ni kwasababu pair ni muunganiko wa currency mbili na ili soko liende juu au chini lazima currency moja iwe na nguvu na nyingine iwe dhaifu na sio pair yote ndio inauwezo wakupeleka price juu au chini, no, bali ni currency, hii iweke kwenye ubongo wako.

Sasa ukishaigawa katika mafungu mawili basi sasa ndio tunaanza kufanya analysis kwenye currency moja moja, tutaanza na yakushoto then tunakuja yakulia....ngoja tuone mfano hapa venye tunatakiwa tufanye.

Kwamfano unataka utrade pair ya USDCHF basi tutaigawa katika mafungu mawili ambayo ni USD na CHF then hatua inayofuata tutaanza kuanalyz USD, sasa utaanalys vipi USD basi hapa ndipo tunapochukua pair zote zenye USD tunazichambua tuone je USD katika pair hizo zingine ameweza kuipeleka trend juu au hakufanikiwa ila amefanikiwa kuipeleka chini, basi kama atakua kaipeleka juu kwa pair zake zote na tukaona ananguvu basi tunanote pembeni then tunakuja kwenye currency ya pili ambayo ni CHF nae tutamfanyia analysis kwenye pair zake zote ambazo yeye yumo tutaangalia kama ananguvu au hana nguvu au yupo katikati yani hana nguvu sana wala hayuko dhaifu sana na ili ujue kwamba yupo katikati basi utakuta pair zake nyingi ulizozichambua price ipo kwenye consolidation, so nayo utainote kwenye daftari lako la uchambuzi.

Baada ya hapo sasa utakuja kuangalia zile pair ambazo USD na CHF wanachangia currency, kwamfano USDJPY na CHFJPY au EURCHF na EURUSD na zingine nyingi, kwenye hizo pair wewe utaangalia hivi.

Kwenye USDJPY utaangalia je USD ananguvu na amefanikiwa kuipeleka price juu, kama ndio basi utajua USD ananguvu kuliko JPY unaweka jibu pembeni, then unakuja kwenye CHFJPY utaangalia je CHF ananguvu na amefanikiwa kuipeleka price juu Au hapana, kama jibu hapana basi utajua hapa JPY alikua na nguvu kuliko CHF kwahiyo utaandika jibu lako.

Na baada ya kumalizia hapo basi utasema hivi kama USD ananguvu kuliko JPY na JPY ananguvu kuliko CHF je kati ya USD na CHF nani atakua na nguvu kuliko mwenzie, umepatia jibu ni USD so katika pair yetu ya USDCHF basi tutaenda kubuy coz price itakwenda juu na hapa tunasema USD ameicontrol price.

Na kama ungekuta CHF nae ananguvu kuliko JPY basi basi hapa inabidi uache kwanza au ntakwambia ufanye nini hapa chini ila kwa Leo ngoja tuishie hapa kwanza and fanyia mazoezi.

kuna wakati unaweza ukawa unafanya analysis zako za pair ya USDCHF ndio ilikua reference pair yetu hii...so unaweza ukafuata process zakuichambua hii pair na ukatumia reference mbali mbali na ukagundua pair zote zinanguvu na tulitumia reference ya USDJPY na CHFJPY ambapo kwenye USDJPY ukakuta USD ananguvu kuliko JPY na kwenye CHFJPY ukakuta CHF ananguvu kuliko JPY pia, hapa nkasema unatakiwa uachane na USDCHF coz unakua hujui nani anaicontrol price labda kama unascalp unaweza ukatrade but kumbuka hizi currency za USD na CHF wanashare currency nyingi pia kwenye pair zao, na nlitoa nyingine ya EURCHF na EURUSD so kama kule ulipata jibu lenye mkanganyiko basi unarudi na kwenye hizo pair nazo unaanza kuangalia kati ya USD na CHF nani atakua na nguvu kuliko mwenzie.

Kwenye EURUSD ukishaichambua na ukagundua EUR ananguvu kuliko USD yani ukiona price inapanda juu basi unanote pembeni, then unakuja kwenye EURCHF naukikuta kwenye hii pair CHF ndio ananguvu kuliko EUR yani price inashuka chini yani tunasell hapa napo unanote jibu lako pembeni, then unarudi kwenye pair yako ya USDCHF lazima utakuta inadrop coz CHF atakua na nguvu kuliko USD na hii imetokana na uwezo wake wa yeye kuwa mkubwa kuliko EUR na wakati huo EUR ananguvu kuliko USD.

Pia ukienda kwenye pair kama EURJPY utakuta nayo inapanda juu unajua why, coz USD alikua na nguvu kuliko JPY na wakati huo EUR ananguvu kuliko USD so obvious EURJPY itakua inakwenda juu tena kwa pips nyingi tu.

Pia CHFJPY itakua inakwenda juu kwa kasi maana CHF atakua na nguvu hapo kama tulivoona kwenye analysis zetu hapo juu.

Na hii hali ndio huwa tunasema correlation of pair so ukishajua hii huna haja yakuomba zile chart ambazo wameandika pair nyingi za kuonesha correlation na uanze kuzikariri no, just do your analysis and utabaini kitu na kumbuka kwa kutumia njia hii unaweza ukafanya analysis ya pair moja na ikakupa muelekeo wa pair nyingine nyingi tu...so nenda kajaribu sasa
Kwa kawaida katika forex huwa tunacurrency 8 ambazo hizi ndio major currency, ambazo ni EUR, USD, GBP, JPY, CAD, AUD, NZD na CHF.

Hizo ndio currency ambazo zipo kwenye forex sasa.....na hizo currency tukiziunganisha ili tupate pair tunapata pair 28 na hizi ndio hasa zipo kwenye forex na kila mtu anazijua ila kwa mfano tu ni hizi hapa.

EURUSD
EURJPY
EURGBP
EARNZD
EURCAD
EURAUD
EURCHF

USDJPY
USDCAD
USDCHF

GBPUSD
GBPCAD
GBPAUD
GBPJPY
GBPNZD
GBPCHF

NZDUSD
NZDCAD
NZDAUD
NZDCHF
NZDJPY

CADAUD
CADJPY
CADCHF

AUDCAD
AUDUSD
AUDCHF

Hizo ni mifano tu ya pair so zingine utamalizia hapo ila mi nimetoa mifano tu hapo so hizo ndio pair kimsingi zinatakiwa ziwe 28 ila mi nimeandika kwa uchache tu ili kukufanya uzielewe.

Sasa tunapofanya analysis hapo kwamfano tunatrade pair ya EURUSD, tunachotakiwa kufanya ni kuitenga katika currency mbili ambazo zimeunda hiyo pair ambazo ni EUR na USD...na baada ya hapo sasa unaanza kuzichambua hizo pair zote ambazo EUR yupo unaangalia trend yake na uwezo wake na hizo pair zingine kama uko juu au chini ili ikufanye uelewe kama EUR anaonekana ananguvu au hana nguvu, kumbuka currency huwezi ukaifanyia analysis kwakuchora ila tunafanyia analysis pair maana kwenye platform za forex hakuna mahali utakuta USD iko pekeake wala ukakuta EUR iko pekeake ila utakuta muunganiko wa currency mbili ambazo zinafanya piar kwamfano hiyo EURUSD, so hilo unatakiwa ulijue kwanza.

So hapo ukishaangalia hizo pair zote za EUR najua utagundua kama EUR ni bearish kwakua pair zote alizopo anashindwa kupeleka price juu au bullish coz kwenye pair zote alizoko amefanikiwa kupeleka price juu.

Ukishamaliza hapo inabidi urudi kwa upande wa USD nae unamfanyia hivyo hivyo ili uelewe yuko bullish au bearish kwenye pair zake ambazo yupo na ukishamaliza hapo inabidi sasa ujiridhishe maana unaweza ukakuta majibu ambayo yanafanana, kwamfano ukikuta EUR anaonekana kwenye pair zake zote ni bullish na pia ukakuta USD nayo ni bullish hapo utashindwa kujua ukafanyeje kwenye EURUSD, so inabidi uchuchue reference pair kwamfano EURJPY na USDJPY angalia hapo kwenye currency ya JPY EUR alikua bullish au bearish ukiona ni bullish basi rudi kwa USDJPY nae ukiona ni bullish basi hiyo pair ya EURUSD inauwezekano wa kuwa kwenye consolidation coz USD na EUR wote wananguvu sawa hapo kaa pembeni ya market acha tamaa.



Na ukiona mmoja kati yao ni bullish na mwingine ni bearish basi hapo kuna ela ...kwamfano ukakuta EUR ameweza kuwa bullish kwa JPY lakini USD amekuwa bearish kwa JPY basi hapo moja kwa moja tutabuy maana EUR ananguvu kuliko dollar coz EUR ameweza kuwa bullish kwa JPY na USD ameshindwa so hatoweza kupambana na EUR kama ameshindwa kwa JPY

Kama tulivyosema support ni mfano wa sakafu na resistance ni mfano wa Dari kwenye nyumba, sakafu inakusaidia uweze kusimama usiporomoke na Dari inakusaidia usiangalie mbali zaidi....

Ndivyo ilivyo kwenye market price ikifika kwenye support huwa inaishia hapo na kugeuza kurudi tena juu na ikifika kwenye resistance inaishia hapo na kugeuza kurudi chini ila hii inategemea na nguvu ya currency husika, kwamfano ukichukua pair ya EURUSD kutrade ukiona inatoka chini na kwenda juu na ikafika mahali ikageuza na kurudi chini basi hapo ilipogeuzia tunasema ni kwenye zone ya wanunuzi yani ndipo ilipo resistance na ikiwa inashuka chini ikafika mahali ikageuza basi hapo ndipo kwenye zone ya buyer na tunaita support so ndipo tutakapoweka mistari yetu juu ya resistance na chini ya support.

Ngoja tuone hapa chini venye tunachora hiyo mistari ya support na resistance sasa.

Hii mistari ya support na resistance huwa inakuaga na sheria zake rahisi sana pindi tunapozichora.

1 kwanza ni lazima ugundue mikunjo ya juu na chini, mikunjo ya juu ni resistance na mikunjo ya chini ni support.

2 weka mstari kwenye hiyo mikunjo ya juu ambayo tutaita resistance na weka mstari kwenye mikunjo ya chini ni support.

3 hakikisha mstari wa juu unagusa kwenye candlestick zaidi ya moja, yani kuanzia mbili na kuendelea na hata mstari wa chini pia ni lazima uguse kwenye candlestick zaidi ya moja kuanzia mbili na kuendelea.

4 kama mstari wa juu utagusa candle moja na wa chini pia basi hapo tutasema resistance na support haziko valid.
Ukishachora hiyo mistari ya support na resistance na ukahakikisha iko valid basi hapo ndio setup yako itakua imekamilika now unasubiri entry point ifike ili uingie sokoni.

Sasa basi katika support na resistance entry point zetu huwa tunasubiri price iende juu ikagonge kwenye hiyo line ya resistance then igeuze ianze kurudi chini kwa kuuza na kwenye support pia hivyo hivyo tu nasubiri price igonge line ya chini na ianze kurudi juu ndipo hapo tunakaa tayari kwa kununua.

Kitu muhimu ambacho unatakiwa ufanye wakati unataka kuingia sokoni kwakutumia support na resistance ni kwamba, wakati price ipo kwenye support ikagonga na kugeuza kurudi juu, unahesabu candle ya kwanza na yapili then ya tatu ikianza unaingia hapo ndio uhakika kwamba kweli price inapanda juu, na hata kwenye resistance pia unatakiwa usubiri hivyo hivyo yani ya kwanza na yapili ikianza ya tatu tu unaingia sokoni...ila kuna wakati mwingine huwa kunakuaga na candle kubwa sana ambayo inanguvu kwenye upande wa support ikiisha hiyo candle basi hainaaja ya kusubiri hadi zifike tatu coz kama ikitokea kwenye support inamaanisha kunastrong bullish movement so ni kubuy tu baada ya hiyo candle kuisha hadi kwenye resistance na ikitokea kwenye resistance basi ni kusell hadi kwa support.
Pia ukishaingia sokoni basi ni lazima ujihami maana forex sio science kuna wakati unaweza ukabuy katika sehemu sahihi ila ghafla soko likageuka na kurudi nyuma na kuendelea na safari yake ya awali, hii huwa inatokea sana na ndio maana huwa tunashauriwa kutumia stop los ambayo hii itatufanya tuwe salama zaidi hata kama soko likirudi nyuma litaishia kwenye SL yetu na kutuacha na ela zetu za mtaji bado zipo.

So katika support na resistance huwa tunaweka SL yani stop los nyuma ya mstari wa support na resistance, kwamfano kwenye support SL yake huwa tunaweka chini zaidi ya mstari wenyewe wa support na kwenye resistance huwa tunaweka juu zaidi ya mstari wenyewe wa resistance
Baada ya kuingia sokoni sasa ni lazima ujue wapi utachukulia faida yako, na Mara nyingi huwa inasisitizwa usiingie sokoni bila kujua wapi utaenda kuchukulia faida yako, maana hii itakufanya ushindwe kuelewa wapi utaweka TP yako yani take profit yako....na ukishindwa kuelewa wapi utachukua faida basi unaweza ukashangaa unachukua kijifaida hata chmwingine. natania asee...

Ila ukweli ni kwamba trader ni lazima ajue entry point yake na SL yake wapi ataweka pia ni lazima ajue TP yake wapi anaenda kuiweka na hii itamrahisishia hata yeye kucalculate pips ambazo atakwenda kuchukua kwa kila trade atakayoingia na pia itamrahisishia ajue anatakiwa aingie trade ngapi kwa siku ili afikie idadi ya pips anazo zihitaji.

Na kwenye support na resistance TP huwa tunaweka chini ya resistance na juu ya support, kwa maana kwamba kwenye support baada ya mstari wa support juu yake tunaweka TP na kwenye resistance baada ya mstari wa resistance basi chini yake hapo tuna weka TP... Na hii ndio tunaita zone to zone, yani unatoka ukanda mmoja na unaenda kuchukulia faida ukanda mwingine.
wakati resistance inabadilika kuwa support na support kuwa resistance.

Hii inatokea kipindi ambacho currency moja kwenye pair inakua na nguvu sana kuliko nyingine, so inaelekea ishindwe kuzuia isiingiliwe kwenye maeneo yake ya kujidai...ni kama team mbili za mpira moja ikiwa na uwezo sana na nyingine ikiwa haina uwezo sana mwenye uwezo sana ni rahisi kufika golini kwa asiye na uwezo na kufunga magori kiurahisi basi ndivyo ilivyo kwenye hizi pair kuna wakati currency shindani huwa zinakua zinauwiano usio sawa yani moja inakua na nguvu sana kuliko nyingine na hii hupelekea yenye nguvu kupita kwenye zone ya currency dhaifu bila kipingamizi na hapa ndipo breakout hutokea na breakout ikitokea kwenye support basi support inabadilika kuwa resistance na ikitokea kwenye resistance basi inabadilika kuwa support..

Kiurahisi chukulia mfano mtu akitoboa paa na akaenda hadi juu ya bati la nyumba akatua pale, bati ndio litakua support yake maana limemfanya asimame pale wakati mwanzo kabla hajatoboa bati lilikua ni resistance yake maana ndipo alipokua anaangalia wakati aliposimama kwenye sakafu...na ndivyo ilivyo hata kwenye price inapovunja resistance na kuingia upande wa pili huwa tunaichukulia ndio support maana imefanya price ianzia hapo na kinyume chake kwenye support nayo ikivunjwa ndio inakua resistance.

Jifunze Forex: Jinsi ya kutambua supply and demand zones

Supply na demand hizi ni kanda au zone ambazo zinapatikana katika chart ya forex, hizi zone huwa ndio zinazozingatiwa sana na matrader wote wa aina tatu, ambao ni seller buyer na institutions, ambao seller na buyer kwa neno moja tunawaita retailer yani wafanya biashara wadogo wadogo na hao walio kwenye taasisi mbali mbali ambazo zinajihusisha katika biashara hii ndio hao tunawaida wafanya biashara wakubwa na ndio hasa wenye nguvu katika soko hili la forex.

N.B:
Kama ndio unaanza kujifunza biashara ya Forex, unashauriwa kujiunga kwa kutengeneza account kwa broker anayekubalika zaidi Afrika Mashariki:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Ukishatengeneza account yako ya Forex, usisahau ku verify email uliyotumia kutengeneza account pamoja na namba yako ya simu

Tuendelee na somo letu la leo:


Jifunze Forex Kiswahili

Kwa hiyo kwakua wafanya biashara wote huwa wanaheshimu zones(ukanda) basi hii inapelekea uhakika zaidi pindi unapotrade kwakutumia zone, maana ndipo jicho la kila mfanya biashara lilipo duniani kote.

Kama nilivyosema hapo juu kwamba support na resistance huwa hazina utofauti sana na supply na demand kwa kuziangalia kwa macho ila kiufundi huwa utofauti upo tena ni wamuhimu sana na ili utrade hii strategy ni lazima uzingatie utofauti huo, maana usipozingatia huo utofauti utakua umetoka kwenye maana halisi ya supply na demand na unaingia kwenye support na resistance

Utofauti uliopo kati ya demand na supply ukilinganisha na support na resistance ni kwamba support na resistance huwa yenyewe inasisitiza sana kwenye idadi ya candlestick ambazo zinagusa kwenye hizo mistari ya support na resistance huwa kadri inavyogusa Mara nyingi na kushindwa kuvuka upande wa pili wa huo mstari basi ndio uimara wa huo mstari wa support au resistance unavyoongezeka.

Ila kwenye supply na demand hii kitu imekataliwa kabisa na kuna sababu nyingi ambazo zimetolewa zinazofanya hiyo point ikataliwe, huku wanasema kwamba ili zone ya demand au supply iwe imara basi ni lazima iguswe na candle moja mbaka tatu zikizidi hapo basi hiyo si ukanda imara kwahiyo achana nao, sasa wakatoa sababu za kwanini haiwi zone imara ikiguswa na candle ya zaidi ya mbili au tatu...tutaziona hapo chini

Kumbuka haya masomo yote nnayoyatoa hapa ni elimu so ni muhimu na wewe ukapita pita kwenye vitabu ili upate zaidi...nnavyosema elimu namaanisha ni kitu nlichobaki nacho kichwani baada ya kupita pita kwenye vitabu vingi so nenda kaongeze maarifa kwenye vitabu baada ya hapa ili upate mengi ambayo hayapo kwenye elimu yangu ndogo, nikiwa na maana kwamba nimeyasahau.

Sababu ya kwanza ya kwanini supply na demand strategy imekataa kwamba idadi ya miguso mingi kwenye ukanda si uimara wa ukanda huo.

Kwanza tupate picha then tutaenda kwenye sababu moja kwa moja, kama tulivyowahi kusema huko juu kwamba soko huwa linamove up and down na wakati mwingine linakua limekaa kwenye usawa na likiwa linapanda juu huwa tunasema demand wananguvu kuliko supply na likiwa linashuka chini huwa tunasema supply wananguvu kuliko demand na likiwa katika usawa hapa tunasema supply na demand wote wako na nguvu sawa.

Kwahiyo ili soko litembee kwenda juu au kurudi chini ni lazima kuwe na kuzidiana kwa nguvu kati ya demand na supply na endapo wakitoshana nguvu basi soko huwa linakua linafanya haki, yani watakao nunua watanunua sawa na watakao uza.

Kwahiyo kutokana na sababu hii ya kinachopelekea soko litembee juu chini au chini juu, ndio sababu ya kwanza inayopelekea supply na demand kukataa ile dhana ya kwamba eti uimara wa zone unapimwa na idadi ya miguso mingi ya candlestick.

Kwa sababu endapo ukanda utaguswa na candle Mara nyingi hii inamaanisha supply na demand nguvu zao hazina utofauti sana au ndio zinaelekea kwenye uwiano sawa, ila endapo itaguswa na candle moja au mbili then reaction ya kwenda juu au chini ikawa imetokea basi hapo tunasema demand na supply hawako katika usawa na hapo lazima kutakua na pips nyingi sana.

Pia kama hujaelewa hapo njoo kwenye mfano huu mwingine wa kawaida sana tu.

Kwamfano chukua kitenesi kidundishe kwenye sakafu then kiangalie vile kitakwenda juu na kurudi kugonga sakafu then kitakwenda baadae kitapungua kasi na baadae zaidi kitaishiwa nguvu na kitaanza kuroll na hatimae kitatulia sehemu moja...basi hata kwenye zone candlestick zitakwenda zitagusa na kugusa tena na tena na baadae zitatulia hapo kwa muda mwingi bila kushuka sana wala kwenda upande wa pili, so kadri zone inavyoguswa Mara nyingi ndio udhaifu wake unaongezeka.....kwenye mpira ukiruhusu timu pinzani iwe inakuja kwenye himaya yako Mara kwa Mara lazima utafanya makosa tu na utaachia na utafungwa goal so miguso ikitokea mingi itafikia mahali usawa utaonekana na usawa ukitokea basi ukatili utafuata(initiative), hii ndio tofauti ya hao jamaa na ndio maana kuna watu wanasemaga support na resistance haina jipya nlimskiaga mtu aliwahi sema hivi pia na marumbano yalikua mengi mno ingawa sijajua kama na yeye alitumia point hii au alikua na maana nyingine.

Kwa kawaida head and shoulder pattern huwa inakua na mabega mawili la upande wa kushoto na upande wa kulia na katikati ya mabega hayo huwa kuna head.

Kimsingi ili head and shoulder iwe valid kwa kiasi kikubwa ni lazima bega la upande wa kushoto liwe kubwa kuliko la upande wa kulia, ndio ikiwa hivi hapa tunakua na uhakika zaidi kuliko kinyume chake....najua utauliza kwanini sasa iwe hivi?, inakua hivi kwasababu zifuatazo.

Kwa kawaida head and shoulder ili itokee ni lazima kuwa na strong momentum ama kwenye support au resistance na hiyo strong momentum inapelekea support au resistance ivunjwe na price itaenda juu bila kufanya pullback baada ya kuvunja support au resistance itaenda juu kwa umbali flani then itakutana na demand au supply wengi so hao waliofanya hiyo initiative wataingiwa na wasiwasi wataanza kuchukua partial profit na kitendo cha kufanya hivi basi itapelekea retracement kutokea na hii retracement itakua kipimo cha kwanza kwa hao waliofanya initiative wataitumia hii kupima nguvu zao, sasa wataitumiaje kupima nguvu zao, twende tuone huu mfano hapa chini.

Majeshi ya nchi Fulani yanapotaka kuvamia nchi nyingine kwa kawaida huwa mashambulizi yanaanzia kwenye mpaka, so wataweka ngome mpakani then wataanzia hapo kuingia ndani ya hiyo nchi kwa mashambulio ya taratibu, ila pia kuna ile unaingia kwa nguvu zote ili kuwaogopesha zaidi then ukiona nao wamejipanga zaidi unarudi nyuma kuweka ngome kwenye mipaka yao ili watakapokuja wewe uanze kuwashambulia hapo, basi ndivyo ilivyo baada ya kuvunja let say support hawakusubiri pullback wakaingia wakakuta nguvu zao nyingi ila hazina effect kubwa so wanaamua kurudi nyuma kwenye zone wanaweka pending order nyingi hapo na hao wa upande wa pili wakifika hapo wanakua hawana uwezo wa kupita upande wa pili na hapo demand wataichukua hiyo nafasi na kuipeleka price juu kwa kasi coz wataona hao jamaa kumbe ni dhaifu maana wameweza kuwaingilia kwenye ukanda wao kwa kasi ila wao wameshindwa kutumia nguvu nyingi kurudisha hayo mashambulizi na kiwarudisha hao demand kwenye zone yao ila wanaishia kwenye mpaka ambao ndio support na hii ndio itawafanya jamaa waongeze nguvu nyingi na kuipeleka price juu zaidi na hapa ndio tunatengeneza head wakati huo bega la kushoto ndio limetengenezwa kwa ile initiative na retracement iliyofanyika so ikishaenda juu itafika kwenye zone ambayo hao jamaa nao wako wengi na pia majeshi ya upande wa pili yataingiwa na hofu so wataanza kupunguza kasi na hapo demand wataanza kuchukua profit zao na kitendo hiko kitapelekea supply waongeze nguvu na kurudisha price chini tena na price ikifika kwenye mpaka yani support itakutana na jamaa bado wapo wengi sana hapo wanasubiri mguso wa pili uje waende nao juu lakini kumbuka wakati initiative inatokea kutengeneza bega la kushoto supply walikua hawakujipanga so baada ya kuona hiyo initiative basi nao wataweka pending order zao mwisho wa hilo bega kwahiyo baada ya mguso wa pili wa kukamilisha head kwenye support, demand watachukua price kwenda juu lakini wakati huo supply wamesogeza ngome karibu yani pale ambapo bega la kushoto limeishia ili wakirudi tena hao demand wasiende mbali zaidi so demand wakifika eneo hilo wanakutana na supply wengi sana na hapo watashindwa kwenda mbali zaidi na price itarudishwa chini tena hapo bega la kulia linakua limekamilika so head and shoulder inakua imekamilika.

Je head and shoulder ni lazima ishuke chini endapo itakua kwenye support? Jibu ni hapana, coz forex si science ila kinachopeleka price up and down ni hali ya utofauti wa uwiano kati ya demand na supply na alama inayotuonesha kwamba supply ana nguvu kuliko demand au kinyume chake basi ni uwezo wa kuipeleka price kwenye zone ya mwenzie bila vikwazo au kuonesha vikwazo wakati unapotaka kushamuliwa kwenye ngome yako.

So kwenye head and shoulder shambulio la bega la kwanza ni lakushtukiza na baadae ikapelekea head na baada ya hapo hao watu wa upande wa pili wataona ela zao nyingi zinapotea au currency yao inakua weak so ili kuipandisha ni lazima waongeze nguvu wauze sana na hapo watakamilisha kichwa na wakifika kwenye zone tena

hawaendi kwa papara watajipanga upya ili kujua nguvu iliyopo upande wa pili kama bado ni ile ile au inapungua na ili wagundue hilo watasogeza zone usawa wa bega la kwanza na hao demand wakishindwa kupita hapo basi watajua kweli wamelegea so wataongeza nguvu zaidi na hatimae kuishuka price chini kwa kuingia kwenye zone yao na hii huwa inatokea sana kulingana na session husika na currency zilizounda pair husika zinauhusiano gani na hiyo session..

Na nlisema patten ni lazima zianze kwenye zone au ziishie kwenye zone, sasa hii pattern ya head and shoulder huwa inatokea kwenye zone na inaishia kwenye zone ila mabega yake huwa yanatengeneza minor zone, but kichwa huwa kinakua kwenye major zone na huku chini tunakoweka neckline huwa ni kwenye major zone pia


Jifunze Forex Kiswahili Huu ndio mfano wa head and shoulder
Ukiangalia hiyo picha utagundua imetokea kwenye support na maelezo yote nliyoyatoa hapo juu yako hapo kwenye picha, ila hapa nataka nielezee kwanza kwa kuunganisha na concept ya supply na demand.

Angalia hapo sasa kwenye neckline utaona hiyo zone imeguswa zaidi ya Mara moja na kama tunavyosema zone kadri inavyoguswa Mara nyingi ndivyo inavyopoteza ubora so baada ya kupoteza ubora nadhani umeona kilichofuta....hii ni confluence ya kwanza.

Pia confluence ya pili ni kwamba ukiangalia upande wa kulia wa hiyo head na bega hilo la kulia utagundua price imeform flat pattern ambayo hii inaonesha kwamba trend imeshabadilika si up tena ila ni down.

Why down ni kutokana na formation higher high ambayo ndio hiyo head then baada ya hapo ikashuka kuform lower high na lower low.


So hapo ndio tunapata confluence ya pili kwamba kuna uwezekano mkubwa wa hiyo price kushuka chini but hii sio sheria ila ni lazima tujue balance ya supply na demand ndio hasa inayosababisha market I move
Technical analysis inatusaidia kutambua mipaka iliyopo kati ya supply na demand ila si kwamba ndio hasa inapeleka soko juu na chini, so si kila mchoro unaouchora na ukausoma ukataka ufanye kazi kama vile ulivyosoma hapo utakua unaifanya forex iwe science wakati haiko hivyo
Nlisema hizi pattern kuna wakati huwa zinaathiriwa sana na session flani flani hasa hizi za triangle ila hizi za divergence Mara nyingi huwa zinatokea wakati soko linapokua haliko kwenye trend yani soko linapofanya fair treatment(haki), so huwa inapoonekana tu lazima ifuate uelekeo wake kwa asilimia kubwa ingawa sio sana, unaweza ukachunguza hii


Soko linapokua kwenye pattern hasa za triangle watu huwa wanafananishaga na mnada,  ndio mnada...kwamba kwenye mnada huwa kunakuaga na mtajo wa bei kutoka chini kwenda juu yani bei inapanda kuzidiana so mwenye ela nyingi anampiku mwenzie so kuna wale ambao huwa wanasubiri hadi bei inapogota sehemu Fulani na ikawa hakuna yeyote ambae anauwezo wa kuongeza juu so hapo ndio anagundua kwamba wameshindwa hawana uwezo tena wa kifedha so yeye ni muda wake wa kuongeza ela kuchukua hiyo bidhaa....Basi ndivyo ilivyo kwa forex tunapokua katika pattern let say ya triangle labda katika pair ya EURUSD katika session ya Asia na hiyo pattern ikadumu hadi asubuhi muda wa London basi hapo kuna uwezekano mkubwa mabadiliko yakatokea na mabadiliko hayo yatambeba zaidi EUR kwa maana hiyo session ya London ndio moja ya currency ambazo zinakipaombele sana pamoja na GBP....ila ikatokea kuanzia asubuhi London imefunguliwa hadi mida ya kukaribia New York session hakuna mabadiliko yoyote kwenye ile pattern basi hapo lazima dollar atakua na uwezo mkubwa wa kufanya initiative coz wataona jamaa wameishiwa nguvu so wao wakiingiza nguvu mpya basi lazima waendeshe price iwe upande wao, but kama nao watashindwa basi choppy itaendelea kuendelea so ndio maana nkasema kama mnada coz kuna mtegeano wa nyakati kabla ya kufanya maamuzi.

Kuna kitu ambacho pia napenda niseme kidogo, kwamba kuna watu wanakawaida ya kubashiri reversal mahali itakapoenda kufanyika kwakuangalia mikunjo so wengine wanadiriki hata kuweka pending order wakiamini price ikifika hapo ni lazima itageuka tu...utakufa kama unafanya hivi coz forex huwa tunatrade tunachokiona so ukianza kubashiri kwamba price ikifika sehemu Fulani lazima igeuke eti kisa kuna resistance au support kongwe acha, na utakua unakosa fulsa kila siku maana utakaa sana kusubiri na price inaweza isifike hapo so unabaki kushangaa tu.

Wataalamu wanasema ni ngumu kutambua reversal hadi itokee na hata big boys wenyewe hawana uwezo wa kutambua reversal sema wao wananguvu kwenye order so big boy mmoja anaweza akaweka order ya matrader wengi sana na akayumbisha soko mahali anapotaka liende yeye and si kweli kwamba wanaweka pending order kwenye zile zone za zamani let say kwenye zone ambayo ni ya miezi kadhaa ilitokea nyuma, hii ni biashara and watu wa nataka wapate ela kila siku so inaingiaje akilini mtu akaweke pending order kwenye zone itakayofikiwa na price ndani ya mwezi au miezi obvious haiwezekani.

So point muhimu ni kwamba usijiaminishe kubashiri reversal ya price kwenye ukanda wa zamani maana si sahihi ila huwa tunaingia au kubashiri kwenye zone ambayo imefikiwa na hapo ndipo ambapo jicho la matrader wengi duniani linapokua na watu sasa wanaanza kuweka order zao hapo na watakao shinda kuwa na order nyingi basi wanakua wameshinda kuipeleka price kwenye upande wanaoutaka wao.

Hii ni muhimu sana kaa nayo kichwani....

Jinsi ya kutambua hizo zone
  1. Demand na supply huwa sheria yake namba moja tunaangalia uwezo wa price kugonga na kutoka kwenye hiyo zone, kama tulivyosema awali ili zone ya demand au supply iwe valid basi ni lazima iguswe na candle zisizozidi tatu, maana hii ni zone so tunategemea kupata order nyingi kwahiyo wingi wa order utapelekea price isikae sana kwenye hilo eneo na endapo itakaa sana basi hiyo zone ni dhaifu coz inaonekana nguvu ya order zilizowekwa na seller na buyer haina utofauti mkubwa that's why price haimove katika ubora.
  2. Hakikisha haubashiri zone kwenye eneo ambalo unaamini itaenda kutokea kisa tu hilo eneo ilishawahi tokea zone siku za nyuma, ndio labda unaweza ukajiambia kwamba hapo mahali huwa kuna pending order but kumbuka pending order sio order mbaka iwe order so haina madhara kwenye movement ya price, kwahiyo kuna mawili price ifike hapo ipiyilize au price ifike hapo irudi ilikotoka na au price ifike hapo ikae kwenye hali ya uwiano.
  3. Ukanda mzuri ni ule ambao unatokea mahali ambapo kuna nafasi kubwa nyeupe, yani price haijafika hilo eneo kwa muda mwingi sana, kwasababu lazima itakua ni juu sana au itakua ni chini sana na hakuna trader ambae hapendi kubuy low na kusell high so zone ikitokea maeneo hayo huwa tunasema imetokea mahali ambapo mauzo yalifanyika mengi mno au manunuzi yamefanyika mengi mno kwahiyo reversal itatokea, ila usisahau forex sio science so hii si sheria hadi ikamilike yani hadi itokee.
  4. Hakikisha ukanda wako umeendana sawa na trend ya kwenye D1 hasa kama wewe ni intra day trader, hii itakufanya uwe na uhakika na kuhold kwa siku nzima maana uelekeo wa soko upo sawa na ulipoweka order yako siku hiyo.
  5. Hakikisha hauchukui zone ambayo imetokea katikati mwa price, coz hizi huwa zinakuaga ni trap za market marker, na nnaposema katikati namaanisha kabla trend haijaonesha kubadilika we ukaingia kwenye retracement hapo lazima ufe, kwasababu big boys huwa wanalichukua soko toka mwanzo mwa trend then wanapanda nalo au wanashuka nalo katika sheria zile zile za 3 impulse and 2 correction so watakwenda nalo then watafika mahali watachukua faida zao hapo utaona kama trend ni up basi soko linashuka kidogo na hapa kuna watu wanavutiwa wataingia hasa wale wa like yes yes soko linashuka hili unatia order yako wataacha tuingie kwawingi then wanarudi tena kwenda kukamilisha trend hapo ndio unaanza kulia, kwahiyo usifanye hivo.

Jinsi ya kuchora hizo kanda, na nilazima kabla ya kujua kuchora tujue hizo zones au kanda huwa zinakua zipo katika mafungu mafungu, kwahiyo ukiiona zone ni lazima uelewe hii ni zone ya aina gani.

Ngoja tuongee kuhusu hizi zone zinazosababishwa na big boys pindi wanapochukua faida na zile zinazosababiswa na big boys pindi wanapoweka order.

Kuna wakati unaweza ukafungua Mt4 yako ukakuta trend ni up ila ikawa inaenda juu then inashuka kwa pips kadhaa halafu inarudi tena kuendelea na trend na wakati inashuka huwa inatengeneza zone basi hii ndio huwa tunaita zones ambazo zimesababishwa na hawa jamaa big boys kuchukua faida zao.

Pia kuna zile zone ambazo ukifungua Mt4 yako utazikuta zinaanzia juu kwenye supply au chini kwenye demand na zinakwenda moja kwa moja katika uelekeo wa trend huku ikitengeneza HH,HL na LH,LL ambazo hazifiki kwenye mahali ambapo zone ipo, hii ndio inaitwa zone ambayo imesababishwa na big boys kuweka order na kinachofanya price isifike kwenye mahali ambapo hizi order zipo ni kwamba hawa jamaa big boys huwa hawaruhusu kitendo hiki kitokee coz wanahofia endapo wataruhusu price ifike kwenye usawa wa order zao basi wananweza wakawavutia wawekezaji wengine wakadhani kwamba hii zone sasa imekwisha muda wake so ni muda wa kuweka order nyingi ambazo zikifanikiwa kuwa nyingi kuliko zilizokuwa kwenye hiyo zone basi price itakwenda kinyume na wao na kupelekea wao kupata hasara.

So hii ni muhimu ambayo ni lazima tuifahamu kwamba zone inayosababishwa na big boys wakati wanachukua faida huwa inakwenda na kurudi mahali kwa awali then inavunja hiyo zone na kwenda juu zaidi kama trend ilikua up au kushuka chini zaidi kama trend ilikua down.

Ila zone inayosababishwa na uwepo wa order nyingi za big boys huwa price ikienda chini kwa downtrend itatengeneza hizo swing za LH, LL ambazo haziwezi kufikia mahali ambapo order iliwekwa, kwanini iko hivi? Hii ni kuonesha kwamba zone bado imara.


Jifunze Forex Kiswahili

Ukiangalia hiyo picha hapo juu trend ni down na Mimi nimejaribu kuonesha kwenye upande wa zone za supply tu ila ukiangalia kwa umakini kwa chini ya hizo zone utaona vijizone vidogo vya demand pia, so navo ni muhimu ukiwa unafanya analysis uvichoree, ila hiyo picha hapo inaonesha upande wa supply na kwa jina moja unaweza ukaiita drop base drop, kwamaana inakua inashuka then inatengeneza consolidation kidogo then inashuka tena, so ndio maana ikaitwa drop base drop...coz inaanza kushuka inatengeneza base ambayo ndio consolidation halafu inakuja kushuka tena...tutaiongelea baadae hii drop base drop, rally base rally na drop base rally pamoja na rally base drop.


Jifunze Forex Kiswahili

Hii ni ile aina ya zone ambayo inatokea baada ya big boys kuchukua faida, iangalie vizuri hapo

Ukirejea hapo nyuma nliwahi kusema uimara wa zone haupimwi na ukongwe wake ispokua zone inatokea pale tu ambako kuna uwingi wa order, ila kuna wakati ukijaribu kuangalia unaweza ukaona zone ambayo ilitokea mwezi uliopita katika D1 ukaona na leo imefikiwa tena na price na inafanya reversal hapo, hapa wengi watapingana na hiyo kauli kwamba zone haipimwi kwa ukongwe wake....ila hiyo kauli iko sahihi ispokua price ikitoka kwenye zone wanasema inaweza ikarudi baada ya muda flani na hii ni kulingana na timeframe ambayo wewe unatumia, kwamfano kwenye 1H timeframe price ikitoka kwenye zone na ikarudi baada ya 24hours basi hii zone tunasema bado iko valid ila ikichelewa kurudi basi hii zone tunasema haiko valid.

Pia kwenye D1 timeframe price ikitoka kwenye zone ili hiyo zone iendelee kuwa valid basi lazima ije irudi baada ya siku 30 kinyume chake basi hiyo zone haitokua valid tena, so ndio maana kuna wakati unaweza ukaona zone ambayo unaamini ni kongwe lakini bado ikawa iko valid ni kutokana na kwamba price ilirudi kwenye eneo hilo kwa muda sahihi na sio kwamba eti ni kongwe hapana.

Sasa unaweza ukajiuliza kwanini price ikitoka kwenye zone itaenda then itarudi baada ya muda flani?

Hii inatokana na kwamba, banks nyingi huwa zinapenda kuweka order zao kwenye zone so price ikifika kwenye zone tu basi bank wataweka order zao hapo, kama ni kwenye supply basi wataweka order za kusell na kama ni kwenye demand basi wataweka order za kubuy, sasa kipindi wanapobuy au kusell katika zone watakwenda na price katika umbali ambao wao watahitaji then wakishafika hapo basi wataanza kuchukua faida zao na kipindi wanafanya hivi basi reversal itatokea na price itaanza kugeuka kurudi tena kwenye zone, na hapa sasa watawavutia ma retailer wengi watadhani sasa trend imechange wataanza kuingia na price ikifika tena kwenye zone bank watatumia ile faida yao waliyoipata kurudisha tena price kule ilikotoka na hapa wengi wataliwa ela zao....hii ni sababu ya kwanza.

Sababu ya pili ni kwamba bank nyingi huwa hazipendi kuuza au kununua katika umbali ambao price zimeachana sana, so ili iwe rahisi kwa wao kucalculate faida wanayohitaji basi wataweka order kwenye zone wataishusha price ila katika izo order kuna zingine zitasalia kwenye zone so watakwenda na order chache then wakishapata faida wanayoitaka watamanipulate soko yani watalipeleka vile wao wanataka na hapa watachukua faida then price itarudi kule kwenye order zao then wataziingiza na hizo order sokoni tena na hapo mambo yatarudi yalikotoka so hii pia itawasababishia watu wengi yani akina sisi kula za us

Ila kuna wakati unaweza ukaona price imetoka kwenye zone ikaenda kwenye upande tarajiwa kwenye upande wa supply au upande wa demand, ila baadae ikafika sehemu price ikawa inarudi sasa ilikotoka na ikafika kwenye zone ikapitiliza hadi upande wa pili, hapa tunasema hao mabank hapa walishatoka so hakuna order ambazo zilibaki kwenye hiyo zone na ndio maana price iliporudi kwa Mara ya pili ikapitiliza, na hapa sasa investor wengine wataingia coz wataamini zone ambayo ilikuepo mwanzo now imekua si valid tena kwahiyo nao wataweka order zao then price itakwenda kwenye upande ambao order ni nyingi.

NB:
Wingi wa order hausababishwi na uwingi wa watu katika demand au katika supply, isipokua anaweza akawa mtu mmoja tu ambae anaela nzuri akaweka order za kutosha na akayumbisha soko na hata kama upande mwingine unawatu elfu kumi ila wakawa na order ambazo ndogo kuliko alizotoa huyo mtu mmoja basi hawatokua na ujanja wa kuyumbisha soko richa ya uwingi wao...na hii aliifanya George Soro

Forex ni nini?

FOREX ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni ambayo imeonekana kuwa na mzunguko mkubwa zaidi kuliko biashara yoyote dunianini kwani inazungusha zaidi ya dolla za kimarekani trillion 5 kwa siku.

Mtu yoyote anaweza kujifunza biashara ya forex, na kuwa Forex trader mwenye mafanikio. Ili kuwa Forex trader, ni lazima uwe na account ya Forex

Biashara ya Forex imechangiwa sana na mapinduzi ya teknolojia ambapo sasa mtu yeyote unaweza ukafanya biashara hii mahali popoke akiwa na huduma ya mtandao wa intaneti kwa kompyuta au simu janja(smartphone)

  1. Forex ni kifupisho cha FOReign EXchange kwa maana ya biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni. Kama unavyoijua kazi ya Bureau de Change, ndiyo iyo hiyo tunaifanya kwenye Forex sema hii ni ya mtandaoni.
  2. Forex ni biashara halali na inafanyika ulimwenguni mwote na taasisi kubwa kubwa za kifedha na mabenki na central banks.
  3. Biashara hii ni ya mtandaoni na wauzaji na wanunuzi hukutana huko ~soko lake ni la mtandaoni na ni la dunia nzima. Inakadiriwa kuwa, biashara hii imevutia wawekezaji ambao kwa pamoja (wakubwa na wadogo) wanaTRADE zaidi ya US Dollars Trilioni 5.3 kila siku!
  4. Hii biashara kwa kuwa ni ya mtandaoni, ukitaka kuifanya ni lazima uwe na fedha mtandaoni. Unafungua account mtandaoni kama unavyofungua bank, unaweka fedha zako. Unazifanyia biashara na siku ukitaka kuzitoa, unazitoa mtandaoni zinakuwa cash za kutumia.
  5. Biashara hii, kwa kuwa ni ya mtandaoni, unaweza kuifanyia popote! Nyumbani, chumbani, njiani, sokoni..popote! Unahitaji tu vitu vitatu:
    • Computer/Laptop ambayo itakusaidia kuliangalia soko na kujua muelekeo (Market Analysis) 
    • Internet connection. Kwa sababu ni biashara ya mtandaoni, unahitaji kujiung na mtandao.
    • Programu maalum yenye uwezo wa kusoma soko. Hii inaitwa Trading Platform. Hii ni software ambayo, unai~download na kui~install kwenye Computer yako. Hizi ziko nyingi sasa lakn moja maarufu ambayo inatumika sana duniani inaitwa Meter Trader 4 (MT4).

Note 1:
Ni lazima uwe na Computer/Laptop au smartphone na u-install MT4 kama unafanya Market Analysis mwenyewe lkn, kama kuna mtu mwingine anaweza kufanya kwa niaba yako na akakupa kile tunaita Trading Signal, sio lazima uwe na computer, unaweza tu ukawa na simu yako au gadget yoyote ile inayoweza kuunganishwa na mtandao. Note 2:
Baada ya kutimiza hayo, kabla hujaanza KUNUNUA NA KUUZA fedha za kigeni mtandaoni, Ku Trade Forex, unamuhitaji mtukati anayeitwa Broker. Kwanini? Nitafafanua zaidi pale chini lakini, kwa hapa niseme tu, ndiye anayesimama kama bank ya mtandaoni kwako. Utafungua account kwake kama unavyofungua account NMB, NBC, Equity, Exim, n.k. Utampatia taarifa zako zote rasmi, Vitambulisho vyote muhimu, Uraia, Anuani ya unapoishi,...kila kitu. Ndipo atakuruhusu kufungua account ya mtandaoni. Niwaonye wanaopenda kudanganya, hapa usijaribu, utafeli. Hapa wanahitaji taarifa zako halisi na sahihi. Hii ni kwa sababu, hii ni biashara halali kabisa, na ni ya dunia nzima na, inakupatia kipato halali. Sasa, siku umepata faida unataka kuzitoa pesa zako, watakuambia hatukupi maana si wewe, endapo utawasilisha utambulisho mwingine tofauti na ule uliojazaga. Baada ya kuifungua account kwa Broker, unaweka hela zako humo, labda USD, GBP, JPY..utakavyo mwenyewe.

Baada ya hapo, sasa upo tayari kuanza biashara.

Forex ni nini?


Katika kuanza biashara ya Forex, jambo kubwa na la muhimu ni kuhakikisha una trade kupitia broker ambaye yupo regulated, na anaaminika zaidi ili kuepuka matatizo mbali mbali yanayotokana na ku trade kupitia broker asiye na sifa.

Bofya link ifuatayo kutengeneza account kupitia broker anayeheshimika zaidi duniani na mwenye clients zaidi ya 2 milion kutoka nchi mbali mbali duniani ikiwemo Tanzania na Kenya na nchi zote za Afrika Mashariki.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT


Zinazosomwa Zaidi

Followers