Showing posts with label Kenya. Show all posts
Showing posts with label Kenya. Show all posts

Jinsi ya kutuma pesa kutoka Safaricom Kenya kwenda Vodacom Tanzania

Kutokana na ongezeko la watumiaji wa Safaricom M-Pesa wanaohitaji kutuma pesa kwenda Vodacom M-Pesa Tanzania, nimeamua kuandika makala hii ili kuwasaidia wale ambao hawafahamu jinsi ya kufanya muamala huo.

Fuata mtiririko ufuatao kufahamu jinsi ya kutuma pesa kutoka M-Pesa Kenya kwenda M-Pesa Tanzania
  1. Kwenye simu yako, fungua application ya ku manage SIM CARD (Sim Toolkit)
  2. Chagua Safaricom kisha fungua M-Pesa
  3. Chagua "LIPA NA MPESA"
  4. Chagua Pay Bill kisha weka namba ya biashara yaani Business Number ambayo ni 255255
  5. Sehemu ya kuweka "Account Number" weka namba ya simu ya Tanzania kwa kuanza na code ya Tanzania pekee bila + yaani 2557XXXXXXXX
  6. Andika kiwango unachotaka kutuma katika Kenyan Shillings KES.
  7. Ingiza namba yako ya siri ya M-Pesa halafu kubali muamala.
Baada ya kukamilisha mtiririko huo, utaulizwa kama unataka kuzuia muamala, uandike herufi yoyote ndani ya sekunde 25, usiandike chochote, acha kama palivyo au waweza bofya CANCEL, baada ya hapo utaambiwa "Thanks for using M-Pesa" na kiwango ulichotuma kitatumwa moja kwa moja kwenye namba uliyotuma Tanzania.

NJIA MBADALA
Iwapo upo Tanzania, na ungependa kutoa pesa moja kwa moja kutoka kwenye laini yako ya Safaricom bila kuituma Vodacom kwanza, unachopaswa kufanya ni ku bofya namba ya M-Pesa ya Safaricom ambayo ni *840#. 

Kama ndio mara yako ya kwanza kubofya namba hiyo, utaambiwa uandike eneo ulilopo, utaandika eneo lolote ulilopo kwa Mfano, Dodoma, au Arusha.

Baada ya kufanikiwa kuhifadhi eneo ulikopo, utabofya tena *840# na utachagua ROAMING PICK UP, hapo sasa utaweka nambaya wakala wa M-Pesa unapotaka kuchukua pesa yako na utaendelea kufuata maelekezo kama kawaida, kwenye njia hii ya pili, badala ya kuweka kiwango kwenye Shilingi za Kenya, unaweka katika Shilingi za Tanzania.

Endelea kuwa pamoja nasi kufurahia elimu tunayoitoa kupitia blog hii ya Biashara ya Forex.

Jinsi ya kudeposit Templerfx kwa kutumia Safaricom M-Pesa

Iwapo una laini ya Safaricom na unatumia huduma ya M-Pesa Kenya, na unataka ku deposit pesa kwenye account yako ya TemplerFx, fuata mtiririko huu ili kufahamu jinsi ya ku deposit kiasi cha pesa upendacho.

Kama bado huna account ya Forex kupitia TemplerFx, bofya kitufe kifuatacho kujiunga:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Jambo la kwanza ni kuhakikisha account yako ya M-Pesa ina balance inayolingana na  kiasi unachotaka ku deposit, waweza kuwa na kiwango chochote kisichopungua KES 200 au Kiwango cha KES kinacholingana na 1 USD

Deposit to forex using mpesa


Jinsi ya kuweka na kutoa pesa Templer Fx kwa Safaricom M Pesa:
  1. Kwa kutumia computer yako, Login kwenye account yako ya TemplerFx
  2. Kwenye menu ya upande wa kushoto, bofya palipoandikwa Finance
  3. Chini yake utaona Deposits, bofya link hiyo.
  4. Kwenye ukurasa utakaofunguka, chagua account unayotaka ku-deposit, na iwapo bado hujatengeneza account, utaambiwa utengeneze account.
  5. Ukishachagua account, bofya sehemu iliyoandikwa Select a payment System
  6. Chagua palipoandikwa IPay Africa
  7. Baada ya hapo utachagua Method of payment
  8. Hapo sasa utachagua M-Pesa Kenya
  9. Bofya/Tick sehemu ya kukubali vigezo na masharti na iwapo ungependa bonus pia.
  10. Bofya kitufe kilichoandikwa DEPOSIT KES XXX 
TemplerFx M-Pesa Deposit

Kwenye page itakayotokea ya kufanya malipo, iwapo upo Tanzania au ncho tofauti na Kenya, utalazimika ku-edit namba yako iliyopo, na kuweka namba yako ya Safaricom, utafanya hivyo kwa kubofya ki-tick kilichoandikwa (I need to change ...) kisha utaweka namba yako ya Safaricom bila kuweka code yaani utaanza na  07XXXXXXXX

Ukisha edit namba yako na kuweka namba ya Safaricom, utabofya PAY NOW, na hapo iwapo unatumia Smart Phone, utakuwa Prompted kwenye simu yako kuweka namba ya siri.

TemplerFx M-Pesa Deposit

Iwapo laini yako ya Safaricom ipo kwenye simu isiyo smart (kitochi) basi waweza amua kutumia njia ya zamani kwa kubofya maneno yenye rangi ya brown yaliyoandikwa

I did not get a prompt on my phone. Take me to the previous MPESA payment method

Baada ya hapo, fuata maelekezo yafuata jinsi ya kulipa pesa, na muda huo huo ukishalipa utaona balance yako kwenye account yako ya TemplerFx
 
Na iwapo bado hujawa na account ya TemplerFX, bofya kitufe kifuatacho kujiunga:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Zinazosomwa Zaidi

Followers