Mbinu kuzuia hasara kwenye biashara ya Forex

Iwapo ndio kwanza umeanza biashara ya Forex, au tayari ni trader mzoefu wa Forex, jambo la msingi kabisa ambalo unapaswa kuzingatia muda wote unapofanya biashara hii ni namna ya kuhakikisha kwamba pesa yako inabaki salama kwa kuzingatia mbinu mbali mbali zenye lengo la kuhakikisha unaepukana na uwezekano wa kuunguza account yako au kufunga positions zako kwa hasara kubwa.

Forex Risk Management

Zipo mbinu mbali mbali ambazo trader unapaswa kuzizingatia ili kuweza kuwa na uhakika wa pesa yako kubaki salama.

Iwapo ndio unaanza kujifunza Forex, na bado hujatengeneza account, bofya kitude kifuatacho kujiunga na Forex:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Kama tulivyokwisha kusoma kwenye post zilizopita pamoja na angalizo juu ya biashara ya Forex, unapaswa kufahamu kwamba haijalishi kwamba una uzoefu na elimu kiwango gani juu ya Forex, muda wowote unaweza kupata hasara itakayopelekea sehemu au pesa yako yote kupotea.

Sasa ili angalau kuweza kuzuia hasara au upotevu wa pesa yako kwenye biashara hii ya Forex, yakupasa kuzingatia mambo yafuatayo:

1. Soma na Fuatilia

Kujifunza kuhusu Forex, jinsi inavyofanya kazi, misingi yake na technique zake zote ndio msingi mkubwa wa mafanikio katika biashara ya Forex. Iwapo utaamua kuwa Forex trader, basi yakupasa uwe makini na kuwa active kwenye kufuatilia mambo mbali mbali au news zinazoweza kupelekea movement kubwa kwenye masoko ya Forex, jambo hili litakusaidia kufanya maamuzi sahihi pale unapoamua kuingia sokoni.

Kusoma na kufuatilia, kutakufanya kuwa na hali ya kujiamini pale unapoamua kuingia sokoni kwa kuwa yapo matukio makubwa ya kisiasa na kiuchumi yanayoweza kugeuza uelekeo wa soko ghafla na kujikuta ukiingia kwenye hasara kubwa.

2. Epuka Brokers wanaolalamikiwa sana

Uzuri tunaishi kwenye nyakati ambazo ni rahisi kufahamu heshima/reputation ya broker unayetaka kujiunga naye, waweza kufahamu zaini kuhusu broker huyo kwa ku search kwenye mtandao au kutembelea tovuti iitwayo ForexPeaceArmy ili kufahamu ni kiwango gani cha malalamiko broker huyo anayo, ni vizuri pia kufahamu mambo mbali mbali kuhusu broker huyo ikiwa ni pamoja na kufahamu njia za kuweka na kutoa pesa, ufahamu fee zao, na pia hakikisha ni broker ambaye yupo regurated na vyombo vinavyoheshimika kufanya regulations za taasisi za fedha.

3. Anza na account ya majaribio (demo account)

Tumeshajifunza jinsi ya kutengeneza account ya demo kwa ajili ya kuanza ku practise ku trade Forex, waweza soma post hii:

Jinsi ya kufungua na kutumia Demo account kwenye Forex

Ni vyema kabla hujaanza kuweka pesa zako kwenye Forex, ukajaribu kutumia demo account ili kujifunza zaidi na kupima uelewa wako juu ya ku trade Forex, vinginevyo kama huna ufahamu wa kutosha, ukikimbilia kuanza ku trade moja kwa moja kwa real account, utapoteza fedha zako.

4. Epuka kutumia Leverage kubwa sana

Moja kati ya sababu zinazofanya Forex ipendwe zaidi ni matumizi ya leverage, leverage ni utaratibu unaowekwa na broker wa kuhakikisha kwamba una uweza wa kupata faida kubwa hata kama kiwango chako ulicho deposit ni kidogo, leverage ni uwiano wa kiwango cha pesa ulicho nacho, na kiwango cha pesa unacho trade. Matumizi ya leverage kubwa yanakupa uwezekano wa either faida kubwa sana, au hasara kubwa sana kwa muda mfupi.

Jinsi ya kucheza forex

Bila shaka umefika kwenye post hii baada ya ku search neno jinsi ya kucheza forex lakini inakupasa kufahamu kwamba Forex sio mchezo wa kubahatisha kama ilivyo michezo mingine ya kubahatisha au Ku-bet kama Sportpesa, Biko n.k

Forex ni biashara inayohitaji ueledi wa hali ya juu katika kutathmini uelekeo wa masoko  ya fedha za kigeni.

Forex inahitaji uwe na uelewa mpana, pamoja na mbinu za kuweza kulielewa soko la fedha ikiwa ni pamoja na kufanya mahesabu mbali mbali yatakayokupa uwezo wa kufahamu ni wakati gani wa kuingia sokoni na ni wakati gani wa kutoka sokoni.

Sasa basi, kama umeshafahamu kwamba Forex sio mchezo wa kuchezwa kama BIKO n.k, ni wakati wako sasa kufahamu ni jinsi gani ya kuweza kujiunga na biashara hii ya Forex. Kupata maelekezo yaliyojitosheleza juu ya namna ya kujiunga na biashara ya forex, bofya link ifuatayo:

Jinsi ya kujiunga na biashara ya Forex

Ukishapitia na kuisoma kwa kuelewa post hiyo, utaweza kufahamu sasa kwamba kumbe cha kwanza kabisa ni kuwa na broker atakayekuwezesha ku trade Forex, ambaye kwa sisi tuliowengi hapa Afrika Mashariki, tunapenda kumtumia broker aitwaye TemplerFx, ambaye kwa bahati nzuri, atakuwezesha kuweka na kutoa pesa zako kwa njia ya M-Pesa.

Kufungua account ya Forex bofya kitufe kifuatacho:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Ambapo utaweza kusoma maelekezo utakayopatiwa ikiwa ni pamoja na ku verify email yako, namba yako ya simu, na taarifa zako za msingi.

Jinsi ya kutoa pesa Skrill kwenda M-Pesa Tanzania

Katika post hii tutaona njia unayoweza kuitumia kuhamisha pesa kutoka Skrill kwenda M-Pesa Tanzania. Skrill ni moja kati ya huduma nzuri kabisa za kutuma, kupokea pesa na kufanya malipo mtandaoni.

Skrill to M-Pesa Tanzania


Kama bado hujajiunga na huduma hii, bofya kitufe kifuatacho kufungua account Skrill.

 

Au waweza soma post hii kuhusu jinsi ya kufungua account Skrill:

Jinsi ya kufungua account Skrill

Kama tayari una account Skrill, na unajiuliza ni mbinu gani utumie kuhamisha pesa zako kwenda M-Pesa Tanzania, ungana nami katika mtiririko huu:

Cha kwanza kabisa hakikisha una account ya Forex ambayo iko Verified kwa broker wa TemplerFX, kama bado huna, account TemplerFX, hakikisha unatengeneza account kwa kubofya kitufe kifuatacho:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

  • Ukishafungua account, hakikisha umei verify, kwa ku upload vitambulisho vyako, pamoja na ku verify card yako ya bank (utaelekezwa kufuta baadhi ya namba zilizopo kwenye card yako ya bank)
  • Ukishakua na full verified TemplerFx account, nenda kwenye sehemu ya ku deposit pesa, ambapo utaona njia mbali mbali za ku deposit
  • Chagua Skrill kama njia ya ku deposit
  • Deposit kiasi cha pesa unachotaka, nacho kitahamishwa muda huo huo kutoka Skrill kwenda TemplerFx.
  • Kiasi chako cha pesa kikishaingia TemplerFx, waweza sasa ukachagua ku withdraw, ambapo utachagua njia ya wallet, ambayo itakuelekeza hatua zifuatazo, na wewe utachagua M-Pesa, kisha utachagua namba yako ya M-Pesa na baada ya hapo muda huo huo kiasi hicho cha pesa kitakua kimehamishwa kutoka TemplerFX kwenda kwenye namba yako ya M-Pesa.
Kama umefurahishwa na post hii, usisahau ku share kuwafahamisha wengine.

Jinsi ya kufungua account Skrill

Skrill ni huduma nzuri sana ya pesa ambayo watu wengi wa Forex hupenda kuitumia na huduma hii ni mbadala mzuri kwa PayPal.

Skrill Tanzania - Skrill Kenya

Waweza tumia Skrill kutuma na kupokea pesa kwa watu mbali mbali duniani, na kufanya malipo mbali mbali pamoja na ku deposit pesa kwenye account ya Forex ambapo brokers mbali mbali hutumia njia hii ya Skrill.

Kujiunga na huduma hii nzuri ya Skrill, bofya kitufe hiki hapa chini:



Kwa wale waliopo Kenya, kuna njia ya moja kwa moja ya kuhamisha pesa kutoka Skrill kwenda M-Pesa na kwa walio Tanzania, pia kuna njia ambayo waweza itumia kuhamisha pesa kutoka Skrill na kuhakikisha imeingia M-Pesa. Soma post ifuatayo kujua namna ya kuhamisha pesa kutoka Skrill kwenda M-Pesa Tanzania.

Jinsi ya kuhamisha Pesa kutoka Skrill kwenda M-Pesa Tanzania

Endelea kuwa pamoja nasi katika mafunzo haya ya mbinu mbali mbali za kufanya biashara ya forex kwa mafanikio.

Jinsi ya kufungua na kutumia DEMO account kwenye Forex

Jinsi ya kufungua na kutumia DEMO account kwenye Forex

Kama tulivyokwisha ona umuhimu wa kuwa na ujuzi wa kutosha kabla hujaanza rasmi ku trade Forex kwa kutumia real account, ni muhimu kuanza na practice account ambayo itakuwezesha kufahamu trend ya soko, na taratibu mbali mbali za ku trade Forex.

Jinsi ya kufungua demo account

Forex Demo Account ni nini?

Forex demo account ni aina ya account maalum ya Forex ambayo inatolewa na wawezeshaji (trading platform au broker wako) ambayo imewekewa kiasi cha pesa ambazo sio halisi kwa ajili ya wewe kujifunza namna ya kufanya biashara ya Forex.

Tofauti ya Demo account na Real account ni kwamba Demo account imewekewa kiasi cha pesa ambacho ni fake, wakati account halisi au real account ni account ambayo umeiwekea pesa halali.

Njia rahisi kabisa ya kufungua account ya demo, ni ku download program ya Meta Trader 4 kwenye simu yako au kwenye computer yako, na baada ya ku install programu hiyo, automatically itakutengenezea account ya demo ambayo waweza itumia kufanya trading za majaribio wakati ukiendelea kujifunza. Iwapo ungepende kufungua LIVE account, basi bofya kitufe kifuatacho:
BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT
Ambapo utaweza kufungua REAL account kwa broker TemplerFx

Jinsi ya kufungua account Forex

Jinsi ya kufungua account Forex

Baada ya kujifunza jinsi ya kujiunga na Forex, na kufahamu kwamba unapaswa kuanza biashara ya Forex kwa kufanya majaribio kwa kutumia account ya DEMO, sasa ni wakati muafaka wa kujua jinsi ya kujiunga na biashara hii kubwa duniani.

Jinsi ya kufungua account Forex
Jinsi ya kufungua account Forex
Kama hukusoma kuhusu jinsi ya kufungua na kutumia demo account ya forex, soma post hii:

Jinsi ya kufungua na kutumia DEMO account kwenye Forex

Kifuatacho sasa ni kufahamu jinsi ya kufungua account ya FOREX, kama nilivyokwisha kuwafahamisha hapo awali kwamba jambo la msingi ni kuchagua broker ambaye utakua unamtumia katika biashara ya forex, na kwa kuwa tunafahamu kwamba broker ambaye atakuwezesha kutuma na kupokea pesa kwa East Africa kwa urahisi zaidi kwa sasa ni TemplerFx ambaye anakuwezesha kutuma na kupokea pesa kwa huduma ya M Pesa ya Vodacom.

Kufungua account ya TemplerFX bofya kiungo kifuatacho ambacho kitakupeleka kwenye fomu maalum ambayo utapaswa kuijaza.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Mara baada ya kutengeneza account, utapaswa kuithibitisha account yako ambapo utaombwa u upload copy ya kitambulisho chako kinachoweza kuthibitisha taarifa kuhusu wewe.

Jinsi ya kujiunga na Forex

Jinsi ya kujiunga na Forex

Baada ya kujifunza kuhusu utangulizi wa biashara ya Forex, sasa ni wakati muafaka wa kujifunza jinsi ya kujiunga na biashara hii ya Forex.

Iwapo tayari umekwisha pitia maelezo ya awali, ni wakati sasa wa kutengeneza account yako ya Forex. Waweza tengeneza account kupitia Broker maarufu zaidi East Africa na Duniani mwenye wateja zaidi ya milion 2.5 katika nchi 190 duniani.

Bofya kitufe kifuatacho kufungua account yako ya Forex bure kabisa:

FUNGUA ACCOUNT

Jambo ambalo ni muhimu zaidi kuhusu biashara ya Forex, ni kufahamu misingi yote ya biashara hii, na kuhakikisha kwamba unafahamu hatua zote muhimu za kuchukua ili kuzuia hasara (Risk Management Strategies)

Jinsi ya kujiunga na forex

Mbinu za kuzuia hasara katika biashara ya Forex unaweza kuzisoma kwenye post ifuatayo

Mbinu kuzuia hasara kwenye biashara ya forex (Risk Management Strategies)

Baada ya kuwa na uelewa mpana wa jinsi biashara ya Forex inavyofanya kazi, na kufahamu mbinu za kuzuia hatari ya account yako ya forex kuungua, sasa unaweza kujiunga na Forex.

Kama ndio unajiunga kwa mara ya kwanza, unashauriwa kuanza kwa kutengeneza account ya majaribio au DEMO ACCOUNT, account hii itakuwezesha kujaribu uwezo wako wa kufanya biashara hii ya forex, kutengeneza account ya majaribio ni rahisi zaidi, kwani unachopaswa kufanya ni ku install app ya Meta Trader 4 kwenye simu yako, account hiyo itakuwezesha kuunganishwa na Forex DEMO bure kabisa bila kupaswa kulipia kitu chochote.

Post ifuatayo nimeandika kwa kirefu kuhusu DEMO account kwenye forex

Jinsi ya kufungua na kutumia DEMO account kwenye Forex

Kujiunga na Forex demo, fungua simu yako, kama ni ya android nenda kwenye Play Store, na kama ni iPhone nenda kwenye App Store, halafu andika neno Meta Trader 4 Hapo itafunguka app hii ya Meta Trader 4 ambapo ukisha i install, moja kwa moja itakufungulia demo account ambayo waweza kuitumia kwa majaribio.

Ukishaweza kutumia demo account vizuri, sasa waweza hamia kwenye REAL ACCOUNT kujiunga na real account waweza mtumia broker wetu ambaye tunamtumia zaidi East Africa anayeitwa XM kwa ku bofya kiungo kifuatacho.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Endelea kuwa pamoja nami katika safari hii ya mafanikio kupitia biashara ya Forex

Jinsi ya kuweka hela Forex

Baada ya kufahamu jinsi ya kutumia M Pesa kuweka hela kwenye account yako ya Forex chini ya broker maarufu East Africa anayefahamika kwa jina la TemplerFX sasa ni wakati wa kujifunza hatua kwa hatua ni namna gani unaweza ukaweka hela kwenye account yako ya Forex.

Jinsi ya kuweka hela Forex
Jinsi ya kuweka hela Forex


Zipo namna nyingi za kuweka hela kwenye account ya Forex kutegemea na broker unayemtumia, wengine wanatumia M-Pesa, PayPal, Visa card au Mastercard, Skrill na baadhi ya njia nyingine za kutuma na kupokea pesa kwa kupitia mtandao.

Kwa kuwa Watanzania walio wengi ni watumiaji wa huduma za fedha kupitia mitandao ya simu, basi tutaenda kujifunza kuweka pesa kwa kutumia M-Pesa.

Kama umeamua kuwa serious na biashara ya Forex, basi ni vyema ukawa na bank account maalum ambayo utaitumia kuweka na kutoa fedha kwa kupitia Visa au Mastercard, njia hizi utaziona pindi unapo bofya kwenye link ya DEPOSIT katika members area ya account yako ya forex.

Na iwapo unalazimika kutumia M-Pesa, basi huna budi kujiunga na broker aitwaye TEMPLERFX kwa kubofya hapa chini:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT
Maelekezo yote ya namna ya kutumia mtandao wa M-Pesa kupitia huduma ya Ipay Africa nimeyaweka kwenye article ifuatayo, bofya link then utaona ni jinsi gani unaweza kuweka hela kwenye account yako ya Forex kwa kutumia M Pesa.

Jinsi ya kuweka hela Forex kwa kupitia M Pesa

Nimatumaini kwamba makala hii imeweza kukuelekeza vizuri namna ambayo waweza itumia kuweka hela kwenye Forex

Na iwapo ungependa kuweka pesa kwa kutumia huduma ya Skrill, bofya link ifuatayo kufungua account Skrill

FUNGUA SKRILL ACCOUNT

Jinsi ya kutumia M-Pesa kuweka na kutoa fedha katika Forex

NOTE:
Huduma ya ku deposit na ku withdraw kwa kutumia M-Pesa Tanzania kupitia Broker TemplerFx kwa sasa imesitishwa hadi hapo iPay na Vodacom watakapokamilisha taratibu zilizowekwa na BOT.
Huduma hii inaendelea kupatikana kupitia Safaricom M-Pesa Kenya ambapo waweza ku deposit au ku withdraw kwa kuchagua M-Pesa Kenya.
Kama bado huna account ya Forex kupitia TemplerFx, bofya kitufe kifuatacho kujiunga:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Moja kati ya changamoto nyingi zinazoikumba biashara ya Forex hususani kwa nchi zinazoendelea ni namna bora ya kuweka na kutoa pesa kwenye account yako ya Forex.

Templer fx M Pesa
Templer Fx M Pesa

Jambo hili kwa kawaida huwa linasimamiwa na broker uliyeamua kumtumia. Brokers walio wengi wanakuwezesha kuweka pesa kwenye account yako kwa kupitia njia ya Bank kupitia credit cards kwa mfano Visa au Mastercard.

Jambo zuri kwa forex Traders wa East Africa ni kwamba yupo broker ambaye anakuwezesha kuweka na kutoa pesa kwa kutumia Vodacom M-Pesa papo kwa papo. Broker huyu si mwingine bali ni TemplerFx ambaye anatumia huduma ya iPay Africa kukuwezesha kuweka na kutoa pesa kwenye account yako ya M Pesa muda wowote. Sasa tukaangalie ni kwa jinsi gani unaweza kutumia huduma hii.

Bofya kitufe kifuatacha kujiunga na Templer Forex kutumia huduma ya M-Pesa kuweka na kutoa pesa kwenye Forex:

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Jinsi ya kuweka na kutoa pesa Templer Fx kwa M Pesa:

Ikiwa umeshajiunga na tayari una account ya templerfx ambayo ni verified. Fuata mtiririko ufuatao:
  1. Kwa kutumia computer yako, Login kwenye account yako ya TemplerFx
  2. Kwenye menu ya upande wa kushoto, bofya palipoandikwa Finance
  3. Chini yake utaona Deposits, bofya link hiyo.
  4. Kwenye ukurasa utakaofunguka, chagua account unayotaka ku-deposit, na iwapo bado hujatengeneza account, utaambiwa utengeneze account.
  5. Ukishachagua account, bofya sehemu iliyoandikwa Select a payment System
  6. Chagua palipoandikwa IPay Africa
  7. Baada ya hapo utachagua Method of payment
  8. Hapo sasa utachagua M-Pesa Tanzania, iwapo upo Tanzania au M-Pesa Kenya iwapo upo Kenya
Baada ya hapo, fuata maelekezo yafuata jinsi ya kulipa pesa, na muda huo huo ukishalipa utaona balance yako kwenye account yako ya TemplerFx

Mtaji wa kuanzia Forex

Je unahitaji mtaji kiasi gani wa kuanzia biashara ya FOREX?

Mtaji wa kuanzia Forex

Kama tulivyoona katika mada ya utangulizi kuhusu biashara ya Forex, kwamba Forex ndio biashara kubwa zaidi duniani ambayo ina mzunguko wa dola za kimarekani trilioni 5 kwa siku. Iwapo na wewe ungependa kuwa sehemu ya mzunguko huu wa pesa, huna budi kujifunza vizuri misingi yote ya biashara hii yenye ushindani mkubwa, ili kuepuka kupata hasara.

Kiwango cha awali cha kuanzia biashara ya FOREX kinategemea na dalali wako wa forex (Forex broker), wapo baadhi ya Forex brokers ambao unaweza ukaanza na kiwango kidogo kidogo cha dola 10 na wengine hata dola 1.

Tena baadhi ya brokers hawa, watakupatia pesa ya ziada ya kulinda account yako kama mkopo (Credit) kwa mfano broker maarufu ajulikanae kwa jina la XM.COM yeye anakuwezesha kuanza na mtaji mdogo wa dola 5 na kukupatia mkopo wa dola 30 iwapo utafungua MT4 account aina ya STANDARD.

Broker mwingine ambaye amekua akitumiwa na watanzania wengi ni TEMPLERFX ambaye anakuwezesha kuanza na kiwango kidogo zaidi cha dola 1 (naam, dola moja tu) ambacho unaweza kuki deposit kwa kutumia account yako ya M-Pesa.

Historia inaonesha kwamba, ni wafanyabiashara wachache sana wa FOREX ambao wana uwezo wa kuanza na kiwango kidogo cha pesa na kuweza kukipandisha hadi kufikia kiwango kikubwa kwani unapokua na balance ndogo, ndivyo ambavyo ni rahisi kwa account yako kuisha pale soko linapo panda na kushuka.

Iwapo ungependa kujiunga na broker anayekuwezesha kuanza na kiwango kidogo cha dola 5 ambacho waweza kukiweka kwa kutumia M-Pesa Mastercard au Skrill, bofya kiungo kifuatacho.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT

Na iwapo hujafahamu jinsi ya kuweka na kutoa pesa za forex kwa kutumia Vodacom M-Pesa, bofya link ifuatayo ambayo nimekuandalia maelezo mengi juu ya namna ya kutumia M-Pesa kuweka na kutoa pesa ya Forex.

Jinsi ya kutumia M-Pesa kuweka na kutoa fedha katika Forex

Jinsi ya kufanya biashara ya FOREX

Post iliyopita ilikuwa na utangulizi muhimu kuhusu FOREX, kama hujaisoma, waweza bofya kiungo kifuatacho kuisoma:
Forex ni nini?

Kama tayari una uelewa wa awali wa biashara hii, bofya kiungo kifuatacho ili ujisajiri na broker anayekubalika zaidi East Africa!

BOFYA HAPA KUJIUNGA

Sasa twende Sokoni. Twende kwa Hatua pia:

1. Forex inafanyika kwa kulinganisha thamani za Sarafu Mbili kwa pamoja (Currency Pairs).
Kule sokoni unapoingia, ili uweze kununu na kuuza, utakuta bidhaa (currency) zimewekwa kwenye mafungu mafungu ya mbili mbili (pairs). Mfano:
i)Euro na US Dollar pamoja,
ii) Paund (GBP) na USD pamoja,
iii) USD na Yen (JPY) pamoja,..nk. nk. nk
Zinavyopangwa, utazikuta hivi:
EUR/USD
USD/JPY
GBP/USD
USD/CAD

Chukua EUR/USD kwamfano;
Hiyo ya mwanzo (EUR) Inaitwa BASE currency, na hiyo ya pili, USD, unaitwa COUNTER Currency. Sasa, bei unazoziona kwenye grafu zikipanda na kushuka ni bei za Base Currency kwa kulinganishwa na Counter Currency. Chukulia hii;

EUR/USD = 1.25358

Maana yake, Euro 1 = 1.25358 USD. Kama unataka kununua EURO 1, utalipa 1.25358 USD.

Bei za Euro sokoni, kwa kulinganishwa na USD, zinaweza kubadilika ndani ya sekunde! Sasa, faida zinapatikana kwa wewe KUNUNUA Currency moja, wakati bei iko chini na KUIUZA wakati bei inapopanda. As Simple as that. Sasa, ili kujua kwamba baada ya muda itapanda ili UNUNUE sasa hivi na uuze itakapopanda, au, kujua kwamba itashuka zaidi ya hapo ilipo ili, UUZE sasa hivi na UNUNUE itakapofika bei ya chini zaidi,...mchakato huo unaitwa MARKET ANALYSIS.

2. Forex Trading, hufanyika kwa "Kubonyeza tu" kitufye cha kuBUY au cha kuSELL. Basi. Hilo tu. Unakuwa umefanya TRADE. Lakini sasa, ili uweze kujua, unabonyeza kipi, muda gani, uTRADE kiasi gani ili upate faida gani, inabidi uwe unajua kufanya MARKET ANALYSIS mwenyewe au uwe na MTAALAMU unayemuamini akufanyie na akupe taarifa hiyo. Sasa, hiyo taarifa ndiyo inaitwa "Fx Signals" au "Trade Signals"..nk.

3. Faida au hasara kwenye Forex Trade zinapimwa kwa PIPS.

PIP ni kitu Gani? Kitefu chake ni "Percentage In Point". Pip ni tofauti ya POINT MOJA katika bei ya Pair ya Currency tokea ulipoweka ORDER yako. Its a 1point Price Movement ama kwenda juu au kuja chini.

Hii tofauti ya bei (Pip) inapimwa katika viwango vya Desimali. Currency Pairs nyingi (sio zote tafadhali) zinatumia SEHEMU NNE ZA DESIMALI. Utakuta kwenye Platform wanaandika SEHEMU TANO lakini ni ili kukusaidia wewe mfanyabiasha, ila zinazohesabika ni NNE.

 Utaelewa vizuri kwenye mfano. Chukulia hiyo ya pale juu:

EUR/USD = 1.25358

Tunaangalia "Price Movement" katika sehemu ya 4 ya desimali. Ile ya tano inakupa tu sehemu ya Pip.

Chukulia hapo bei ibadilike ama kwenda juu au chini kama ifuatavyo:


EUR/USD = 1.25458
                     ⬆️
EUR/USD = 1.25358
                     ⬇️
EUR/USD = 1.25258

▶️ Kutokea 1.25358 kwenda 1.25458 maana yake bei imepanda kwa 10pips.

▶️ Kutokea 1.25358 mpaka 1.25258 bei imeshuka kwa 10pips.

Swali, je kutoka 1.25258 mpaka 1.25200?

Jibu, imeshuka kwa 5.8pips. Sawa mpaka hapo?

Kwa hiyo, FAIDA na HASARA katika Forex zinapimwa kwa PIPS. Ukiwakuta watu wanaambiana, mimi leo nimepata, 30 USD, 50 Yen, 70 Paunds...unajua tu hawa sio professionals. Kule watu wanajisifia Pips sio Dola au Paundi au Yen. Utakuta mtaalam anasema, Mimi ninapata Average/Wastani wa 500Pips, au 700Pips au 1100Pips kwa wiki au kwa mwezi, nk. Sio Dola! Na mtaalamu anayependwa na wateja,..Anayeaminiwa kwamba anao uwezo wa Market Analysis mzuri ni yule anayejikusanyia PIPS nyingi mwisho wa siku.

Swali: Je, naweza kupata PIPS kidogo na nikawa na faida KUBWA kuliko aliyepata PIPS nyingi kunizidi?

Jibu: Ndio. Inawezekana! Lakini, wooote, tutakujua kwamba huna PROFFESSIONALISM bali umeRISK sana na ungeweza ukapoteza hela nyingi sana pia! Sema tu bahati yako leo. Hakuna mtu mwenye hela zake atakayekuamini tukikujua hivyo. Nitaeleza zaidi hili sehemu inayofuata.

5. Nini Thamani ya PIP moja? Ili nijibu hili swali, kuna maelezo lazima nikupe. Ila kwa kifupi, thamani ya PIP moja inaweza kuwa ni 10 USD, au 1 USD, au 0.1 USD. Angalia:

Kumbuka, hii ni biashara kubwa sana. Kule kwenye soko la dunia, CURRENCY zinauzwa kwa jumla. Huwezi kwenda kununua eti Dola 1, au Paundi 5 au Euro 8. No. Unanunua kwenye mafungu! Kule kuna mafungu matatu tu maalum yanayouzwa:

a) 100,000 USD, au
b) 10,000 USD, au
c) 1,000 USD

Kwani hata Buteau de Change si wanauza kwa mafungu? Utakuta;

1 - 50 USD bei yake
51- 100USD bei yake
101- 1000USD bei yake
N.k. nk, nk..ndo ivo ivo kule.

Sasa,..

Wale waliosoma Science Sekondary mnikumbushe hii: S.I Unit maana yake nini tena? International Standard Unit? Nimesahau. Ila maana yake ni hii. Kipimo maalum kilichokubalika dunia nzima kupimia kitu mfano;
Urefu, S.I.Unit ni Meter
Ujazo, S.I.Unit ni Litre
Uzito, S.I.Unit ni Gram
N.k, n.k,...

Sasa kwenye Forex, kipimo kilichokubalika kupimia kiwango cha MAFUNGU ya kuuza na kununua Currency kinaitwa "Lot" Tumezoea kuita, "Standard Lot".
➡️ Lot moja ukiigawa kwa KUMI utapata 1 Mini~Lot.
➡️ Mini~Lot moja ukiigawa kwa KUMI (au Standard Lot moja ukiigawa kwa MIA) unapata 1 Micro~Lot.

Angalia sasa;

1 Std Lot = 100,000 USD,
1 Mini~Lot = 10,000 USD
1 Micro~Lot = 1,000 USD

Nenda kinyumenyume, utaona kwamba:

1lot = 10 mini~lots = 100 micro~lots

Au kwa namna nyingine;

1Micro~lot = 0.1 Mini~lot = 0.01lot.

Sasa, unapokwenda KUPLACE ORDER ya kuBUY au kuSELL kuna sehemu utaulizwa ujaze SIZE ya ORDER yako. Utajaza 1Lot kwa maana ya unanunua au kuuza 100,000USD au utajaza 0.1lot kwa maana ya unauza au kununua 10,000USD au utajaza 0.01lots kwa maana ya unauza au kununua 1,000 USD.

Sasa twende kwenye thamani ya PIP.

Endapo ULIUZA au KUNUNUA "1 Standard Lot", kila PIP moja unayoipata sokoni kama faida, ni sawasawa na 10 USD. Maana yake, kwa 100,000 USD ulizoTRADE, umepata faida ya 1PIP au 10 USD.
Kama uliTRADE 1minilot, 1PIP ni sawa na 1 USD na kama uliTRADE 1 microlot, PIP moja ni sawa na 0.1 USD.

Umenielewa mpaka hapo? Ngoja nikusisitize yafuatayo kama NB.

Note1: Si kila Currency Pair PIP yake inapimwa kwa 4decimal places. Kuna baadhi sio, mfano Currency Pairs ambazo zina Japaneese Yen ndani yake kama EUR/JPY au USD/JPY na zingine, PIP yake moja inahesabiwa katika sehemu MBILI za Desimali. Ukishakuwa sokoni utazizoea tu usiogope. Utazijua zote.

Note 2: Sio kila 1PIP ni sawa na 10USD kwa 1lot. Kuna tofauti zake pia. Baadhi ya currency pairs, 1lot zao, 1PIP utakuta ni 8USD, 11USD au hata 7USD. Inategemea. Ile ya 1Pip = 10 USD ni Standard. Utazielewa pia ukishaingia sokoni. Ila mpaka hapa, unaweza kuelewa kwamba, aliyepata 25pips za 1lot za:
i) EUR/USD,
ii) EUR/JPY, na
iii) GBP/USD
wanatofautiana kwenye hela kwa sababu thamani ua 1PIP kwao zinatofautiana. Ila tofauti zao si kubwa saaana. Zoote, zinakaribi pale pale kwenye Kwa 1std lot, 1Pip = 10 USD.

6. Hivi Kweli, kuna Retail Trader ataweza kununua 1lot, au 1minilot, au hata 1microlot (kiasi cha chini kabisa cha order moja ambacho ni 1000usd = 2.4mil Tzs) na akasavaivu kwenye hii biashara kweli. Huko si ni kubaguana? Wataifanya wenye nacho tu, si ndiyo?

Hapo sasa, ashukuriwe Mungu kuna Mtukati anaitwa Broker. Ndiye anayetuwezesha mimi na wewe tushiriki Forex. Vingenevyo, ingebaki kuwa ni biashara ya Mabenki, Serikali, Taasisi kubwa kubwa za Kifedha ma Matycoon wakubwa.

Kazi kubwa ya Broker ni kukukopesha hela zake ili uzifanyie biashara ya Forex. Atakuambia kwamfano; ukifungua account ya mtandaoni kwangu, uka~deposite hela, kwa kila Dola 1 utakayo~deposite, nitakukopesha Dola 100 au, 200, au 500 au wengine mpaka 1000! Hicho kitendo kinaitwa "Leverage".

Wanaandika hivi:

Leverage:
1:50 (kwa kila dola 1 uyakayoweka kwangu, nakukopeaha 50), au
1:100 (weka 1, kopa 100), au
1:500 (weka 1 kopa 500) n.k, n.k


What is PIP in Forex



Kwamfano sasa, ukiweka USD 100 kwenye account yenye Leverage ya 1:500 maana yake ni nini?

Kwa kila dola 1 uliyo~deposite anakukopesha dola 500. Kwa hiyo, jumla utakuwa na dola 100 x 500 = 50,000. Hiyo inaitwa "Purchasing Power". Hapo maana yake ni kwamba unauwezo sasa wa kununua au kuuza USD 50,000 ambayo ni sawa na 0.5 lot size, tofauti na awali ambapo ungetegemea 100$, usingeweza kuuza au kununua chochote (hata order ndooogo kabisa ambayo ni Micro~Lot = 1000usd).

Brokers wanakuchaji wewe comission wakati wowote unapoTRADE, ndipo kipato chao kilipo. Siku nyingine nitawazungumzia kwa undani kidogo hawa maBroker.

Kama tayari una uelewa wa awali wa biashara hii, bofya kiungo kifuatacho ili ujisajiri na broker anayekubalika na kuaminika zaidi East Africa

BOFYA HAPA KUJIUNGA

Forex ni nini?

FOREX ni biashara ya ubadilishaji wa fedha za kigeni ambayo imeonekana kuwa na mzunguko mkubwa zaidi kuliko biashara yoyote dunianini kwani inazungusha zaidi ya dolla za kimarekani trillion 5 kwa siku.

Mtu yoyote anaweza kujifunza biashara ya forex, na kuwa Forex trader mwenye mafanikio. Ili kuwa Forex trader, ni lazima uwe na account ya Forex

Biashara ya Forex imechangiwa sana na mapinduzi ya teknolojia ambapo sasa mtu yeyote unaweza ukafanya biashara hii mahali popoke akiwa na huduma ya mtandao wa intaneti kwa kompyuta au simu janja(smartphone)

  1. Forex ni kifupisho cha FOReign EXchange kwa maana ya biashara ya kununua na kuuza fedha za kigeni. Kama unavyoijua kazi ya Bureau de Change, ndiyo iyo hiyo tunaifanya kwenye Forex sema hii ni ya mtandaoni.
  2. Forex ni biashara halali na inafanyika ulimwenguni mwote na taasisi kubwa kubwa za kifedha na mabenki na central banks.
  3. Biashara hii ni ya mtandaoni na wauzaji na wanunuzi hukutana huko ~soko lake ni la mtandaoni na ni la dunia nzima. Inakadiriwa kuwa, biashara hii imevutia wawekezaji ambao kwa pamoja (wakubwa na wadogo) wanaTRADE zaidi ya US Dollars Trilioni 5.3 kila siku!
  4. Hii biashara kwa kuwa ni ya mtandaoni, ukitaka kuifanya ni lazima uwe na fedha mtandaoni. Unafungua account mtandaoni kama unavyofungua bank, unaweka fedha zako. Unazifanyia biashara na siku ukitaka kuzitoa, unazitoa mtandaoni zinakuwa cash za kutumia.
  5. Biashara hii, kwa kuwa ni ya mtandaoni, unaweza kuifanyia popote! Nyumbani, chumbani, njiani, sokoni..popote! Unahitaji tu vitu vitatu:
    • Computer/Laptop ambayo itakusaidia kuliangalia soko na kujua muelekeo (Market Analysis) 
    • Internet connection. Kwa sababu ni biashara ya mtandaoni, unahitaji kujiung na mtandao.
    • Programu maalum yenye uwezo wa kusoma soko. Hii inaitwa Trading Platform. Hii ni software ambayo, unai~download na kui~install kwenye Computer yako. Hizi ziko nyingi sasa lakn moja maarufu ambayo inatumika sana duniani inaitwa Meter Trader 4 (MT4).

Note 1:
Ni lazima uwe na Computer/Laptop au smartphone na u-install MT4 kama unafanya Market Analysis mwenyewe lkn, kama kuna mtu mwingine anaweza kufanya kwa niaba yako na akakupa kile tunaita Trading Signal, sio lazima uwe na computer, unaweza tu ukawa na simu yako au gadget yoyote ile inayoweza kuunganishwa na mtandao. Note 2:
Baada ya kutimiza hayo, kabla hujaanza KUNUNUA NA KUUZA fedha za kigeni mtandaoni, Ku Trade Forex, unamuhitaji mtukati anayeitwa Broker. Kwanini? Nitafafanua zaidi pale chini lakini, kwa hapa niseme tu, ndiye anayesimama kama bank ya mtandaoni kwako. Utafungua account kwake kama unavyofungua account NMB, NBC, Equity, Exim, n.k. Utampatia taarifa zako zote rasmi, Vitambulisho vyote muhimu, Uraia, Anuani ya unapoishi,...kila kitu. Ndipo atakuruhusu kufungua account ya mtandaoni. Niwaonye wanaopenda kudanganya, hapa usijaribu, utafeli. Hapa wanahitaji taarifa zako halisi na sahihi. Hii ni kwa sababu, hii ni biashara halali kabisa, na ni ya dunia nzima na, inakupatia kipato halali. Sasa, siku umepata faida unataka kuzitoa pesa zako, watakuambia hatukupi maana si wewe, endapo utawasilisha utambulisho mwingine tofauti na ule uliojazaga. Baada ya kuifungua account kwa Broker, unaweka hela zako humo, labda USD, GBP, JPY..utakavyo mwenyewe.

Baada ya hapo, sasa upo tayari kuanza biashara.

Forex ni nini?


Katika kuanza biashara ya Forex, jambo kubwa na la muhimu ni kuhakikisha una trade kupitia broker ambaye yupo regulated, na anaaminika zaidi ili kuepuka matatizo mbali mbali yanayotokana na ku trade kupitia broker asiye na sifa.

Bofya link ifuatayo kutengeneza account kupitia broker anayeheshimika zaidi duniani na mwenye clients zaidi ya 2 milion kutoka nchi mbali mbali duniani ikiwemo Tanzania na Kenya na nchi zote za Afrika Mashariki.

BOFYA HAPA KUFUNGUA ACCOUNT


Zinazosomwa Zaidi

Followers